Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Hali ya afya ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari, si nzuri na mchana huu anasafirishwa kwenda India kwa matibabu. Sumari ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, alianza kuugua hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambako baadhi ya maeneo alilazimika kusaidiwa kampeni. Tunamuombe Mungu ampe afya njema arudi kujenga Taifa.
Taarifa ni kwamba amepata tatizo kubwa katika ubongo wake ambako madaktari wamegundua kitu kilichoota ndani ya kichwa, kitu ambacho kinaathiri ubongo wake kiasi cha kupoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili wake. Sumari ambaye alilazimika kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anaondoka leo kwa ndege ya Oman Air.
Iliwahi kuzungumzwa hapa, japo baadhi yetu tulijadili bila utu. Tujaribu kuweka ubinadamu mbele, siasa baadae.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mbunge-wa-arumeru-mashariki-ni-mgonjwa.html