Serikali ya Rais Samia inajenga vyuo 89 vya VETA nchi nzima. Haya ni mapinduzi kwenye sekta ya elimu ya ufundi

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,380
8,435
Habari zenu wadau.

Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dr.Samia Suluhu Hassani inajenga jumla ya VETA 89 Nchi nzima.

Kati ya hizo Veta 4 Ni za Mikoa na Veta 85 ni za Wilaya.

Mwaka 2021/2022 ilianza kujenga Veta 25 kwenye Wilaya na mwaka huu 2022/2023 inajenga Veta 60..

Ikumbukwe kwamba Lengo la Serikali Ni Kuhakikisha kila Wilaya ya Tanzania na Mkoa inakuwa na Chuo Cha Veta ili.kuleta mapinduzi ya Elimu ya ujuzi kwenye fani mbalimba zitakazowawezesha maelfu ya Vijana kujiajiri na kuajiriwa..

Ni elimu ya Ufundi pekee ndio itakayoleta mapinduzi ya kiuchumi na ajira za uhakika kwa vijana..

Imagine just within less than 2 years toka awe Rais Mambo haya makubwa yanafanyika yet kuna watu Wana kejeli na Kutaka asisifiwe wakati tumekuwa na Marais hapo kabla Hakuna kitu kikubwa walifanya.

Hii Ni sekta Moja tu ya Elimu ya Ufundi lakini Moto huu uko kwenye sekta zote za Uchumi.

Pamoja na pongezi hizi tunaiomba Serikali ifikirie kununua vifaa vya kutosha vya kujifunzia kwenye vyuo hivyo kwa wakati na pia waweke utaratibu wa kutoa tenda kwa vijana watakaohitimu kwenye vyuo hivyo kwa mahitaji mbalimba ya kiserikali badala ya kila kitu kuagiza China.

Pia vijana wabunifu wapewe motisha na mitaji watakapohitimu.

Kama huoni kwa macho utaoneshwa tuu,video.👇

Attachments

  • Screenshot_20221130-072108.png
    Screenshot_20221130-072108.png
    173 KB · Views: 11
  • Screenshot_20221130-071743.png
    Screenshot_20221130-071743.png
    179.6 KB · Views: 9
  • wizara_elimutanzania_1669788796576298.jpg
    wizara_elimutanzania_1669788796576298.jpg
    123.7 KB · Views: 10
Hii Ni kazi nzuri iliyotukuka na inayostahili kupongezwa na wapenda Maendeleo wote 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20221130-091433.png
    Screenshot_20221130-091433.png
    189.1 KB · Views: 12
  • Screenshot_20221130-091535.png
    Screenshot_20221130-091535.png
    68.4 KB · Views: 10
Hizo pesa za ujenzi zinatoka wapi? Ni kodi na tozo za wananchi, au ni pesa za mikopo au misaada au ni pesa zake mwenyewe??

Kama ni makusanyo ya kodi na tozo kuna haja gani ya yeye kusifiwa??

Kama ni mikopo au misaada kuna haja gani ya kumsifu??

Mtu anapotimiza majukumu yake anahitaji kusifiwa kweli??? Lakini, ikiwa hizo pesa zinatoka mfukoni mwake basi ana haki ya kusifiwa.
 
Na Mimi ndio nashangaa kwamba mtu akitimiza wajibu wake inakuaje dhambi kusifiwa au kupongezwa?

Kwamba wewe hujawahi pongezwa kwa kutimiza wajibu wako?
 
Na Mimi ndio nashangaa kwamba mtu akitimiza wajibu wake inakuaje dhambi kusifiwa au kupongezwa?

Kwamba wewe hujawahi pongezwa kwa kutimiza wajibu wako?
That is preposterous! Unapongezwa kwa kutimiza wajibu wako wakati unalipwa mshahara na marupurupu kwa kazi uliyopewa??
 
VETA , washirikiane na Sido na sido iwe inapeleka watu wao VETA ili kufundisha watu wapate ujuzi wa kutengeneza vitu mbalimbali, kama sabuni , na baadhi ya mashine za kuchakata bidhaa, watu wajifunze kufanya packaging vizuri, ili tuanzie hapo kuelekea viwanda vidogo vidogo baadae viwanda vya kati na baadae viwanda vikubwa, hayo yanawezekana kabisa.
 
That is preposterous! Unapongezwa kwa kutimiza wajibu wako wakati unalipwa mshahara na marupurupu kwa kazi uliyopewa??
Hujanijibu swali langu hapo juu,wewe hujawahi pongezwa kwa kutimiza wajibu wako?

Kama Ni salary wengi tuu hulipwa Ila hawatimizi inavyotakikana na Kama Ni Urais walishapita wengi tuu na hawakufanya yanayofanywa Sasa.
 
That is preposterous! Unapongezwa kwa kutimiza wajibu wako wakati unalipwa mshahara na marupurupu kwa kazi uliyopewa??
magufuli aliyeimbwa na kila mtu alikuwa anatoa pesa zake mfukoni?.hii nchi inashida sana.yaani hujui umuhimu wa motisha mtu anapotimiza majukumu yake?.sifa ni motisha sio malipo ya kazi
 
Back
Top Bottom