Mbunge Mariam Kisangi agawa vitendea kazi kwa UWT ngazi ya kata hadi mkoa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

MBUNGE MARIAM KISANGI AGAWA VITENDEA KAZI KWA UWT NGAZI YA KATA HADI MKOA

Atoa Jumla ya Viti vya Ofisi 214, Meza 107 pamoja na Majiko ya gesi 350.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es salaam (UWT) Mhe. Mariam Kisangi leo tarehe 25 Oktoba, 2023 amewezesha vitenda kazi kwa Ofisi za UWT kwa kata zote 102 Mkoa wa Dsm, Wilaya 5 pamoja na Ngazi ya Mkoa yenyewe.

Mhe. Kisangi ametoa jumla ya Viti 214, Meza 107 pamoja na majiko ya gesi 350 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa PTA ndani ya Viwanja vya Sabasaba.

Katika Hafla hiyo, Mgeni rasmi alikuwa Ndugu Abbas Mtemvu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam ambaye ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mhe. Kisangi kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake sambamba na Ilani ya CCM ilivyoelekeza katika kuwawezesha Viongozi wa Jumuiya anayotokana nayo pamoja na Wanawake wote Mkoani Dsm.

Ameendelea kumoongeza kwa kuonesha Uongozi wenye uhtubutu, ukarimu, usikivu na kujitoa wakati wote katika kuyasemea yale yote yanayoendelea kutekelezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye Mhe. Kisangi amewataka Wanawake wote kuendelea kuwa na Umoja, Upendo na mshikamano na kutembea vifua mbele katika kumnadi Rais Samia kwa mazuri anayoendelea kuyafanya haswa katika kuwezesha Wanawake.

"Wanawake ndio jeshi la Mama Samia, tuwe mstari wa mbele katika kumnadi Rais wetu Mama yetu kipenzi Mhe. Dkt. Samia kwani ni Mwanamama anayejiamini na kuwathamini Wanawake wote nchini na kwa kudhiirisha hilo aliamua kuunda Wizara mpya ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum hii yote ni katika kuhakikisha kunakuwa na tija kubwa katika uwezeshaji wa Wanawake, lazima tumpongeze na kuendelea kumuunga mkono" Alisema Mhe. Kisangi.

Aidha, Mhe. Kisangi amempongeza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Cde. Jokate Mwegelo kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM na kumtakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

#UgawajiVitendaKazi #UWTJeshiKubwa
#CCMImara #KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.02.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.02.jpeg
    52.3 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.03.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.03.jpeg
    58.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.06.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.06.jpeg
    52.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.08.jpeg
    51.7 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.08(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-10-26 at 12.03.08(1).jpeg
    46.9 KB · Views: 1
ni huyu huyu mariam kisangi ,alietufundisha shule ya msingi rangi tatu 2005 nakumbuka kipindi kile alikuwa mwalimu mkuu,tulipo maliza shule alitupa hela kila mwanafunzi aisee tunampenda sana ana upendo mwingi,alikuwa mwalimu mkuu lakini alikuwa anakuja kutupiga pindi,ila baadae tulisikia amepata ubunge kwenye utawala wa kikwete
 
Back
Top Bottom