Mbunge wa CCM atelekeza wa wananchi-Ukonga waishi kama hawana Mbunge

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WAKAZI wa Kata ya Kivule, jijini Dar es Salaam, wamelalamikia kitendo cha madereva wa daladala kuwatoza wanafunzi sh. 300 kwa kisingizio cha ubovu wa barabara.

Wakizungumza katika kikao cha kuchangia ununuzi wa Kivuko cha Kipunguni Mtaa wa Mara Picknic kilichoitishwa na Diwani wa Kivule, Nyansika Gaitama, wakazi hao walisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza kusababisha wazazi kushidwa kupeleka watoto wao shule.

Kutokana na hali hiyo, mmoja wa wakazi hao Mwalimu Mulokozi aliitaka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), kupeleka watendaji wake huko ili kujionea hali halisi badala ya kubaki maofisini.

Katika uchangishaji wa kivuko, jumla ya sh milioni 3.6 zilipatikana ambapo kati ya hizo Diwani alichangia sh.100,000.
Diwani Gaitama alisema kukamilika kwa kivuko hicho kutawezesha barabara hiyo kupitika hadi kipidi cha mvua.

Hata hivyo, alisema zinahitajika sh milioni 11.6 ili kukamilika kwa ujenzi wa kivuko hicho ambapo alitoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia.

Wananchi wa Ukonga wamekuwa kwa muda mrefu wakipata matatizo makubwa kutokana na miundombinu mibovu ya barabara kiasi kwamba katika nyakati za mvua hususan masika nauli ya daladala imekuwa ikifika hadi shilingi 1000 kwa safari moja.Mbali ya kivule maeneo mengine yanayoathirika na hali hii kwa ubovu wa barabara ni Mombasa kwenda Moshi bar hadi kwa Mkolemba, Mombasa hadi kwa diwani banana kwenda Machimbo na banana hadi kitunda.

Pamoja na malalamiko ya muda mrefu lakini mbunge wa jimbo hilo mwanamama Eugene Mwaiposa amekuwa hachukui hatua yoyote hata ya kuzungumza na wananchi wake kiasi cha kulifanya jimbo hilo kuwa hatarini kupokonywa mikononi mwa CCM

Source:Tanzania Daima.
 
Hakika hii habari imenisikitisha sana.Inashangaza kama kweli haya mambo yanatokea katika majimbo ya Dar.Inabidi wahusika wafuatilie kwa karibu.Wananchi nao wanapaswa kuwa makini hasa nyakati za uchaguzi.Baadhi ya wabunge wamekuwa ni walilia posho tu kama huyu
 
Hakika hii habari imenisikitisha sana.Inashangaza kama kweli haya mambo yanatokea katika majimbo ya Dar.Inabidi wahusika wafuatilie kwa karibu.Wananchi nao wanapaswa kuwa makini hasa nyakati za uchaguzi.Baadhi ya wabunge wamekuwa ni walilia posho tu kama huyu

Mkuu hata mimi hii habari inanusikitisha sana
 
Nadhani wanaopaswa kulaumiwa ni wananchi wenyewe kwa kujiruhusu kuendelea kufanya makosa ya kuchagua watetea posho badala ya maslahi ya wananchi. Hayo hayo makosa wayarudie tu ifikapo 2015!!!!!
 
Nadhani wanaopaswa kulaumiwa ni wananchi wenyewe kwa kujiruhusu kuendelea kufanya makosa ya kuchagua watetea posho badala ya maslahi ya wananchi. Hayo hayo makosa wayarudie tu ifikapo 2015!!!!!

Mkuu wangu uliyosema ni ukweli mtupu
 
Niwapongeze wananchi wa kivule kwa kujitolea kujiletea maendeleo, kwani ccm haijawahi kuwa na mpango wa kutumia kodi zetu kutuletea maendeleo, hasa ujenzi wa miundombinu ambayo ni kazi ya serikali yoyote ile duniani.

Huyu mbunge wetu ametu disappoint kwa kiasi kikubwa sana, haonekani kujali maslahi ya wananchi.

Wakati wa mafuriko ya mwezi december mwaka jana, ambapo mawasiliano ya barabara kati ya mongolandege na ulongoni yalikatika huyu mama hakuonekana hadi vyombo vya habari viliporipoti wananchi wakimuulizia mbunge wao aka yupo nchini ama amesafiri nje ya nchi ndipo akajitokeza kutembelea daraja la msimbazi/mongolandege.

Hata ukiwasikiliza wanaccm wenzake wamemchoka, wanatamani miaka hii mitano iishe haraka waachane nae. Kwakweli sijafahamu huyu mama anafanyia wapi kazi zake za kibunge.
 
mh mbunge anamalizia posho zake, maana magamba wanao taka nafasi yake ni wengi kamuachia meya wa ilala afanye kazi, naye anahisi akitengeneza wananchi watajua mbunge ndio katengeneza, na jery slaa naye anafanya nn
 
Hii habari ni ya kweli kabisa kwani hata mie ni mmoja wa wakazi wa maeneo hayo na kinachosikitisha sana, na Mbunge mkimwita na kumwambia anatoa majibu ya hovyo sana, kweli ni aibu.
 
Back
Top Bottom