Mbunge Malocha ahutubia Wananchi dhidi ya Mwekezaji; Wateketeza Matrekta ya shamba la Kanisa Efatha

Kukojolewa kitabu chochote kile ni tabia mbaya inastahili kukemewa na yeyte mwenye akili timamu.Anayeshabikia kitend cha mtoto kufanya hivyo ana walakini na simuungi mkono.Tutumie alkili zetu sawa na si ushabiki wa kijinga ambao huzaa magonvi na uharibifu usio na sababu.

Kuhusu uharibifu wa mashamba nallo pia si tendo jema. Kiongozi wa kisiasa kuchoochea uharibifu si sawa.Haya ni matokeo ya mfumo mboovu wa uongozi wa CCM katika sera zake za ubinafsishaji.Cha kusikitisha, ingekuwa ni mashamba ya mzungu au mwarabu wangepelekwa polisi mapema lakini kwa mtanzania basi hadithi ni ileile.
to conclude, hii ni aibu kwa CCM na wapambe wao, bila ya kujali dini zao kwani ubaya hauna dini.
Asalaam aleykum
 
Hii ni kutokana na mgogoro wa ardhi, haina uhusiano na dini na hakuna kanisa lililochomwa hapo. Ni muendelezo wa chuki baina ya wawekezaji na wananchi wanaomzunguka, kama vile mgodi wa Nyamongo. Serikali inabidi iangalie upya makubaliano ya uwekezaji. Halafu nashangaa mbunge wa CCM kuitumia kaulimbiu ya "Nguvu ya Umma" kwenye mkutano wake na wananchi, ingawa yeye utekelezaji wake umesababisha madhara
 
Hakuna kanisa lililochomwa. Ni matrekta mawili pamoja na kambi ya shamba linalomilikiwa na mwekezaji ambaye ni kanisa la Efatha. Kwa ufupi ni mgogoro wa ardhi kati ya wanakijiji na mwekezaji, na mbunge wa Kwela (Sumbawanga Vijijini - CCM) alifanya mkutano siku chache kabla wananchi hawajavamia shamba. Huyu mbunge akamatwe, uchaguzi urudiwe
 
SASA KWA HILI TUACHE UNAFIK, TNASUBILI TAMKO LA KADINAL AU TUTAMIN MMEPATA LA KUSEMA, AU KWA KUWA WALOCHOMA AYO MATREKTA NI WAKRISTU BASI HAMNA NOMA OW NDO INAKUA SOO, AU KUNYA LZM ANYE KUKU, AKINYA BATA KAHARISHA. ACHENI UCHOCHEZ WA DINi
Akili yako haina akili!
 
Mtume na nabii Josephat Mwingira ana mashamba makubwa rukwa,Bagamoyo ana Ephata bank! Kibwetere type!

Watanzania bwana mna roho za kwa nini!...mkuu kama una ushahidi wa kasoro katika upatikanaji wa mali si ujulishe vyombo husika?
Kama wewe utakua ni mkristo, biblia husema anipataye mimi(Yesu , kapata kitu chema...
Nilidhani utaongelea wageni wanaochuma na kutuachia mashimo, au viongozi wanaoiba na kufilisi mashirika ya umma(wananchi).
Hayo mashamba wakati yanamilikishwa wananchi walishirikishwa na aliyeyazindua ni Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, wanachofanya hao wananchi ni yaleyale ya kuendekeza chuki za kidini.
 
ACHA UJINGA WEWE, UYO KIKOJOZ WAKO AU WENU MLOMTUMA KM ANGENASWA SIKU IYO ANGEPATA ADHABU KUBWA ZAIDI YA IYO, NAKUAPIA KM ANGENASWA LEO HII NATMAI ANGETAMAN KUWA MJUS AU CHIZI MAANA ASINGEBAKI DUNIA HII, ATA WEWE JARIBU KUIKOJOLEA, UTAOMBA HERI UWE MBWA KULIKO KTAKACHOKPATa KENGE MKUBWA WEWE

Ha ha haa sasa mkuu kubaliana na hoja ya msingi basi kuwa ukikojolea hiyo msaafu hutabadilika chochote sawasawa?
 
Hii ni kutokana na mgogoro wa ardhi, haina uhusiano na dini na hakuna kanisa lililochomwa hapo. Ni muendelezo wa chuki baina ya wawekezaji na wananchi wanaomzunguka, kama vile mgodi wa Nyamongo. Serikali inabidi iangalie upya makubaliano ya uwekezaji. Halafu nashangaa mbunge wa CCM kuitumia kaulimbiu ya "Nguvu ya Umma" kwenye mkutano wake na wananchi, ingawa yeye utekelezaji wake umesababisha madhara

ingekua bagamoyo mngesema WAISLAM,ILA RUKWA MNASEMA WANANCHI,,,,
 
ingekua bagamoyo mngesema WAISLAM,ILA RUKWA MNASEMA WANANCHI,,,,
Sasa mbunge aliwahutubia akina nani kama sio wananchi? Basi ili ufurahi, ngoja isomeke "Mbunge wa CCM awahutubia waisilamu, wachoma moto matrekta na shamba"
 


NABII MWINGIRA ALIPANGA NJAMA UHALIFU KIBAHA JUMATATU YA PASAKA!!!!!!!!!

.Fredrick summaye chaguo la Nabii Mwingira
.Nabii alisimamia kura za maoni
.Alikwa Mgeni Rasimi Uzinduzi kanisa Eftha


Bibilia inasema pasipo haki hapana amani na tena Amani na haki ni vitu mapacha!!
Haki ni tunda la Amani na utulivu katika jamii yoyote ile isiyopenda unafiki. Huwezi kulazimisha amani wakati hakuna haki na wala huwezi kutafuta haki kwa maguvu vinginevyo utasababisha kuvunjika kwa amani.

Katika Taifa letu tumeshuhudia , migogoro mikubwa ya ardhi,maandamano ya wanafunzi, wafanyakazi, na vyama vya siasa vimekuwa vinadai haki lakini vyombo vya dola wamekuwa wanapiga mabomu kuzima maandamano hayo ya kudai haki bila hata mafanikio.!!

Wapo watawala ambao wamekuwa wakipuuza maandamano ya kudai haki na vuguvugu la siasa wakidai kuwa ni upepo unaopita huku wakisahau haki inakandamizwa na hivyo wana andaa bomu la uvunjifu wa amani!!!

Siku zote katika jamii iliyochanganywa Wanyonge na Matajiri huwa Matajiri wananunua haki kwa mali walizo nazo wanateka watawala kwa misingi ya kutafuta madaraka.

Matajiri hawa wamejiimarisha kwa Ulinzi wa kutosha na kumiliki silaha . Ni kwa sababu hii mtu yoyote anayekuwa na mali nyingi utamkuta anatafuta kumiliki silaha na baadaye anatafuta kampuni ya ulinzi au anaunda kampuni ya ulinzi kulinda mali zake na ni kwa sababu hii Nabii Mwingira baada ya kujiribizia miradi Mingi yakiwemo Mashamba ya kule Mironje Rukwa na Efatha Benki aliamua kuanzosha FUNGUKA SECURITY GUARD inayo ongozwa na Brigedia General Ambrose Bayeka ambaye ndiye bodigadi wa Nabii Mwingira na amekuwa anamulinda na kupanga safu ya Wapambe safari zote za nje ya mkoa wa DSM.
Taarifa kutoka kwenye vyanzo ndani ya Jeshi la polisi vinasema Nabii Mwingira alionekana akiwa na huyo bodigadi alipo alikwa kumusimika Rais Kikwete Mwaka 2005.
Matajiri hawa wanakwenda mbali zaidi na kushika dola na watawala.

Nimelazimika kufanya utafiti baada ya kusikia maneno yaliyotolewa na Waumini wa Nabii Mwingira siku ya Jumatatu ya Paska na ujasiri wa kulitishia Jeshi la Polisi na kumukebehi IGP Mwema kuwa Wao kama Kani Efatha wana Jeshi kubwa kuliko Polisi!!!

Maneno haya hayawezi kutolewa na mtu wa kawaida isipokuwa nimeyasikia mara kwa mara ninawaombea wagonjwa wenye mapepo ambao husema ‘Hatutoki tupo wengi, tutamuua huyu mpaka mtupe ngombe”.

Utafiti wangu wa kina umebaini kuwa operation zote za kubomoa majengo yaliyo karibu na Efatha zimekuwa zikisimamiwa na Askali wastafu wa JWTZ ambao ni waumini wa Mwingira na Kwamba Mtekelezaji wa operation ni Afande LEVI KWARO (JWTZ) ambaye yupo kwenye kampuni ya FUNGUKA security iliyoundwa na Nabii Mwingira.
Taarifa kutoka kwa waumini waliokamatwa baada ya kufanya tukio hilo zinasema , mpango wote wa kuteka walinzi wa kiwanda cha afro Plus ulifanywa na Afande Kwaro na kwamba njama na maandalizi ya tukio hilo yalifanyika Kibaha Mkoani Pwani kwenye kambi ya maombi ya Nabii Mwingira.

Mpango huo ulikuwa siri na kufahamika kwa wachache akiwemo Brgedia Ambrosi, Mch Davi Mwakisole, Nabii Mwingira na Kikosi cha askali wateule wa Funguka .
Waumini hao ambao wamefichua siri baada ya kuswekwa rumande wamesema usiki kabla ya tukio hilo , Nabii Mwingira aliitisha kusanyiko la dharura na kutangaza kuwa vijana wote wenye nguvu kutoka wakazi wa DSM wapiti Mbele na akaanza kuchagua mwenyewe watu wenye Vifua vikubwa na kumukabidhi Mch Mwakisole ambaye aliambatana nao kwa kutumia basi la EFATHA Benki na kusafiri mpaka MWenge Efatha tayari kwa operation hiyo.

Waumini hao ambao walikuwa wanaongea kwa machozi wanasema kikundi hicho kilifika hapo na kujificha kabla ya kutawanywa kwenye maeneo maalumu kabla ya utekaji na kwamba hata wakati wa mapambano walizidiwa na Mwingira aliyekuwa anafuatilia kwa makini tukio hilo alijulishwa na kuchanganyikiwa.

Askali wa Funguka na Wauni wanasema Nabii Mwingira aliwapigia simu kwenda eneo la tukio kwa kuwa wenzao walizidiwa nay ale mapambano baada ya Jeshi la polisi kutumia medani za kujeshi kupambana nao kabla ya kuwateka askali wa Funguka!!!!.
Chanzo kutoka polisi kinasema tukio hilo liliratibiwa kijeshi kiasi cha kuwasumbua kuliko hata lile la Magomeni Mwembe Chai.


Hata hivyo baadhi ya wazee wa kanisa ambao wapo karibu na Nabii Mwingira wanasema , Umiliki wa Kiwanja chao ulifanikishwa na Waziri Fredrick Summaye ambaye baada ya ujenzi kukamilika ndiye aliyearikwa kuwa mgeni rasimi siku ya ufunguzi.
Baada ya ufunguzi huo Nabii Mwingira alimubariki Sumaye kuwa atakuwa Rais wa 2005 na alimupaka mafuta ya utawala na kulitangazia Kanisa la Efatha.
Mwaka 2005 Wakati kampeni zinafanyika Dodoma Nabii Mwingira alijaribu kusafiri kwenda Dodoma kukemea mapepo ili Sumaye apitishwe kura za Maoni lakini Polis Trafick wanasema alikwama DUMIRA na kukodi gari nyingine n kufika Dodoma akawakuta CCM wanashangiria ushindi wa kumupitisha Rais Kikwete.
Nabii Mwingira alimwita Sumaye na kumwambia hata kama Kikwete atakuwa Rais hata maliza muda wake kwani atakufa kabla ya kumaliza muda na uchaguzi utarudiwa!!
Mwingira alienda mbali na kuhubiri maneno haya kanisani kwake na kuwashangaza waumini!!
Kutokea hapo Nabii Mwingira amekuwa anaitukana serikali ya Rais Kikwete kuwa viongozi wote wa serikali yake nay eye Wanalala makaburini na hata alipoitwa na RPC Kenyera , Mwingira alitoa kebehi hiyo kanisani kwake na gazeti la Uhuru liliandika habari hiyo kwa upana .

Ni jambo la kushangaza Mwingira ambaye ndiye ameshitaki majirani zake kutafuta haki mahakamani halafu huyohuyo anageuka na kudharau mahakama na serikali.
Mimi niekwenda mbali na kubaini kuwa chanzo chake kinaweza kuwa ni matokeo ya conflict of interest ambapo yeye hakutaka Kikwete awe Rais na kwamba anasubiri afe ili sumaye achukue.
Najua Nabii Mwingira asingefanya dharau mahakama na serikali kama Sumaye angekuwa ni rais wa nchi sasa hivi!!!

Baada ya kupata undani huu ndipo nikagundua kuwa kiburi cha Mwingira kimejengwa katika mamulaka ya Fredrick Sumaye na kulindwa na Askali Waastafu wa JWTZ.

Ni jambo la kushangaza Mch David Mwakisole ambaye alishiriki kupanga njama za kubomoa kiwanda amekuwa wa kwanza kukanusha kwenye vyombo vya habari.!!!
Pia inashangaza kuwa Kiwanda cha jirani kinabomolewa halafu Nabii Mwingira kama hahusiki na tukio hilo kwa nini asikemee tukio hilo ambalo limemuhisisha?? Lakini badala yake amenyamaza kimya na kujificha Kibaha.!!!
Kitendo cha kusambaza nyaraka za umiliki kwenye vyombo vya habari kililenga kuficha uhalifu na kwamba yeye Nabii anaonekana hana imani na mahakama ambako alipeleka kesi yeye mwenyewe bali anaimani na magazeti na nguvu ya ubomoaji.
Matokeo ya ubomoaji huu yamezua upotevu wa mitambo ya Tshs 10 bils mali ya SIMON ENGENEERIN na sasa Nabii Mwingira anachnguzwa kwa upotevu huo na kanda maalumu ya DSM, hiyo ndiyo hasara ya kukosa hekima kwa jamii.


Makala yaliyopita niiliandika haya…..


Hakuna kazi ngumu kama ya kujua tabia ya mtu katika jamii inayo kuzunguka , au unayetaka kumupa kazi au madaraka au kumwamini kwa kumupa wadhifa wa kukuwakilisha
Hii ndio sababu kubwa hata Jeshi la Wananchi hufanya kazi kubwa sana kufuatilia mtu anayetaka kuajiriwa hapa kabla hata hajapata kazi hiyo.

Pia Uteuzi wa balaza la mawazili kuanzia kwa Waziri Mkuu huwa unachukua muda kwa hofu kuwa huenda wahusika wakawa na tabia mbaya.
Ugumu wa kujua tabia unatokana na mhusika kuficha tabia yake kwa hao wanao taka kumupa kazi na kujifanya malaika wa nuru na munyenyekevu. Vivyo hivyo kwenye vyama vya siasa Mtu anaweza kuanza kwa kujificha sana wakati anapo jiunga na chama Fulani lakini muda mfupi akageuka na kuwashambulia wenzake na wakati mwingine kuwapindua kabisa.!!
Tabia hii ni asilia ya wanadamu kwa mfano wa Paka kuficha makucha na kujipenyeza kwenye nyumba na wakati Fulani anaweza kulala karibu na kitanda na mtuasisituke kuliko hata Mbwa kumbe paka ni hatari zaidi.
Hivyo watu huajiriwa katika Jeshi la Polisi na kwa sababu za kujificha tabia tumeona Polisi wakikamatwa kwa makosa ya Ujambazi na wengine wamefukuzwa kazi kwa kukutwa na SMG kwenye DISCO tabia ambayo haikupaswa kuonekana kwa Watu waliopewa kazi ya kukamata Wahalifu na wavuta Bangi
Hivi karibuni RPC Wa mkoa wa Mara akitangaza kusimamishwa kazi kwa OCD kwa makosa ya kukutwa akijihusisha na wizi wa dhahabu jambo ambalo linathibitisha kuwa hata ndani vigogo polisi kuna watu wanaficha tabia ya uhalisia wao na baadaye kuanza kujionyesha kama ilivyo jitokeza kwa Nabii Mwingira!!

Mwanadamu anaweza kuficha tabia yake kwa muda Fulani lakini hawezi kuficha kwa muda wote na hata akifanya hivyo Mungu ambaye hapendi watu waangamie kwa uhalifu huweza kumufichua!!
Hivyo hata kama mtu kateuliwa katika nafasi ya kuwa Waziri mkuu na akawa na tabia ya wizi , ufisadi, rushwa , hawezi kufanya wizi kwa muda wote akafanikiwa!!
Kwa upande wa viongozi wa dini Mungu ndiye anayechunguza mioyo yetu na kutoa kazi ya kuchunga kondoo na kuwaongoza katika haki na utakatifu. Mungu ndiye anayetuteua wote kufanya kazi hata kama tunayo matatizo Roho wake anatuongoza tufikie toba na ndio maana hakuna mtu ambaye amepewa kazi na Mungu bila toba!!
Kabla ya kuanza kazi ya utumishi ,Bibilia katika kitabu cha Wibrania 12:14 inasisitiza kutafuta kwanza kuwa na amani na watu wote wanao kuzunguka kabla ya kuanza kuhubili injiri na hakika hatuwezi kuhubiri injiri katika mazingira ambayo risasi zinarindima na hivyo kukosekana kwa amani
Nimelazimika kuandika makala haya baada ya kufuatilia kwa makini tukio la moto na ubomoaji la tarehe 9 april 2012, jumatatu ya Pasaka mahira ya saa kumi na mbili asubuhi katika maeneo ya kiwanda cha Afro Plus kinacho milikiwa na Zaine Shaarifu ambao Mungu amefichua tabia na Nabii Mwingira na waumini wake Efatha Mwenge DSM na kurushwa live Katika kituo cha ITV.
Nianze kwa kumushukuru Mungu kuliweka wazi tukio hilo kwa kuwa hakuna mtu ambaye angejua kuwa pale Efatha kuna silaha ndani ya Kanisa na uhalifu unafanyika na waumini usiku kwa maelekezo ya Nabii Mwingira.
Najua polisi walipata taarifa lakini kwa upeo wangu mungu ndiye aliyefanikisha mpango mzima wa kulifichua tukio hilo siku ya pasaka ambapo wengi wasingetazamia uhalifu ufanyike kanisani kama wasiomjua Mungu wanavyofanya Uasherati siku ya Pasaka na kufanya Disco la pasaka na ulevi kama sehemu ya sherehe ya kumukumbuka Kristo.
Katika tukio hilo jeshi la polisi Kinondini liliripoti kukamatwa waumini 52 wa Kanisa la Efatha linalo ongozwa na Nabii Mwingira akiwemo Mch .David Mwakasole kwa kosa la kuwazuia polisi kufanya kazi zao na kufanya vurugu na uharibifu wa mali ikiwa ni pamoja na kuchoma kiwanda cha AFRO PLUS LTD na vitabu .
Mumiliki wa Kiwanda hicho Bw Zaine Shaarif aliwaamba waandishi wa habari kuwa vitabu vilivyochomwa moto ni pamoja na JUZU AMMA(Koran) ,vitabu vya dini ya kiislam na vya Shule. Aliongeza kuwa tukio hilo la uvamizi na uharibifu ni la tatu yakiwemo matukioa ya January 8,2012, April 6, 2012 na April 8,2012 na sasa amepata hasara zaidi ya 2.5 billions na akasikitika kuwa shauli na.156/2005 lililofunguliwa na Mwingira liko mahakama kuu kitengo cha Ardhi. N a aliongeza kwamba kwamba katika matukio yote matatu Mwingira hajafanya uahalifu mkubwa kama huu wa kuchoma vitabu vya dini ya kiislam
Taarifa zaidi za polisi zilieleza kuwa walinzi wawili wa kiwanda hicho kutoka kampuni ya KWANZA ; Salehe Lisigale na Abudul Kihenya Walitekwa na Walinzi wa Kampuni ya FUNGUKA SECURITY GUARD inayomilikiwa na Nabii Mwingira , wakawafunga kamba mikono na miguu mithili ya ng’ombe anayetaka kuchinjwa na kuwaweka chini ya ulinzi mkali baada ya kuwatesa kuwa muda mrefu.
Tukio la utekaji wa Walinzi hao lilifanikisha ubomoaji wa kiwanda,Uporaji wa mali na uchomaji wa vitabu vya dini ya kiislamu uliosababisha moshi mzito katika anga la Mwenge na kuwasitua majirani.
Taarifa za intelligensia ziliwafikia polisi KINONDONI ,ambapo walijipanga kwa kupeleka kikosi maalumu kilichoambatana na magari mawili ya zima moto na kuelekea kwenye eneo la tukio kwa lengo la kutoa msaada.
Hata hizo taarifa za polisi zinaonyesha kuwa baaada ya kufika katika eneo la tukio walikuta askari wa Mwingira wamefunga milango yote ya kuingia katika kiwanda hicho. Polisi waliomba walinzi hao kufungua milango ili wafanye kazi yao lakini walikata.

Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kinondoni Moses Fundi alijitambulisha kwa walinzi hao na kuwasihii wafungue milango kuruhusu gari za Zima moto kufanya kazi , lakini walinzi hao walikaidi amri hiyo na polisi wakaamua kukata makufuri ya milango kwa mkasi na kuingia kuokoa mali na maisha ya Walinzi waliokuwa wametekwa.

Wakati wa tukio la polisi kutumia mkasi kukata makufuri, Risasi zilifyatuliwa kutoka ndani ya Kanisa la Efatha kuwazuia polisi wasiingie ndani kufanya kazi lakini polisi waliyumia mbinu za kijeshi na kuwazidi wahalifu na kuingia ndani na kuwateka waliokuwa wanafyatua risasi kwa kuwatisha wakiongozwa na Joseph Richard(22) mkazi wa kibaha aliyekamatwa na bunduki aina ya short gun, Elikan Leornad(35) Mkazi wa Mbezi na Edson Georg(21) Mkazi wa Kibaha na wote waumini wa Mwingira.
Wakati hayo yanaendelea ,Polisi walifanikiwa kuzima moto na kuwaokoa walinzi wa kiwanda waliokuwa wametekwa na Walinzi wa Mwingira na waliwakuta wakiwa wamefungwa kamba mwilini huku wakiwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao.
Kamanda Kenyela anasema polisi walipo fika ndani ya kiwanda hicho walikuta kundi kubwa la Waumini wa Efatha waliokuwa wanabomoa na kuchoma moto vitabu wakiwa na mapanga,nondo,Mashoka,mitalimbo,sime,majambia na walipowaona askari walikimbilia ndani ya kanisa la Efatha na kuanzisha ibada ya kumushukuru mungu iliyo ongozwa kwa dharura na Mch David Mwakisoli ili kuwapoteza boya polisi huku wakiwa na silaha hizo ndani ya Kanisa.

Tukio hili la uvamizi linatuweka wazi kuwa Nabii Mwingira ni kiongozi wa namna gain kwa kuwa shughuli hiyo haiwezi kufanyika bila baraka zake na kwamba hata kama hakutoa baraka hizo basi watu anao waongoza ni wahalifu na yeye ni kiongozi wa wahalifu.
Pia tumeona matamko ya Efatha vyombo vya habari yakisisitiza umuliki wa eneo hilo na ushahidi jambo linalo onyesha wameamua kuhukumu kesi wenyewe na kubomoa kiwanda.
Nyaraka walizo sambaza katika magazeti zilipaswa kuwa vielelezo vizuri mahakamani ili kupata ushindi wa kesi na sio kupeke kwenye vyombo vya habari ili kuficha uhalifu wa kuteka walinzi na ubomoaji.
Hata kama Efatha wana haki ya Kumiliki eneo hilo ,lakini kwa sababu kuna kesi shart ni kwamba haki hiyo ingepatikana mahakamani na hakuna aliyejuu ya sheria.
Tamko la Efatha kuwa waliokamatwa walikuwa wanafanya ibada ni jambo linalotia shaka na wasiwasi hasa misingi ya uadilifu kwa ibada za Wakristo siku za pasaka ambapo ni ajabu kubwa waumini kuingia na Mapanga, Jambia , Sime na silaha zingine katika ibada na kwa tukio hili inatuonyesha kuwa umefika wakati watu wote wakiwemo viongozi wa dini na madhehebu yote kuepuka dhana kwamba wanaweza kufanya uhalifu , ujambazi, madawa ya kulevya kwa makusudi halafu wakakimbilia kwenye nyumba zao za ibada kujificha makucha yao!!
Tumeona kesi nyingi hata Rais Mstafu Mkapa alilazimika kwenda mahakamani kutoa kiapo ili haki ipakane sasa Mwingira ni nani asiyeheshimu sheria za nchi??
Zipo kesi nyingi zana za Makanisa na misikiti zote zimechuku muda mrefu sana na hakuna hata kiongozi wa dini anayethubutu kuunda jeshi la silaha na kuhamasisha uvunjishi wa sheria za nchi !!.
Aina ya Uharibifu , uhalifu na mbinu zilizotumika katika tukio la jumatatu ya pasaka zinatufundisha kuwa wapo baadhi ya watu wanaolitumia kanisa kama chaka lao la kuficha uhalifu na tabia zao za uhalifu na hapa ndipo nakubaliana na Rais Kikwete kuwa huenda wapo viongozi wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

Afande Kenyela anasema kuwa siku ya tikio tangu saa 2:00 usiku ,polisi walizuiliwa hadi saa 10:00 alfajiri walipoingia na kuwanusuru mateka na kuokoa kiwanda na hapa tunaweza kujua Mwingira ni Nabii wa namna gain na anaye ongoza waumini wenye ukatili wa kutisha tofauti na jamii ilivyotemea kwa mtu kama Kiongozi wa dini mwenye wito wa kuhamasisha amani na utulivu.
Mpaka naandika makala haya nilifanya mahojiano na Katibu Mkuu wa PCT Askofu David Mwasota kuhusu namna ya kushirikishana na kushauriana katika matatizo mbalimbali .
Askofu Mwasota kwanza alilaani vikali kitendo kitendo cha Nabii Mwingira kuhamasisha waumini na kuchoma Kiwanda wakati wa jumatatu ya pasaka ,na kuwa huo ni unyama wa kutisha ambao haupaswi kufanya na mtumishi wa Mungu hasa siku takatifu ambayo alipaswa kuwaongoza watu katika toba .
Aliongeza kuwa hata yeye ana kesi mbalimbali na zimechukua muda mrefu na anasubiri mahakama itoe hukumu.
Aliongeza kuwa yeye kama katibu wa PCT walishindwa kumusajiri Nabii Mwingira katika orodh ya Wapentecisiti hapa nchini kwa sababu ya baadhi ya mahubiri ambayo yanakwenda kinyume na maadoili ya Mungu yakiwemo yale ya kufungisha ndoa wakati bi Arusi ni mke wa mtu.
“Kwa sasa tumefanya mchakato wa kutambuana Wapentecosite ili kuboresha viwango vya maadili na mafundisho ili tuwe kielelezo kwa jamii na sio kufanya matukio ya uhalifu kama hilo na Mwingira”

“Wapo walio watumishi waliotajwa kwa biashara haramu ya dawa za kulevya na hivyo sasa tungependa kila mtu achukue tahadhari na Mungu amuongoze ili kujua mahali pa kuabudu ili aurithi ufalme wa binguni ambapo hatuwezi kufika endapo tutakuwa tunafanya unyama na Uhalifu”
Naye Mch Christopher mtikila alipotakiwa kutoa maoni alisema kwamba “Kitendo cha Mwingira kumiliki Jeshi la silaha za moto na kuwatisha polisi wakati wa ubomoaji kiwanda ni Uhaini wa kutisha ambao unatakiwa kukemea na kuchukuliwa hatua za haraka ili usijitokeze sehemu nyingine,kwani unahamasisha uasi wa sheria za nchi na dharau kwa watawala wan chi wenye dhamana ya kusimamia sheria hizo” “Haiwezekani Waumini wa Mwingira waseme kuwa wana Jeshi kubwa kuliko la Said Mwema (IGP) huo ndio uasi mkubwa na waumini hao wamejengwa kwenye kiburi Cha Mwingira kulindwa na makundi serikalini” “Mimi ni kesi zaidi ya 40 mahakamani na zimechukua zaidi ya miaka 7 , nilisha fungwa jela kwa lakini bado naheshimu mahakama na sijawahi kuhamasisha uasi kama huo”.”Kitendo cha kumwacha Mwingira anatamba na kuvunja sheria kitawafanya Waumini wote wa Mwingira waige tabia yake kwa kuwa ndiye msahuli wao na hapo mbele uasi huu utasambaa na hata katiba mpya ikiwa nzuri hakuna atakaye pata haki maana tutakuwa tunaongozwa kwa mabavu ya viongozi wa dini (Fanaticism) ‘
Baada ya kupata maoni mbali mbali kwa wadau nifike mahali nimushauri Mwingira kuwafuata mara moja Wamiliki wa Kiwnda kilicho chomwa moto na kuwaomba radhi ili kuhamasisha amani iliyopotea kwani hata kama atapata haki Mahakamani , lakini kitendo cha kuchoma Korani ambayo ni kitabu kinacho ongoza watu wengine katiaka imani yao kinaweza kisiishe haraka na hivyo kuleta chuki ya milele.Maoni ya mumiliki wa Kiwanda hicho Bw Zain Shaarif ana sema amepata hasara kubwa baada ya Koran kuchomwa moto kuliko kuungua kwa kiwanda chenyewe!!.
Ni maoni yangu kuwa Kitendo cha kurusu na kuhamasisha waamni wenye jazba kufanya uhalifu na kukimbilia kanisani ni kinyume na misingi ya dini yoyote ya kweli na yenye matashi mema kwa umma na kuelekea kuhalalisha uovu huo ni kulitukanisha na kulinajisi Kanisa la Mungu duniani na kwamba kwa tukio hilo wote tunaweza kupima ukweli juu ya nani kamupa Mwingira Unabii na Utume!!!.
Umefika wakati viongozi wa dini kutambua kwamba pamoja na kuwa na umati unaokufuata , mali nyingi hapa nchini haukufanyi kuwa juu ya sheria za nchi kwa kufanya uhalifu na kujificha katika nyumba za ibada.
Pia nawaomba viongozi wengine wa dini ya Kikristo kujitokeza hadharani kutoa msimamo juu ya tukio hilo kwani kunyamaza kimya kunaonyesha kuwa wapo nyuma ya Nabii Mwingira ama wanamuogopa: Hilo linaleta mtego mkubwa kwani endapo tukio kama hilo litafanywa na mtu wa dini Kiislamu kuchoma mali za kanisa wapo wengi ambao ni wepesi kukemea !!
Ikumbukwe kuwa hatuwezi kumutetea Mungu kwa uhalifu na kwamba uhalifu unasura ya Shetani kwa kumufanyia mtu yoyote na Mungu awabariki!!!

 
Ni sawa tu kwa sababu ni mtanzania mwenzetu au mnataka wakenya na wahindi ndio wamiliki hivyo vitu?

hatukatai yeye kumiliki, bali njia anazozitumia kumiliki hayo maeneo na na wananchi wa maeneo jirani na hayo mashamba wanavyoteseka.
Kuna wananchi katika maeneo hayo wamepoteza mashamba yao bila fidia yoyote na wengine wamekatwa hadi masikio kwa kukatisha tu katika shamba hilo lilopo huko sumbawanga mkoani Rukwa.
 
inasikitisha saana kuona watu wanashabikia vurugu kiukweli hii sio dalili nzuri kwani siku inchi hii yakitokea machafuko hakuna atakaye pona kwa wote tuliopo,naomba tuhamasishane kuwa na utulivu na kuzifanyia utatuzi wa busara tofauti zetu,vinginevyo hata pona mtu hapa!!
 
Ni sawa tu kwa sababu ni mtanzania mwenzetu au mnataka wakenya na wahindi ndio wamiliki hivyo vitu?

Rosemaria!! mashamba ya ephata yote yana migogoro ya ardhi na wanakijiji ambao hawana sehemu ya kulima! Toa constructive argument
 
SASA KWA HILI TUACHE UNAFIK, TNASUBILI TAMKO LA KADINAL AU TUTAMIN MMEPATA LA KUSEMA, AU KWA KUWA WALOCHOMA AYO MATREKTA NI WAKRISTU BASI HAMNA NOMA OW NDO INAKUA SOO, AU KUNYA LZM ANYE KUKU, AKINYA BATA KAHARISHA. ACHENI UCHOCHEZ WA DINi

Mkuu inaonekana umepewa kichwa cha kufugia nywele na sio kufikiri.
Yaani kila kitu unawaza kiudini tu.
Nani kasema waliochoma mali hizo ni makundi ya wakristo?

Kila kitu kipo wazi hao ni raia waliochochewa na mbunge wa CCM kwenda kuharibu hizo mali.
 
Back
Top Bottom