Mbunge Malocha ahutubia Wananchi dhidi ya Mwekezaji; Wateketeza Matrekta ya shamba la Kanisa Efatha

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Aug 19, 2012
145
28
mbunge huko sumbawanga amehamasiha watu kuchoma moto KANISA,GHALA LA MAHINDI,NYUMBA NA MATREKTA chanzo ITV wenye taarifa kamili tunaomba mtujuze hapa jf.
 
ndugu yangu hii ni breaking nyuzi, sasa saa tano hii wengi hawajalala kweli? Nami nasubiri habari hii
 
Mbunge wa chadema ambae alishinda kesi ya uchaguzi sumbawanga....chadema kama uamsho
 
Sumbawanga wana mbunge au? nafahamu hawana baada ya aliyekuwa mbunge kushindwa rufani. Weka taarifa ya kueleweka, siyo kukurupuka!
 
huu,mzozo hauhusiana na haya mambo yanayoendelea sasa ya waumini wa dini ya kislamu kuchoma makanisa,huu ni mzozo wa cku nyingi kati ya wanakijiji na kanisa la efatha,la mchungaji mwingira,kuchukua eneo kubwa na kuweka uzio ambapo hata wanakijiji wanakosa mahali pa kupita!na ndio yale yale mambo ya kuchukulia mambo kidhaifu,bila kutafuta suluhisho la kudumu.
 
huooo ni uzushi hakuna kanisa lilochomwa moto sumbawanga......nimempigia anko wangu kaniambia hakuna kitu kama hichooo acheni uzushiii
 
(PICHA, HABARI NA JOSHUA MWAKABUNGU WA FULLSHANGWE SUMBAWANGA)
……………………………………………….
Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.

Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.

Kamnda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani
DSC06984-1024x684.jpg

Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.

DSC06985-1024x684.jpg

Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.

DSC06989-1024x684.jpg

Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba hilo.
 
Ni Matunda ya FREE MARKET? Kubadilisha Siasa za NCHI bila kuwahusisha Wananchi? Wachache kuwa na MALI na Kutajirika?
 
Hivi kama kweli kanisa limechomwa, je hiyo ndio njia sahihi ya kutatua mzozo huo wa siku nyingi?
 
Mtume na nabii Josephat Mwingira ana mashamba makubwa rukwa,Bagamoyo ana Ephata bank! Kibwetere type!
 
SASA KWA HILI TUACHE UNAFIK, TNASUBILI TAMKO LA KADINAL AU TUTAMIN MMEPATA LA KUSEMA, AU KWA KUWA WALOCHOMA AYO MATREKTA NI WAKRISTU BASI HAMNA NOMA OW NDO INAKUA SOO, AU KUNYA LZM ANYE KUKU, AKINYA BATA KAHARISHA. ACHENI UCHOCHEZ WA DINi
 
Back
Top Bottom