Mbunge Ester Matiko apata ajali mbaya akitoka kumjulia hali Mhere Mwita, mmoja afariki

Pole sana Mh Ester Matiko kwa ajali mbaya sana.na R.I.P marehemu
 
Stephen Wasira Bado lile jimbo analingangania bado
Kakwambia? Mzee katulia kabisa, wapiga kula wa Bunda ndio wanalihangaikia hilo jimbo.

Lakini, mind you huyu Ester aliyepata ajali sio Ester wa Bunda huyu ni Ester wa Tarime mjini.
 
Stephen Wasira Bado lile jimbo analingangania bado


Hao ndio vijana wetu. Hawaelewi mambo, hawawezi kudadavua, hawawezi tofautisha Bunda na Tarime ama Bulaya na Matiko. Matokeo ya GPA system
Halafu ni wabishi kweli kweli, wanajifanya wanajua kila kitu, walipoambiwa na Mkapa kuwa CCM ni chama cha ukombozi walibisha na wanabisha hadi sasa.
 
Kuna madaktar wanatumia pikipiki za serikali kwa ajili ya kuwahi kutoa huduma za dharura anapopigiwa simu kuna dharura anaona ili awahi ni bora aende na pikipiki kuliko kusubiri gari itoke ilipo kumfuata, na hosp nyingi zina pikipiki
 
Polis kumsaidia mbunge haimaanishi kuwa polis wote ni wema na pia si kweli kwamba polisi wote ni polisisiem mbona mi nimewakatia kadi wengi tu ila kuna wale ambao mi nawaita hawajui walitendalo wakitumwa na miguu chemba hawanaga mental digestion
 
SIMIYU: Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko apata ajali mbaya usiku wa kuamkia leo wakati akitoka Kumjulia hali Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Geita, Kamanda Mhere Mwita. Katika ajali hiyo mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha.

=======
Napenda kuwashukuru kwa kuniombea kutokana na ajali mbaya niliyoipata leo katika eneo la kitambaa kilometa chache tu toka mto Simiyu. Namshukuru sana Mungu kwa upendeleo wa pekee wa kuniokoa katika ajali hii mbaya.

Nawashukuru watanzania wote bila kujali itikadi walivyo jitahidi kutoa misaada mbali mbali mara tu baada ya ajali kutokea. Wananchi wa eneo husika, wasafiri watumiao ile barabara, Jeshi la Polisi, Wabunge, Viongozi wa wangu wa chama wa Taifa, Mkoa wa Simiyu na Mwanza, marafiki , kipekee kabisa kaka yangu mbunge wa Magu amejitolea sana kuhakikisha tunapata huduma za dharula hadi usiku wa manane. Mungu akubariki sana na akurudishie ulipojitoa.

Nimeletwa Mwanza nina maumivu makali kwenye mgongo, kiuno na mbavu ila najua Mwenyezi Mungu atatenda miujiza. Niwafariji wafiwa wa ndg yetu alipoteza maisha katika tukio hili.

Marehemu alikuwa akitokea Busega ila akawa anatembea upande wa gari za kutoka Magu. Na ndio chanzo cha ajali hawa madereva wa pikipiki tuwaombee kwa Mungu.

Ahsanteni sana Ndg zangu.

View attachment 474313

View attachment 474314 View attachment 474314
POLE SANA MAMA YETU, MUNGU NI MWEMA NA NI WA WOTE. ATAKUPONYA MAPEMA!
 
Back
Top Bottom