Aliyesaidiwa Ada na Jakaya Kikwete mwaka 2003, Leo Hii ni Mbunge wa Jimbo la Rorya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE JAFARI CHEGE - KIJANA ULIYEMSAIDIA ADA MIAKA 10 ILIYOPITA LEO HII NI MBUNGE WA JIMBO LA RORYA

"Miaka 10 iliyopita, mwaka 2003 nikiwa kidato cha Tatu wakati nikiwa nahangaika kutafuta Ada kwaajili ya kunifanya niendelee na masomo yangu. Wakati ule Mhe. Jakaya Kikwete ulikuwa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, nilikutana na wewe Chang'ombe" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Ndugu yangu mmoja anaitwa Julius amehudumu kama msaidizi wako Mhe. Jakaya Kikwete baada ya kusikiliza ukasema huyu kijana anasoma wapi, shida ni nini kwamba huyu bwana mdogo anahitaji Ada ya Shilingi 321,000 ili aweze kumaliza masomo yake na amebakiza siku tatu afanye mtihani wake. Nakumbuka ulitoa Shilingi 400,000 ukampatia Julius ukamuambia mpe huyu kijana aende kusoma na ukanipa usia" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Binafsi imebaki kwenye nafsi yangu, lakini nikushukuru na kukuambia kuwa Kijana uliyemsaidia zaidi ya miaka 10 iliyopita bila kujua ndoto na dhamira yake ya mbele ndiye aliyesimama hapa mbele na ni Mbunge wa Jimbo la Rorya" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Mungu aendelee kukuongezea, Akupe maisha Marefu na sisi kama Viongozi wabunge vijana tunayo ndoto ambayo tunakuiga kwa namna ulivyokuwa unaongoza nchi hii. Umekuwa mstaarabu, Mvumilivu hata pale unapopigwa mishale" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Ndugu zangu wa Rorya, nimeshiriki nanyi tangu ujenzi wa Kanisa, harambee ya kwanza ya vifaa vya Kanisa, ikaja Harambee ya pili kwaajili ya ujenzi wa Kanisa, kwa mara nyingine ya tatu nitachangia Shilingi Milioni Moja (1,000,000) - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

View attachment 2724248
Safi sana kumbuka safari yako daima
 
Kwa hiyo unajifunza wizi na ufisadi wake?
Ndio maana bunge limekuwa la kifedhuli namna hiyo!
Ndiyo maana bunge linapitisha mikataba ya ovyo namna hiyo?

Na hili ndio litakuwa bunge la ubunge wako wa mwisho ndugu Jaffary Chege Wambura!

Mtupishe tuweke watu wenye kujitambua huko bungeni.
Salamu zikufikie popote ulipo iwe Rorya au Dodoma.
Anzeni kufungasha maana 2025 mtakiona kivumbi.
 
Siasa ni uwanja mzuri wa kukuza jambo kwa kweli
Amin 400k kwa Pesa alizonazo Uyo mzee ni sawa na mimi tu navowabless madogo Jero jero za Pipi sioni haja ya kusifiwa na kutangazwa kama hivi.
Aache Kukuza Kambo ndugu Wambura asitwambie hajawah saidiwa na watu wengine pesa zaidi ya hiyo.
 
Ukute anamshukuru JK kwa hiyo laki 4,anaacha kumshukuru mjomba wake au shangazi yake,ambaye labda alijinyinyima,akatoa 5000/= na yawezekana ndiyo alikua kabaki nayo ndani.Huyo mbunge anajua mtu kujisacrifice....?
Asome biblia asome kile kisa cha yule mama aliyetoa sadaka ya kweli.Kikwete hiyo laki nne ni ndogo sana kwake, yawezekana huyo chawa wake aitwae Julius,alimwambia JK nimempa milioni mbili,yeye Wambura anajua ilitoka laki 4.
 
Back
Top Bottom