Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,501
- 9,279
Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Malapo amesema elimu ya Tanzania inaathiriwa na matamko ya kisiasa.
Tunza ameyasema hayo jana Jumatano Mei 5, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Amesema kubadilisha mtaala kufanyike kwa utulivu kwa kusikiliza wadau wa elimu wakiwemo wataalam wa elimu.
“Mara nyingi elimu yetu inaathiriwa na matamko ya kisiasa. Wakati mwingine mwenye madaraka akiamka asubuhi anatamka bila kufuata ushauri wa wataalam,” amesema.
Amesema kubadili mtaala sio suala la siku moja na kwamba wanatakiwa kufanya utafiti mfumo uliopo kama haufai na kama haufai kiongezwe nini katika mitaala hiyo. Tunza amesema pia maandalizi ya walimu yanatakiwa ili waweze kufundisha.
“Kinachofanyika sasa walimu wa ngazi ya cheti wanachofundishwa sio tunachotaka wanafunzi wafundishwe. Tuangalie tumetoka wapi tunaenda wapi? Tuache mihemko, tuwatumie wataalam tuepuke siasa,” amesema.
Chanzo: Mwananchi