Mbunge Malocha ahutubia Wananchi dhidi ya Mwekezaji; Wateketeza Matrekta ya shamba la Kanisa Efatha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Malocha ahutubia Wananchi dhidi ya Mwekezaji; Wateketeza Matrekta ya shamba la Kanisa Efatha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KYALUMUKUNZA, Oct 18, 2012.

 1. K

  KYALUMUKUNZA Senior Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mbunge huko sumbawanga amehamasiha watu kuchoma moto KANISA,GHALA LA MAHINDI,NYUMBA NA MATREKTA chanzo ITV wenye taarifa kamili tunaomba mtujuze hapa jf.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mbuge wa CCM huyo
   
 3. D

  Dopas JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu hii ni breaking nyuzi, sasa saa tano hii wengi hawajalala kweli? Nami nasubiri habari hii
   
 4. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama huna taarifa maalum si ukae kimya?
   
 5. K

  KIBE JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa chadema ambae alishinda kesi ya uchaguzi sumbawanga....chadema kama uamsho
   
 6. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mimi hapo sitii neno.....
   
 7. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  hz habari za kweli jamani?
   
 8. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sumbawanga wana mbunge au? nafahamu hawana baada ya aliyekuwa mbunge kushindwa rufani. Weka taarifa ya kueleweka, siyo kukurupuka!
   
 9. w

  white wizard JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 2,462
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  huu,mzozo hauhusiana na haya mambo yanayoendelea sasa ya waumini wa dini ya kislamu kuchoma makanisa,huu ni mzozo wa cku nyingi kati ya wanakijiji na kanisa la efatha,la mchungaji mwingira,kuchukua eneo kubwa na kuweka uzio ambapo hata wanakijiji wanakosa mahali pa kupita!na ndio yale yale mambo ya kuchukulia mambo kidhaifu,bila kutafuta suluhisho la kudumu.
   
 10. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Lisemwalo,lipo kama halipo linakuja !;ni msemo wa kweli ?
   
 11. T

  The Worshiper JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida ni ile ile Dini inayopenda vurugu.Sijui huyo Mungu wanayemuabudu ni yupi>
   
 12. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 1,748
  Trophy Points: 280
  huooo ni uzushi hakuna kanisa lilochomwa moto sumbawanga......nimempigia anko wangu kaniambia hakuna kitu kama hichooo acheni uzushiii
   
 13. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Huyu Mbunge bila shaka ni wa serikali tawala!

  Kiongozi wa watu kweli??
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  (PICHA, HABARI NA JOSHUA MWAKABUNGU WA FULLSHANGWE SUMBAWANGA)
  ……………………………………………….
  Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.

  Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.

  Kamnda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani
  [​IMG]
  Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.

  [​IMG]
  Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.

  [​IMG]
  Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba hilo.
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ni Matunda ya FREE MARKET? Kubadilisha Siasa za NCHI bila kuwahusisha Wananchi? Wachache kuwa na MALI na Kutajirika?
   
 16. G

  GAZK New Member

  #16
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi kama kweli kanisa limechomwa, je hiyo ndio njia sahihi ya kutatua mzozo huo wa siku nyingi?
   
 17. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CCM wanaikubali falsafa ya nguvu ya umma! safi sana!
   
 18. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mtume na nabii Josephat Mwingira ana mashamba makubwa rukwa,Bagamoyo ana Ephata bank! Kibwetere type!
   
 19. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Ni sawa tu kwa sababu ni mtanzania mwenzetu au mnataka wakenya na wahindi ndio wamiliki hivyo vitu?
   
 20. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  SASA KWA HILI TUACHE UNAFIK, TNASUBILI TAMKO LA KADINAL AU TUTAMIN MMEPATA LA KUSEMA, AU KWA KUWA WALOCHOMA AYO MATREKTA NI WAKRISTU BASI HAMNA NOMA OW NDO INAKUA SOO, AU KUNYA LZM ANYE KUKU, AKINYA BATA KAHARISHA. ACHENI UCHOCHEZ WA DINi
   
Loading...