Mbunge Ester Midimu Asimikwa Ungole, Aitwa Ngole Sane

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Baraza la Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Simiyu jana (Januari 14, 2024), limemsimika Ungole Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo, Ester Midimu na kumpatia jina la Sane kutokana na kuwatumikia Wanawake kwa muda mrefu.​

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Simiyu Mariam Manyangu amesema wamemsimika Mbunge huyo wa Viti Maalumu kutokana na juhudi zake anazozifanya ikiwemo kuwatetea wanawake katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma za Maji, Afya na Elimu.

Akitoa shukrani baada ya tukio hilo, Mbunge Ester amewapongeza wanawake hao kwa kuendelea kushirikiana nae huku akiahidi kuendelea kuwatumikia katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kuwasilisha kero zao kwa Dk. Samia Suluhu Hassan.

‘’Nitaendelea kuwatetea wanawake wa Mkoa wa Simiyu na maeneo mengine ili mpate mahitaji msingi ya kibinadamu, nitahakikisha mnapata haki sawa za kielimu, afya na huduma za maji’’ amesema Mbunge Ester.

WhatsApp Image 2024-01-17 at 23.06.02.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-17 at 23.06.03.jpeg
WhatsApp Image 2024-01-17 at 23.06.03(1).jpeg
 
Back
Top Bottom