Mbunge Fyandomo ashtukia upigaji ujenzi wa stendi Tukuyu. Hizi sio paving ni mchanga na wahandisi wapo

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mbunge wa vitu maalum Mkoa wa Mbeya Mhe. Suma Ikenda Fyandomo, ameshtukia mchezo unaofanywa na wataalamu katika ujenzi wa stendi ya mabasi katika Mamlaka ya mji mdogo wa Tukuyu Mkoani Mbeya, kwa kupanga tofali ndogo za nzege (PAVING BLOCK) zilizo chini ya kiwango hali inayo hatarisha ubora wa stendi hiyo.

Akizungumza mbele ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Fyandomo amesema aina ya tofali ndogo zinazo pangwa katika stendi hiyo hazina tofauti na zile zilizo pangwa katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya hiyo, ambazo zimeharibika katika kipindi Cha muda mfupi kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango hivyo hupukutika na kubaki mchanga pekee.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Juma Homera ametoa masaa 24 kwa Mhandisi wa Halmashauri hiyo kutoa tofali hizo zote zilizo chini ya kiwango na kuzuia malipo yote ya mzabuni aliye uza utofali hizo.

20231118_073848.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom