MBUNGE: POLISI wameshaninyang'anya JIMBO langu...

Labda niwasaidie kidogo, ripoti za kiinteligensia za kinafiki zimemponza. Miscalculation ni hatari sana sana. Hii intelinsia yetu ni mbovu kuliko ya makaburu.
 
[

Ama kweli ukizeeka sana huogopi chochote zaidi ya kifo na kwa bahati mbaya nacho hakikwepeki.[/QUOTE]

Hahaha nimeipenda hii mkuu
 
Mwambie aende akagombee Maiti Ya Huyo kijana aliyefariki jana ili aweze kujipambanua yeye ni Bingwa wa Kuwazika watu!! Ila kutoa madawa na vitu Vingine Mahosipitalini ili kuokoa maisha haoni Umuhimu!! Kalagabao!!
 
Mbunge yuko sahihi. Kila siku serikali inawasaidia Chadema kupata wanachama kurokana na presha zao. Hivi ikiwa watu wanaandama barabarani huku hawana silaha yoyote isipokuwa mabango na wengine wamebeba magazeti kama marehemu comredi Ally alivokutwa, kwa nini kuwazuia hadi kwa kufyatua bunduki.
Kama wangewasaidia ili waandamane vizuri ingekuwa na hasara gani kwao?
Hivi kwa kufyatua bunduki na kuua raia kumewasaidia nini zaidi ya kujenga chuki kwa wapiga kura wa mheshimiwa Abood?.

Ama kweli ukizeeka sana huogopi chochote zaidi ya kifo na kwa bahati mbaya nacho hakikwepeki.

Bahati mbaya waliwatumia polisi wa kutuliza ghasia badala ya polisi wa usalama barabarani ambao wamefundishwa kuelekeza magari na waenda kwa miguu. Hawa jamaa wa FFU kazi wanayojua wao ni moja tu ya kutuliza ghasia. Wakikuta hakuna ghasia wanaianzisha wao ili wasije wakarudi kikosini bila kukamilisha kazi waliyotumwa kufanya.

Ushauri wa bure kwa jeshi la polisi: Kwenye maandamano ya amani tumieni askari wa usalama barabarani watafanya kazi nzuri zaidi. Hawa FFU watumieni kwenye kazi za usiku za ukorokoroni.
 
Huyu kwanza si yule aliyekuwa na kashfa ya kuzika wahanga wa ajali la basi lake la ABOOD pale MDAULA kuficha kashfa ya mabasi yake ya ajali dhidi ya mshindani wake HOOD.Atulie

Yaani mkuu umenitonesha kidonda kabisa. Yaani alizika maiti na wale walioumia aliwapeleka dispensary za uchochoroni na kuwahonga ila tu wengine walipoteza maisha baadaye na wenngine vidonda septic wakakatwa miguuu. Cha kusikitisha polisi walijua na ile habari ikaripotiwa mara moja tu vyombo vya habari halafu ikapotea. Mfisadi na mnyama mkubwa huyu halafu eti ndiye aliyeonekana na merits za kupewa ubunge na SSM. Kweli SSM ina mashaka na viongozi wake. So dhaifu!
 
Kutumia nguvu kwa CCM ni mtaji wa CDM, maana kwa kufanya hivyo ndio wanazidi kuwaongezea hasira wananchi na kupandikiza roho ya chuki na visasi.
 
Back
Top Bottom