Mbunge Musukuma na Usomi phobia, kutokusoma siyo sifa!!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
17,547
Reaction score
28,494

Mbunge machachari Msukuma ana upeo mkubwa wa kuongea na kuongea.

Lakini wakati mwingine kinachomtoka mdomoni ni pumba zisizo ainisha mantiki ya usomi nyuma yake.

Huwa anawa nanga sana wasomi, utaifikiri mikakati ya mwalimu Nyerere kufuta ujinga ilikuwa kupoteza muda na fedha.

Msukuma namshauri afute shule zote jimboni mwake ili watu wake wawe madereva wa mabasi na malori na makondakta , kama yeye.

Juzi Bungeni kawananga wazee, Wakurugenzi na Wenyeviti wa Bodi, ati wazee.!!
Hilo ndilo kosa la kukosa usomi!
Experience(uzoefu) na elimu ndiyo pinnacle ya uongozi.

Huwezi muweka kijana wa UVCCM kuongoza Bodi, ile siyo kazi ya mtulinga, ni kazi ya ushauri unaotokana na uzoefu.

Mbunge Msukuma ajifunze kuwa na kiasi na kujiwekea speed governor ya mdomo.
 
Umuhimu wa Elimu utabaki kua na umuhimu wake mpaka mwisho wa Dunia,
Huwezi kuibeza Elimu ikiwa magari anayoendesha,Simu anayoitumia,Ndege anazopanda akisafiri ni matokeo ya Elimu,

Siku akiumwa hawezi kukubali kutibiwa na Dokta asiye na elimu,Mwenye elimu hawezi kua sawa na asiye na elimu hata kama aliye na elimu ni masikini na asiye na elimu ni tajiri,

Utofauti wetu kwenye hii Dunia ndio unaifanya Dunia ya leo kua hivi,huwezi kuidharau Elimu kisa umefanikiwa kimaisha kwa kununua assets ambazo ni matokeo ya elimu,hata Nyumba anayoishi,kitanda anachokilalia,Tv anayoiangalia,nguo anazozivaa,viatu anavyovivaa ni matokeo ya Elimu.
 
Hilo ni kweli, hasa kwa wasukuma!
 
Umepiga mule mule, ELIMU itabaki kuwa ELIMU.
 
Msukuma na Kishimba hawabezi elim,Bali wanabeza aina ya elim inayotolewa!!

Kifupi tumechelewa sana!

Elimu ya Sasa ni utumwa wa kuajiriwa ,usipoipata ajira ujue kabisa Elim yako itabaki kuwa makaratasi coz haijui kutafuta pesa kwa matumizi ya kila siku!!

Huwezi kujisifu kuwa na elim ya kutosha kama ajira pekee ndio hitimisho la elimu yako!

Elimu inapaswa kutawala asili na sio asili kumtawala msomi!!
 
Kuna mtu huko kakwambia , Msukuma na Kishimba kwa vile wamefanikiwa kifedha basi wanafikiri wao ni wajanja kuliko wasomi wote.
Basi, wakajitibu na miti shamba wakiumwa na wasiwaajiri wahandisi kuwajengea nyumba.
Na wote wanatoka sehemu moja, wafundishe wengine siri za kupaa na helikopta zao za Gamboshi kutoka Mwanza hadi Dodoma Bungeni.
 
Wasomi wenyewe kama ndiyo wa aina ya kina Kabudi, Mkumbo, Nchemba, Bashiru, Mwambegele, Mutungi, Mwanga na mazafakas wengine kama hao, ni vigumu sana kuona thamani ya usomi.
 
Wasomi wenyewe kama ndiyo wa aina ya kina Kabudi, Mkumbo, Nchemba, Bashiru, Mwambegele, Mutungi, Mwanga na mazafakas wengine kama hao, ni vigumu sana kuona thamani ya usomi.
Bado ni ujinga uliokithiri kudharau usomi wakati mwenyewe una ufinyu wa usomi huo.
Akili inakuambia elimika na wewe uonyeshe mwenyewe utofauti wa usomi unaoutaka.
Jawabu lake haliko katika kutokusoma kabisa na uwe mbumbumbu asiyejua tofsuti ya mwanga na jua.
 
Hana maana hiyo though. Anawapa challenge wasomi waoneshe thamani ya usomi wao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…