Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

Jionee huruma mwenyewe. uploadfromtaptalk1367032998226.jpg
namuonea huruma Lema!
 
Maofisa wa Jeshi la Polisi, waliokuwa na mbwa, mabomu ya machozi na silaha nyingine za moto, usiku wa kuamkia jana waliruka ukuta na kuingia katika eneo la makazi ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambako walizingira nyumba yake kwa zaidi ya saa nne.


Operesheni ya kutiwa mbaroni Lema iliogozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD), Gillel Muroto ambaye alifuatana na askari zaidi ya 25 waliokuwa na silaha hizo.


Walifika nyumbani kwa Lema saa 5:00 usiku lakini walilazimika kusubiri hadi saa 9:10 walipomkamata Mbunge huyo baada ya yeye mwenyewe kujisalimisha. Habari zinasema Lema aliyekuwa akihojiwa na polisi hadi jana jioni, alinyimwa dhamana kwa maelezo kwamba “anaweza kuhatarisha amani”.


Mashuhuda waliokuwa karibu na anakoishi Lema, eneo la Njiro Mwisho wa Lami, walisema polisi hao walifika wakiwa kwenye magari manne na kwamba ili kuchunguza ndani ya uzio wa nyumba yake, walipanda juu ya mabega ya wenzao huku wakielekeza mitutu ya bunduki tayari kukabiliana na lolote ambalo lingejitokeza.

Baada ya kuchungulia baadhi yao walitumbukia ndani ya uzio na kwenda kusimama mbele ya milango na madirisha ya nyumba ya Lema na huku nyuma wengine walipanda tena kwenye mabega ya wenzao kuendelea kuweka ulinzi kwa walioingia ndani.


Askari hao wanadaiwa kwamba waliwataka walinzi wa nyumba hiyo iliyopo karibu na Chuo cha Ufundi Veta, kuwafungulia mlango, lakini walinzi hao walikataa hivyo kuzua mabishano makali.

Kutokana na mabishano hayo, Lema aliyekuwa ndani amelala alishtuka na kuanza kufuatilia na kubaini kuwapo kwa polisi nje ya nyumba yake hiyo. Mke wa Lema, Neema alimpigia simu Katibu wa Wilaya wa Chadema, Aman Golugwa kumwarifu kuhusu uwepo wa watu walioruka ukuta.


Golugwa jana alithibitisha kupokea simu ya mke wa Lema na kwamba alipopata taarifa hizo alimwarifu Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) wa Mkoa wa Arusha, Camillius Wambura ambaye baadaye alimuahidi kwamba angefuatilia suala hilo.


“Baadaye alithibitisha kuwapo kwa polisi waliotumwa kwa ajili ya kumkamata Lema lakini akasema amewapa maelekezo ya kufuata taratibu za kawaida,”alisema Golugwa na kuongeza:“Baada ya hapo, wale askari waliokuwa wameruka ukuta walitoka nje ya uzio”.


Habari zinasema wakati baadhi ya askari wanaruka ukuta, wengine walibaki nje wakizingira uzio wa nyumba ya Lema huku wakiwazuia viongozi wa Chadema waliokuwa eneo hilo kusogea.

Kukamatwa kwa Lema katika mtindo wa aina yake kumefanywa saa chache tangu alipotoa kauli ya kukataa kujisalimisha polisi, kutokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo. Mulongo aliagiza Lema akamatwe kwa tuhuma kwamba alichochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).


Katika vurugu hizo, wanafunzi hao walimzomea Mulongo na kurushia mawe msafara wake wakati alipokwenda kusikiliza malalamiko yao yaliyotokana na kuuawa kwa mwanafunzi mwenzao, Henry Kago (22) ambaye alichomwa kisu na watu wasiofahamika wakati anatoka kujisomea saa 4:00 usiku.

source: Gazeti la mwananchi
 
Aisee kama Osama alivyokamatwa na wamarekani hebu toeni documentary tuone wakuu..
 
Nchi hii ina vioja kweli wanaong'oa kucha na meno bila ganzi wapo wanakula maisha na kulindwa juu, wakina kamihanda wapo wanatoa kauli za kijeuri bila kuogopa hao walioua wala hawashugulikiwi ila anayeuliza kwanini hayo yatokee anatafutwa kuliko waliolipua kule boston marekani.

Kweli tutaona na kusikia mengi.
 
Power in hands of a foolish person is very dangerous. Poleni wana arusha kuwa na mkuu wa aina hii.
 
jeshi letu limejaa vimeo wanaofanya kazi kwa kuburuzwa na wanasiasa uchwara,inakuwaje wasiwakamate wang'oa kucha? haki ya mungu aka ka nchi ka ajabu kweli.
 
Hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho.huu unyanyasaji kuna siku utafika mwisho tu.
 
mtu mmoja anapelekewa magari 4 na zaidi ya askari 24 kweli askari wetu ni vimeo tosha hata OCD anatia aibu kuongoza na kikundi kikubwa kiasi kama hicho
 
wamewekeza nguvu kubwa katika kumwinda, kumvamia na kumkamata Mheshimiwa Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema) kuliko hata nguvu watumiayo kumsaka muuaji wa marehemu mwanachuo wa chuo cha uhasibu Arusha. Daaaah...
 
Huo ugaidi wa wazi, cna imani km tanzania itaendelea kwa mabavu haya.
 
heh Tanzania zaid ya uijuavo, mambo gani sasa haya...... hadi OCD.....
 
Back
Top Bottom