Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
SIMIYU: Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko apata ajali mbaya usiku wa kuamkia leo wakati akitoka Kumjulia hali Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Geita, Kamanda Mhere Mwita. Katika ajali hiyo mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha.
=======
Napenda kuwashukuru kwa kuniombea kutokana na ajali mbaya niliyoipata leo katika eneo la kitambaa kilometa chache tu toka mto Simiyu. Namshukuru sana Mungu kwa upendeleo wa pekee wa kuniokoa katika ajali hii mbaya.
Nawashukuru watanzania wote bila kujali itikadi walivyo jitahidi kutoa misaada mbali mbali mara tu baada ya ajali kutokea. Wananchi wa eneo husika, wasafiri watumiao ile barabara, Jeshi la Polisi, Wabunge, Viongozi wa wangu wa chama wa Taifa, Mkoa wa Simiyu na Mwanza, marafiki , kipekee kabisa kaka yangu mbunge wa Magu amejitolea sana kuhakikisha tunapata huduma za dharula hadi usiku wa manane. Mungu akubariki sana na akurudishie ulipojitoa.
Nimeletwa Mwanza nina maumivu makali kwenye mgongo, kiuno na mbavu ila najua Mwenyezi Mungu atatenda miujiza. Niwafariji wafiwa wa ndg yetu alipoteza maisha katika tukio hili.
Marehemu alikuwa akitokea Busega ila akawa anatembea upande wa gari za kutoka Magu. Na ndio chanzo cha ajali hawa madereva wa pikipiki tuwaombee kwa Mungu.
Ahsanteni sana Ndg zangu.