Kwa wapenda haki kuachiwa mbunge Lijuakali na jaji Munisi kwa msingi eti hati ya mashitaka ilikosewa kujazwa ni kutoitendea fani ya sheria haki. Lijuakali alikutwa na makosa (was found guilty) kwa makosa aliyoshitakiwa nayo kwa hivyo mahakama ya juu kumuachia kwa kasoro ya kujazwa fomu ya mashitaka inaonesha uzembe au kukosa uwajibikaji kwa jaji.
Ingekuwa sahihi jaji kuelekeza mashtaka yafunguliwe upya kuliko kumuachia mhalifu. wapo wanasheria kama Lissu ni hodari wa kuwatoa wahalifu lupango kwa makosa ya kiufundi.
Ukichukulia wanasheria wengi kuwa na kawaida ya kuuza haki idadi ya wahalifu kuachiwa kwa sababu za kiufundi huku tayari wakiwa wameonekana na makosa yaweza kuongeza huko tunakoelekea.
Kwa wapenda haki mbunge Lijuakali bado ni muhalifu kwa sababu rufani yaka haikumuona hana kosa aliloshitakiwa nalo.