Manyara: Msafara wa Waziri Kigwangalla wapata ajali. Waziri ajeruhiwa na Mmoja afariki dunia

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,450
12,317
Mtu mmoja amefariki dunia kwenye msafara wa Waziri wa Utalii Hamisi Kigwangalla, aka HKigwangalla huku mheshimiwa waziri mwenyewe akiwa amejeruhiwa....

Aliyefariki ni mwana JamiiForums mwenzetu Ndg. Hamza Temba, ambaye alikuwa Afisa Habari wa Wizara anayeambatana na Waziri.



IMG-20180804-WA0001.jpg
IMG-20180804-WA0006.jpg


======

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla amepata ajali akitokea Arusha hali yake ni mbaya na wanasubiri Helicopter ili wamhamishe Hospitali na Mtu mmoja Mwandishi wa habari amefariki" amesema Mbunge wa Mbulu Vijijini Flaitey Masai.

IMG-20180804-WA0002.jpg

IMG_20180804_111505.png

TANAPA wameweza kumsafirisha kwa Helkopta kutoka kituo cha afya cha Magugu hadi Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro, sasa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla anaendelea vizuri na matibabu katika Hospitali ya KCMC

Taratibu za kidharura zinafanyika nje ya Hoteli ya Kitalii ya Mount Meru ili kumsafirisha Waziri Kigwangwala pamoja na majeruhi wengine katika Hospitali ya Mount Meru kwa matibabu zaidi.


UPDATES;

HABARI: Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla aliyepata ajali ya gari amepelekwa Hospitali ya Seliani mkoani Arusha kwa matibabu zaidi.

UPDATES;

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Ndege iliyombeba waziri huyo imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12 jioni, msafara kuondoka kuelekea Muhimbili.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya na mkurugenzi mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru pamoja na jopo la madaktari wamempokea Dk Kigwangalla katika kitengo cha magonjwa ya dharura Muhimbili.

Dk Kigwangalla amepata ajali leo Jumamosi Agosti 4, 2018 eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini

Awali, waziri huyo alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta.

Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba amefariki dunia.

UPDATES:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.

Rais Magufuli ameshirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara.

Ndege hiyo iliwasili majira ya 12 jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
jp.jpg

Hii ni mara ya nne anapata ajali ya gari. Zaidi soma => Mbunge Kigwangala apata ajali mbaya!!

Msafara wa Waziri Kingwangala wategwa mawe, washindwa kupita
 
Back
Top Bottom