Mbunge Sumari azidiwa, anapelekwa India leo

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Hali ya afya ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari, si nzuri na mchana huu anasafirishwa kwenda India kwa matibabu. Sumari ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, alianza kuugua hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambako baadhi ya maeneo alilazimika kusaidiwa kampeni. Tunamuombe Mungu ampe afya njema arudi kujenga Taifa.

Taarifa ni kwamba amepata tatizo kubwa katika ubongo wake ambako madaktari wamegundua kitu kilichoota ndani ya kichwa, kitu ambacho kinaathiri ubongo wake kiasi cha kupoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili wake. Sumari ambaye alilazimika kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anaondoka leo kwa ndege ya Oman Air.

Iliwahi kuzungumzwa hapa, japo baadhi yetu tulijadili bila utu. Tujaribu kuweka ubinadamu mbele, siasa baadae.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-mbunge-wa-arumeru-mashariki-ni-mgonjwa.html
 
Ona sasa, huyu yuko taabani tangu mwaka jana, lakini posho ya mafuta analipwa kila siku!
 
Mungu amponye haraka ugonjwa unaomsumbua, ila nadhani atakuwa kama taahira!
 
Ubinadamu mbele namtakia asafiri salama na Mwenye enzi Mungu ampe baraka apone na kurudia afya yake. Masikini watu wa jimbo lake wamekaa miezi mingi bila mwakilishi wao kufika bungeni, hata kule kluapishwa tu, sijui CCM yetu ilianfgalia wapi ikachagua mgombea mgonjwa!! Ushauri wa bure, akipata nafuu ajiuzuru ubunge kutoa nafasi uchaguzi kurudiwa na wengine wagombee na kuwapa uiwakilishi wananchi.
 
Ugua pole baba.
Kumbe tangu kipindi kile hajawahi kupona!?
Dah pole sana.
 
Mungu amponye mzee Sumari!Naomba kujulishwa kama huyu mheshimiwa aliwahi kuapishwa kwenye bunge hili la Makinda..!
 
kama alichaguliwa halali na wananchi wake mungu amjalie apone haraka,kama aliiba kura kama walivyozoea na chama chake mungu amuwaishe mbinguni akajibu kesi yake
 
Hali ya afya ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari, si nzuri na mchana huu anasafirishwa kwenda India kwa matibabu. Sumari ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, alianza kuugua hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 ambako baadhi ya maeneo alilazimika kusaidiwa kampeni. Tunamuombe Mungu ampe afya njema arudi kujenga Taifa.

Taarifa ni kwamba amepata tatizo kubwa katika ubongo wake ambako madaktari wamegundua kitu kilichoota ndani ya kichwa, kitu ambacho kinaathiri ubongo wake kiasi cha kupoteza mawasiliano na sehemu nyingine za mwili wake. Sumari ambaye alilazimika kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anaondoka leo kwa ndege ya Oman Air.

Iliwahi kuzungumzwa hapa, japo baadhi yetu tulijadili bila utu. Tujaribu kuweka ubinadamu mbele, siasa baadae.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-
siasa/149200-mheshimiwa-mbunge-wa-arumeru-mashariki-ni-mgonjwa-3.html

Tunashukuru kwa taarifa yako, na tumwombee Mungu amjalie afya njema arudi kuliwakilisha jimbo lake na kuendelea utumishi wake kwa taifa.

Tofauti za kiitikadi si chuki kama wengi wetu tulivyozoea kuziendesha hapa, tunashindana kwa hoja ndio maana ya demokrasi, lakini wakati huo huo tunatakiwa kudumisha utu na upendo kati yetu ndiyo silaha kubwa ya kutunza amani katika nchi yetu.
 
Ubinadamu ni jambo jema, hasa kwa sisi Watanzania ambao hulka zetu za ukarimu na upamoja ni za jadi yetu. Akipona tuanze madongo yetu na kumtaka aeleze, alivyowatumikia wapiga kura wake.
 
Japo magamba siwapendi lakini kama binadamu tunamtakia heri apone haraka aje kutekeleza ahadi alizo ahidi kwenye kampeni.

Pipoz power!
 
Pole sana na tunakuombea nafuu ya haraka ili urudi kuendelea na majukumu yako.
 
Sawasawa kabisa, hospitali za India kwa sasa ndio zimekua hospitali zetu kubwa za rufaa! Why not? Tuko busy na kuponda hela kusherekea miaka 50 ya uhuru, hatuna pesa za kurekebisha na kununua vifaa vya kisasa Muhimbili, sisi sio wajinga bwana, we know what we are doing!
 
Back
Top Bottom