Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
1,177
3,316
Ilirushwa habari kwenye TBC Aridhio tarehe 9 Novemba 2022 ya mkuu wa mkoa wa Songwe Ndugu Waziri Kindamba akipiga marufuku uchomaji wa mkaa katika mkoa wake. Haya.

Unamwambia mwananchi asitumie mkaa, atatumia nini? Tuwe na uhalisia tuache kufanya maamuzi yasiyotekelezeka. Maandalizi ya nishati mbadala ya kupikia yamefanyika? Tuweke mipango na mifumo mizuri kama tunataka kutumia nishati mbadala (kugawa mitungi ya gesi siyo mipango yenye akili).

Tusipotumia akili tutachochea biashara ya magendo itakayo haribu zaidi mazingira tunayotaka kulinda.
Ni bora wataalamu wetu wafanye tafiti wapate aina ya miti ya kupandwa kwenye mashamba kwa ajili ya kuni na mkaa.

Dunia nzima mkaa na kuni vinatumika, na yapo mapishi usipopikia hii nishati ladha inabadilika. Hata tukihamia kwa wingi kwenye nishati mbadala bado hatutaepuka matumizi ya kuni na mkaa.
 
Anahangaika tu na kutengeneza ulaji kwa maafisa wa serikali kupiga rushwa na kuonea wananchi..angepambana kwanza kuwepo na nishati mbadala yenye bei na fuu na upatikanaji wa haraka na uhakika kuliko mkaa na kuni.

Hakika angeishinda hii vita ya uchomaji mkaa kirahisi mno..shida hawa viongozi wetu nguvu nyingi akili kisoda.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hakika rushwa itashamiri sana.
 
Back
Top Bottom