Mbunge wa Misungwi acha kutumia mabavu

Syston

JF-Expert Member
Nov 6, 2017
229
500
Naandika uzi huu kwa masikitiko sana. Mheshimiwa kabla ya kuwa mbunge alikuwa mkuu wa mkoa Manyara. Wakati huo alifanya ujenzi na akampa kazi ya nondo kijana mmoja pale Misungwi. Yuke kijana alipata loss akashindwa kumaliza ile kazi. Cha kusikitisha ni kuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa wakati huo aliagiza askari wa mkoa Mwanza kuweka kufuli katika ofisi za kijana yule.

Pale Misungwi kuna kituo cha Polisi lakini mheshimiwa alitumia cheo kuagiza askari wa mkoani. Kijana yule ana mke na watoto wanamtegemea unapomfungia ofisi unamaanisha nini?

Kama unamdai njia pekee ya kukulipa ni akifanya kazi we unatumia kiburi na jeuri ya madaraka kumfungia ofisi.

Halafu bila aibu ukarudi kuomba kura za ubunge hapohapo. Hii kupita bila kupingwa ni dhuruma kubwa iliyotesa watu wengine.

Kama Mbunge unawafanyia hivyo watu wako itakuwaje kwa watu baki? Ndio tunajua vijana wana changamoto zao lakini wewe yule ni kama mdogo wako. Familia zenu zina historia na isitoshe enzi unakaa vijiweni hao ndio vijana waliokupa kampani.

Badilika nisiandike sana nikakutukana maana unakera sana.

Mbunge gani unamfungia ofisi mtu kisa unamdai tena jimboni kwako.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
97,852
2,000
Naandika uzi huu kwa masikitiko sana. Mheshimiwa kabla ya kuwa mbunge alikuwa mkuu wa mkoa Manyara. Wakati huo alifanya ujenzi na akampa kazi ya nondo kijana mmoja pale Misungwi. Yuke kijana alipata loss akashindwa kumaliza ile kazi...
Ndiyo mkome kuburuzwa na kudanganywa kwa kofia na t-shirt za mbogamboga
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
97,852
2,000
Kama kazi huiwezi unachukua ya nini? Vijana acheni tamaa. Alivyoona kazi ni ya mkuu wa mkoa akajua pesa itakua inatoka tu kila anapotaka. Kila mtu anatafuta hela kwa jasho na ana uchungu nazo. Badala ya kulia lia hapa ungesema sababu zilizomfanya ashindwe kumaliza kazi aliyopewa.
Ccm ni janga la kitaifa
 

butron

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
1,427
2,000
Kwani ingekuwa wewe unajenga halafu fundi hakumaliza kazi,hela kala ungemchekea tu?
Ningekuwa mimi ndiyo Mbunge husika KWA kuzingatia heshima niliyopewa na jamii yangu na kwa kuzingatia miongozo ya kimaadili KWA kiongozi;ningemshitaki mahakamani!
Una swali jingine?
 

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
532
500
Huwezi kuitenganisha sisiemu na uonevu

Kwa id yako sipotezi muda wangu kubishana na wewe mkuu
Ni kwa sababu huna cha kubishania. Hivi wewe ukimpa fundi hela akala na kushindwa kumaliza kazi utamchekea tu. Labda kama hujawahi kujenga. Kuna mafundi hua wanafikiri hela kwa bosi zipo tu haziishi. Mwambieni ndugu yenu arudishe hela kama kazi imemshinda sio kuja kulia lia hapa
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
97,852
2,000
Ni kwa sababu huna cha kubishania. Hivi wewe ukimpa fundi hela akala na kushindwa kumaliza kazi utamchekea tu. Labda kama hujawahi kujenga. Kuna mafundi hua wanafikiri hela kwa bosi zipo tu haziishi. Mwambieni ndugu yenu arudishe hela kama kazi imemshinda sio kuja kulia lia hapa
Huna hoja wewe Matonya wa ccm
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom