Mbunge Musukuma acha kiherehere cha kutusemea watu wa Kanda ya Ziwa

Afanye siasa lakini hasituingize watu wa kanda ya ziwa kwenye agenda zake binafsi za kisiasa na ukabila wake. Kwa bahati nzuri yeye ni mbunge kwanini asizungumze kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake hadi atuhusishe wananchi wote wa kanda ya ziwa,?
Hahahahaaa... Mkuu, hamtaki kuhusishwa katika hili?
 
Mbunge msukuma sisi wakazi wa kanda ya ziwa hatukukutuma na hatujawahi kukuchagua kuwa msemaji wetu kwa jambo lolote.

Sisi wazee na watu wa kanda ya ziwa hatukukutuma kusema hayo unayoita mapigo ya kumjibu Antony Diallo na kama ulikuwa na nia ya kujibu mapigo ungemjibu kwa utashi wako au kwa niaba ya wananchi wa jimbo lako la geita vijijini lakini sio kutuhusisha watu wa kanda ya ziwa kwenye maugomvi yako binafsi na kusema kwamba sisi ndio tumekutuma ukatusemee.

Sisi wazee wa kanada ya ziwa ni watu wenye busara na hekima, kama kuna jambo linaenda ndivyo sivyo tuna njia zetu za kuwasilisha maduku duku yetu ikiwemo kujisemea wenyewe na sio kutuma kijana mropokaji kama wewe.

Kuhusu kifo cha hayati magufuri unasema tuliofiwa ni watu wa kanda ya ziwa. Kimsingi hii ni kauli ya kijinga kabisa kutolewa na kiongozi wa wananchi kama wewe kwa sababu Rais magufuri hakuwa Rais wa kanda ya ziwa bali alikuwa ni Rais wa watanzania wote wa kanda za mikoa yote nchini. Sasa unaanzaje kusema kwamba tuliofiwa ni watu wa kanda ya ziwa pekee?

Huoni kama kauli yako inalenga kutugawa watu wa kanda ya ziwa na watu wa kanda zingine?

Kwa mara nyingine mbunge msukuma usituhusishe tena wazee na watu wa kanda ya ziwa kwenye ugomvi wako binafsi wa kutafuta umaarufu wa kisiasa na sifa za kishamba na UKOME kabisa kutusemea kwa sababu hata sisi tuna midomo ya kujisemea.

Message sent & delivered
Wewe utakuwa mchagga sio Bure
 
Nafikiri wanaosema Msukuma hastahili kuisemea Kanza ya Ziwa wapo sahihi kabisa hasa kwa vitu mbavyo hakutumwa. Moja pili je hiyo kanda ya ziwa hukutana lini na katika forum ipo inayojulikana kikatiba katiba inatambua Mkoa na sio kanda sasa sijui kuna NGO au chama kinachowakilisha kanda ya Ziwa? Je sera zake na je kimesajiliwa na Wizara ya mambo ya ndani? au ni kusadikika tu? Je uongozi huo wa kanda hiyo pendwa unajulikana kisheria? na wanamsemaji wao ambae ndio Msukuma? Wasukuma amkeni mtatumiwa na hata ambao sio wasukuma na kujifanya wasukuma ili kujipatia uongozi. Tafakari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom