Mbunge Kainja ajikita kuwainua Wanawake kiuchumi mkoa wa Tabora

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE KAINJA ATOA MILIONI 81 KWA WANAWAKE (UWT) KUWAWEZESHA KIUCHUMI KATIKA MKOA WA TABORA

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Tabora Mhe. Jacqueline Kainja Andrew ametoa fedha kiasi cha Shilingi Millioni 81 kwa Kata 206 za Mkoa wa Tabora yenye lengo la kuwawezesha wanawake wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kiuchumi.

Katika hafla ya Uzinduzi wa Utoaji fedha za Miardi kwa Wanawake, Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Katibu Tawala Mkoa wa Tabora (RAS), Mhe. John Roghat Mboya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batlida Burian.

Akizungumza katika halfla ya uzinduzi wa utoaji fedha za miradi kwa Wanawake wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Kainja amesema kuwa "Hii ni kiu yangu kuinua wanawake kiuchumi, juzi tulikuwa na kipindi cha Redio Uhai na niliwaambia kuna vitu vingi nimefanya"

"Nimegusa vikundi mbalimbali lakini nimeona nitoe kwa wanajumuiya wa UWT ili kuweza kuinuana kiuchumi. Nategemea watafanya mazuri na watakaofanya vizuri wataongezewa zaidi na nitapita kwenye hiyo miradi kuona imefika wapi" - Mhe. Jacqueline Kainja Andrew

Aidha, Mbunge Mhe. Kainja alipata nafasi ya kuwasilisha na kuwasomea akina Mama wa Mkoa wa Tabora kitabu cha Utekelezaji wake wa Ilani ya CCM kwa majukumu yake kama Mbunge kwa kipindi cha Miaka mitatu ya utendaji wake.

Kwa upande wao Wanawake wa UWT Mkoa wa Tabora wamempongeza Mbunge Kainja kwa Upendo wake na kuona haja ya kuwainua wanawake kiuchumi kuwa ni kipaumbele cha muhimu kwake, hivyo wamemshukuru sana!

Wanawake wa UWT Mkoa wa Tabora wamempatia zawadi mbalimbali Mbunge Kainja kama ishara ya kuonyesha upendo wao kwake na kuahidi kuendeleza ushirikiano wao wa kutosha kwa Mbunge huyo.


WhatsApp Image 2023-07-07 at 18.26.00.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 18.26.00(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 18.26.00(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 18.26.53.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 18.26.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 19.01.13(6).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 19.01.13(4).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 19.01.13(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-07 at 19.01.13(1).jpeg
 
Back
Top Bottom