Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

Mbunge Jeremiah Sumari afariki dunia

marejesho

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
6,634
Reaction score
3,660
Kuna habari zimenifikia sasa havi kwamba Mbunge huyu amefariki!.

Mbunge huyu alikuwa mgonjwa na hakuapishwa 2010.

Alipelekwa India na iliandikwa hapa jukwaani, hali ilikuwa mbaya sana!

Baada ya kupata matibabu ya uvimbe kwenye ubongo, alirudishwa kimyakimya na sasa nimesikia amefariki.

UPDATE:

Naibu Spika kathibitisha habari hizi na marehemu alifariki saa 8 usiku wa kuamkia leo akiwa hospitali ya taifa - Muhimbili
 
Habari nilizozipata ni kuwa aliyewahi kuwa naibu waziri wa fedha na mbunge wa Arumeru mashariki bwana Sumari ameaga dunia.

Poleni wafiwa.

Source: MOI
 
Habari nilizozipata ni kuwa aliyewahi kuwa naibu waziri wa fedha na mbunge wa Arumeru mashariki bwana Sumari ameaga dunia.

Poleni wafiwa.

Source: MOI
Asante kwa taarifa mkuu,amefia India?
 
Je, mpaka anafariki alikuwa mbunge? Poleni sana wafiwa.
 
duh may he RIP.nilisikia habari za kuugua kwake hapa jf.
 
Nilisikia muda mrefu kuwa yu mgonjwa lakini sikusikia kama aliwahi kupelekwa India kwa matibabu kama wenzie................. Hivi kumbe kupelekwa India kwa matibabu inategemea na nafasi uliyo nayo serikalini!
Mungu amlaze mahali pema peponi...............Amina
RIP Bwana Sumari
 
Alipelekwa India kwa matibabu na taarifa hizo ziliwekwa hapa jukwaani
RIP (Mbunge mteule)
 
Duh hivi vifo? Jana tu tumezika mbunge kabla hatujaanua matanga msiba mwingine! Poleni wafiwa na mwenyezi mungu amlaze mahala pema marehemu.
 
Poleni wote mlioguswa na msiba huo. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina
 
Hakuna wa kudumu -dunia mapito. Ngoja wanaoutamani ubunge wajipange kwa kuanzia kwa kalimanzira. Ole wao. Tupokezane vijiti hivyo
 
Alipelekwa India kwa matibabu na taarifa hizo ziliwekwa hapa jukwaani
RIP (Mbunge mteule)
Haya mambo yanapotokea ndio tunajifunza pia hivi unaweza kukaa muda gani bila kuapa kama Mbunge mteule kwa wabunge waliochaguliwa na wananchi? Sheria zetu hazitoi muda kutengua Mbunge Mteule na kuitisha uchaguzi kama Mteule akishindwa kuapa kwa sababu yeyote? Watu wa Arumeru hawakuwa na Mbunge kipindi chote hiki na pengine ingekuwa zaidi ya hapa kama angeendelea kuumwa kwa miaka mingine? Napenda kujifunza kupitia tukio hili wakuu.
 
Back
Top Bottom