Mbunge Ighondo: Mikopo ya Elimu itolewe na kwenye Vyuo vya Ufundi kwa sababu hawa wanafanya kazi moja kwa moja bila kusubiri ajira

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,638
2,000
Mbunge Jimbo la Singida Kaskazini, Ighondo Ramadhan Abeid, ameiomba Serikali kupanua wigo wa kutoa Mikopo ili kuwafikia walioko kwenye Vyuo vya Ufundi ikiwemo VETA.

Amesema, sio kila Mwanafunzi anaweza kwenda Vyuo Vikuu hivyo wale wanaokwenda Vyuo vya Ufundi wawezeshwe kwani uzuri wao wanafundishwa na wanakwenda kufanya kazi moja kwa moja na kuweza kurudisha Mkopo.

Ameongeza kuwa, 'Graduates' wameshakuwa wengi na Serikali inashindwa kuwaajiri wote wamejaa tu mtaani.
 

ZNM

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
1,159
2,000
Kwani huko katika vyuo vya ufundi wao wanasemaje?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,813
2,000
Vyuo vya VETA vya serikali hata sidhani kama wanahitaji mkopo ada ni ndogo mno serikali sehemu kubwa ina subsidize

Mikopo itolewe kwenye fani zenye ajira ndani na kimataifa. Rwanda mfano ingharimia sana bure wanafunzi wake kusoma masomo magumu ndani na nje yenye masoko makubwa ya ajira nje lengo wakitaka Rwanda iwe knowldge hub ya kupata best skills in Africa

Rwanda wanataka kila mtu mwenye fani yake awe na international certification awe engineeer, awe, aktari etc Sisi hapa mikopo inatolewa hovyo haiko strategic. Unakopesha mtu eti kisa tu kasoma shule ya kata toka msingi hadi kidato cha sita!!! Akimaliza anaenda kusoma degree ya historia na unajua kabisa ajira haipo kwenye hiyo fani lakini unamwaga pesa. Akimaliza kazi hana na mkopo haulipiki

Mikopo nadhani mwanzoni kulikuwa na vigezo nchi ilikuwa inatoa mikopo eneo ambalo inaona ina uhitaji mkubwa mfano madaktari, mainjinia, wataalamu wa kilimo na mifugo nk ambao walau waweza nusa kuwa pale paweza kuwa na kaajira au akajiajiri lakini baadaye naona bodi ya mikopo limekuwa shamba la bibi inatolewa kwenye eneo unaona wazi kabisa pale huu mkopo hautalipika

Serikali itoe kipaumbele kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa sana mfano sasa hivi tunataka viwanda ina maana tutahitaji kuzalicha wataalamu wengi wa eneo hilo wa viwanda tofauti tofauti nk kama food processing, chemical engineering, pharmacy, mechanical and electrical engineering, nk ilI WAWEKEZAJI WAKIJA TU watu hawa hapa.
 

3 Angels message

JF-Expert Member
Aug 3, 2017
3,396
2,000
Nilichomkubali ni alipomponda Spika kuhusu kuwakumbatia watu wa drs la 6 na kuwapuuza wasomi nilimuona ana uthubutu maana alisema bila kupepesa macho kuwa siyo sawa vile kiti cha Spika kinavyofanya.
 

78Kuku

Senior Member
Mar 31, 2021
188
250
Vyuo vya VETA vya serikali hata sidhani kama wanahitaji mkopo ada ni ndogo mno serikali sehemu kubwa ina subsidize

Mikopo itolewe kwenye fani zenye ajira ndani na kimataifa.Rwanda mfano ingharimia sana bure wanafunzi wake kusoma masomo magumu ndani na nje yenye masoko makubwa ya ajira nje lengo wakitaka Rwanda iwe knowldge hub ya kupata best skills in Africa

Rwanda wanataka kila mtu mwenye fani yake awe na international certification awe engineeer ,awe,daktari etc Sisi hapa mikopo inatolewa hovyo haiko strategic.Unakopesha mtu eti kisa tu kasoma shule ya kata toka msingi hadi kidato cha sita!!! Akimaliza anaenda kusoma degree ya historia!! na unajua kabisa ajira haipo kwenye hiyo fani lakini unamwaga pesa.Akimaliza kazi hana na mkopo haulipiki

Mikopo nadhani mwanzoni kulikuwa na vigezo nchi ilikuwa inatoa mikopo eneo ambalo inaona ina uhitaji mkubwa mfano madaktari,mainjinia ,wataalamu wa kilimo na mifugo nk ambao walau waweza nusa kuwa pale paweza kuwa na kaajira au akajiajiri lakini baadaye naona bodi ya mikopo limekuwa shamba la bibi inatolewa kwenye eneo unaona wazi kabisa pale huu mkopo hautalipika

Serikali itoe kipaumbele kwenye maeneo yenye uhitaji mkubwa sana mfano sasa hivi tunataka viwanda ina maana tutahitaji kuzalicha wataalamu wengi wa eneo hilo wa viwanda tofauti tofauti nk kama food processing,chemical engineering,pharmacy ,mechanical and electrical engineering ,nk ilI WAWEKEZAJI WAKIJA TU watu hawa hapa
Hivi huwezi kutoa hoja pila kupondea upande flani? Unalalamika kwamba mikopo inatolewa kwa fani ambazo hazina ajira je hizo fani unazosema zina ajira ie. Engineering., MD na kilimo mbona graduates wengi wa hizo fan wamejazana mtaani wakiwa ma jobless.
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,212
2,000
Kuna kitu nimekiona kwenye hii habari nimesisimka sana. Muda unakwenda mbio sana.
RamdhaniIghondu.jpg
 

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,301
2,000
Shida sio mikopo. Shida ni mfumo wa elimu wa nchi yetu ni mbovu.

Kila msomi nchi hii anataka aajiriwe. Ajira hakuna sasa inakua ni kero bin mateso.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Mbunge Jimbo la Singida Kaskazini, Ighondo Ramadhan Abeid, ameiomba Serikali kupanua wigo wa kutoa Mikopo ili kuwafikia walioko kwenye Vyuo vya Ufundi ikiwemo VETA

Amesema, sio kila Mwanafunzi anaweza kwenda Vyuo Vikuu hivyo wale wanaokwenda Vyuo vya Ufundi wawezeshwe kwani uzuri wao wanafundishwa na wanakwenda kufanya kazi moja kwa moja na kuweza kurudisha Mkopo

Ameongeza kuwa, 'Graduates' wameshakuwa wengi na Serikali inashindwa kuwaajiri wote wamejaa tu mtaani.
Pointless kabisa, vyuo vikuu vyenyewe mikopo haitoshi sembuse vyuo vya kati?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom