Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,692
- 218,210
Kauli hiyo ya kishujaa ameitoa ndani ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akichangia kwenye bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu
Pamoja na hilo pia amependekeza umuhimu wa kuwa na Tume huru ya uchaguzi , ambapo amedai kwamba pamoja na yeye kushinda kwa kishindo kwenye nafasi ya ubunge kwa uchaguzi wa 2010 na 2015 lakini kabla ya matokeo kutangazwa kwa mbinde kulitokea mauaji ya mtu mmoja na ulemavu kwa watu watatu ambao anawahudumia hadi leo
Note : Tunashindwa kuweka video hapa kwa vile bunge la Tanzania limedhibitiwa na linaendeshwa kama vikao vya siri
----
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ ametaka sheria za uchaguzi zibadilishwe ili matokeo ya urais kupingwa mahakamani kama ilivyo kwa ubunge.
Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 2, 2020 katika mjadala wa bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2020/21.
Sugu ambaye pia ni mwanamuziki amesema mbali na matokeo kupingwa, uwepo wa tume huru ya uchaguzi utafanya uchaguzi uwe huru na haki.
“Mbeya hamjawahi kunipa ushindi kwenye silver plate, mwaka 2010 alikufa mtu mmoja kwa ajili ya kulinda kura, uchaguzi wa mwaka 2015 walemavu watatu hadi leo bado nawahudumia.”
“Kwa hiyo tunataka tume huru yenye uwezo wa kuchagua wasimamizi wake na watumishi wake yenyewe ila isiteuliwe,” amesema Sugu.
Mwananchi