Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
MBUNGE CHIKU ABWAO ANUSURIKA KUFA AJALI YA GARI
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasia na maendeo (Chadema) Chiku Abwao amenurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 252 BSX VX ambalo alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kuja Iringa kukwanguliwa na fuso katika eneo la Doma mkoani Morogoro usiku wa leo
Akizungumza na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima leo mbunge huyo alisema kuwa lori hilo aina ya fuso lilimfuata upande wake na kumgonga na kuendelea na safari na kuwa bila umakini wa dereva wake hali ya usalama wake ulikuwa mdogo sana.
Kwani alisema kuwa lori hilo baada ya kukwangua upande wa dereva halikuweza kusimama liliendelea na safari na wao kupelekea taili la moja lilipasuka na kupelekea gari lao kuhama njia .
Hata hivyo alisema katika gari hilo walikuwa yeye na dereva wake na kuwa hakuna aliyejeruhiwa kutokana na kufunga mikanda na kuwa mikanda na mwendo mzuri wa dereva wake ndio umesaidia kupona katika ajali hiyo.
Mkuu huenda alikuwa na mambo yake huko Moro. Halafu pamoja na kwamba Dom - Iringa ni karibu lakini barabara si nzuri watu wanaepusha viuno na migongo yao. Ajali zitatumaliza.Ajali haina kinga, kisa cha kutoka Dodoma ukapita Doma? wakati kuna njia Dodoma - Iringa, shortcut kabisa. Una VX halafu unaona ubahili kulipitisha rough road, faida yake nini kuwa na gari kama hilo?
Distance between Iringa and Dodoma is 177.66 km
Dodoma - Morogoro 224 km - Iringa 242 km Total: 466 k,
Duh naona CHADEMA hamjamaliza kutoana kafara? Who is next?