Mbunge wa Arusha Mjini, kikao kijacho cha Bunge usisahau kufuatilia kiwanda cha General Tyre

Kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre kiliwahi kuwa na mchango mkubwa sana katika uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla.

Kili generate ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Shughuli za kiuchumi zilichangamka kiasi chake.

Baada ya kusimamishwa shughuli zake mkoa umepata pigo kwa kweli kwani shughuli za kitalii nazo ni za msimu.

Namkumbusha tu mbunge wa Arusha mjini , akifika bungeni kikao kijacho asiache kuulizia serikali kuhusiana na kukifufua kiwanda hiki.
Bado kikao cha bunge hakijafika umkumbushe mbunge wako?
 
Mambo bado aisee.

Ila tutatoboa tu.
Tatizo ya nchi hii tunawakombatia sana importers,kwenye bidhaa zao
We unafikiri general tyre kingesimama
Haya mataili ya kibweg toka China yangeuzika
Maana general tyre ilikuwa taili imara
Sana

Ova
 
Kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre kiliwahi kuwa na mchango mkubwa sana katika uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla.

Kili generate ajira nyingi za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Shughuli za kiuchumi zilichangamka kiasi chake.

Baada ya kusimamishwa shughuli zake mkoa umepata pigo kwa kweli kwani shughuli za kitalii nazo ni za msimu.

Namkumbusha tu mbunge wa Arusha mjini , akifika bungeni kikao kijacho asiache kuulizia serikali kuhusiana na kukifufua kiwanda hiki.
walikiamishia kenya kina late kigoda ,mkapa na kina shalukhan
 
Gambo hata huko Muriet kwa wanyonge amehama kahamia kwa makabaila wenzake Njiro. ....hakuna jinsi mtatoboa
Hicho kiwanda kitarudi tu kwa uwezo wa Mungu.

Ila bado hata huko njiro ni ndani ya jimbo lake.

Ingawa ni kwa makabaila na mabwanyeye.
 
Mambo yanabadilika ni vema tukajiuliza, tuna comparative advantage ? Au tuangalie ni viwanda vipi tunahitaji zaidi

Mfano usindikaji wa vyakula au ngozi ambavyo wakulima wanavyo na vinaozea mashambani na kuwakatisha tamaa.

Kwahio kama tuna comparative advantage basi na kijengwe kama ndio vile tena basi tuangalie kwenye tija
 
Hicho kiwanda kitarudi tu kwa uwezo wa Mungu.

Ila bado hata huko njiro ni ndani ya jimbo lake.

Ingawa ni kwa makabaila na mabwanyeye.
Labda kiuzwe kwa bwanyenye. Hii serikali haina uwezo wa kukifufua.

Wambie viongozi wa Arusha wajenge barabara za lami. Jiji lote halina lami mitaani zaidi ya hapo mjini kati! Hata Moshi imewaacha mbali sana kwenye ujenzi wa barabara
 
Labda kiuzwe kwa bwanyenye. Hii serikali haina uwezo wa kukifufua.

Wambie viongozi wa Arusha wajengw barabara za lami. Jiji lote halina lami mitaani zaidi ya hapo mjini kati! Hata Moshi imewaacha mbali sana kwenye ujenzi wa barabara
Arusha tunaonewa sana kwakua sasahivi hatuna kiongozi mwenye ushawishi wa kisiasa kama hapo zamani.
 
Back
Top Bottom