Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
MBUNGE MASACHE AOMBA ONGEZEKO LA BAJETI YA BARABARA
Aprili 16, 2025
Mbunge wa jimbo la lupa Mhe. Masache Kasaka ameomba serikali kuongeza bajeti ili kufanya ukarabati wa barabara za kuingia katika vitongoji.
Sambamba na hilo Mhe. Masache Kasaka amempongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vyema maendeleo ya sekta mbali mbali na utekelezaji wa miradi ikiwemo miradi ya afya, maji, elimu pamoja na upatikanaji mzuri wa mikopo ya asilimia kumi kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalum ( walemavu).
Mhe. Masache Kasaka ametumia wasaa huo kuomba wananchi kuendelea kumpa imani na kura za kishindo Dkt Samia Suluhu ifikapo oktoba 2025.
SAMIANAMASACHE
CHUNYAKAZINAUTU
TUNASONGAMBELE