Mbunge CCM Hamisi Kingwangalla atishia kujiuzuru

• ADAI AMECHOSHWA NA KUNYANYASWA WAPIGA KURA WAKE

na Mustapha Kapalata, Nzega

MBUNGE wa jimbo la Nzega Dk. Hamis Andrea Kigwangalla (CCM), ametishia kujiuzulu ubunge endapo serikali ya chama chake itashindwa kutenda haki kwa wananchi wake.

Mbunge huyo alitoa tishio hilo juzi mara baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Nzega, akikabiliwa na tuhuma za makosa sita, likiwemo la kuvamia Kituo cha Polisi cha wilaya ya Nzega.

Kigwangalla, akiwa na watuhumiwa wenzake watatu, alisema kama suala lake halitafanyiwa uchunguzi na kupata suluhu pamoja na kuangalia haki kwa pande mbili za walalamikaji, atafanya maamuzi mazito.

Alisema hawezi kuendelea kuwa mbunge huku akishuhudia wananchi wake wakinyanyaswa na kunyimwa haki zao na serikali iliyo madarakani kwani mgogoro huo unajulikana hadi ngazi ya juu.

“Kama serikali isipoingilia na kutenda haki kwa wananchi wa Isunga, Ngwanda, Mwabangu na kwa mbunge wao na watu wengine ambao wameshtakiwa bila utaratibu, mimi naweza kuchukua hatua kali zaidi na hata kujivua ubunge kwa sababu siamini katika dhana ya kufanya kazi ya kuwawakilisha wananchi ya kufanya kazi katika mazingira ya dhuruma, unyanyasaji na ukandamizaji usio na maana.

“Bahati nzuri mimi ni mbunge wa CCM na kama Serikali ya CCM ni sikivu, basi leo isikie kilio changu na ifanye maamuzi. Yaliyonikuta na yaliyonitokea ni mazito na siwezi kuvumilia. Mimi kama mimi, nitaamua kujitoa ubunge na pengine kutokugombea nafasi yoyote ile ya uongozi ndani ya chama,” alisema Dk. Kigwangalla.

Mbali ya kutishia kujivua ubunge, mbunge huyo pia alifikia hatua ya kusema kwamba yuko tayari kufa kutetea haki ya wananchi wake dhidi ya manyanyaso ya serikali ya CCM.

Wengine wanaoshtakiwa na mbunge huyo ni Mrisho Hamis, Mathew Dotto na Mwanja Mwandu ambao wote kwa pamoja wanadaiwa kuhamasisha wanakijiji wa Mwabangu kuvamia kituo cha polisi kupinga manyanyaso dhidi ya wachimbaji wadogo wa madini.

Huku ndio kule kule kuwaza kwa kutumia masaburi. Mbunge ulichaguliwa kuwawakilisha na kuwatetea wananchi wa jimbo lako, leo unatishia kujiuzulu kwa sababu tu umetiwa msukomsuko na polisi inashangaza mawazo haya ya kimasaburisaburi. Wewe huoni kuwa ukijiuzulu ndio umewasaliti wale waliokuchagua??? Au wewe ulifikiri kuwatetea wananchi ni kula kuku na kupanda ndege na bakshishi za barick??? Kuwatetea wananchi wako maana yake ni kujitoa mhanga uone haki inatendeka na yale waliyoporwa wanarudishiwa na faida. Mambo wanayofanyiwa wabunge wa vyama vya upinzani kama wote wangewaza kama wewe huo upinzani usingekuwepo leo. Kama kweli wewe ni muwakilishi wa jimbo hilo dawa sio kujiuzulu kwa sababu utawasaliti wapiga kura wako. Unachotakiwa kufanya ni kupambana mpaka kieleweke. Wakikutimua uanachama wa magamba hamia upinzani halafu gombea tena wananchi watakurudisha kwa vile watakuwa wamejenga imani kwako
 
Angekuwa wa kujiuzulu angefanya kama alivyofanya Rostam Aziz. Angefanya maamuzi magumu halafu anatueleza siku ya utekelezaji.
 
Hahahaha anatishia kuachia ushuzi wakati anaharisha! Shauri yake maji yenyewe yamekatika!
 
Hana lolote, ajue kuwa akijiuzuru basi ajue hata leseni yake ya udaktari atanyang'anywa maana anatumia jina la mtu. Hana korodani za kumfanya ajiuzuru, anajikosha tu.
 
Mtu alitishia kujinyonga mpe na kamba ya kujinyongea hatajinyonga kamwe,kama ana piga mkwara wa kujiuzulu aambiwe ruksa,jamaa mwnyewe kigeugeu tushamzoea,bungeni aliponda maandamano huku amesahau kuwa siku chache zilizopita aliongoza maandamano,ajiuzulu tu kama ana ubavu wa kufanya hivyo.
 
Sisi tumetumia kodi nyingi kumsomesha udaktari yeye akaamua kwenda kulala bungeni......arudi haraka sana hospitali kutibu watanzania waliomsomesha
 
Kama anatetea watu wake tumtie moyo, viongozi wengi wamesahau kupigania raia maskini wanaowaongoza. Pigana Kigwan Gala hata kama wewe si tajiri kama Aziz lakini pia kujiuzuru ni vema

Huyu kigwagala hawezi kupigania haki za wananchi wake wanyonge, sababu chombo anachotumia kufiaki malengo yake si sera yake.Ni kama nahodha kulazimisha kufika pwani akiwa baharini kwa kuoegelea bila chombo.Mwisho ni kufia baharini.Akitaka ahame chama, mawili atakuwa kolimba wa pili au kupewa masilahi ya kifisadi anyamaze.Muulize nape mbona hakufanya kapemni igunga wakati yeye ndo mc mkubwa kuliko nchemba?
 
Kama anasimamia anayoyatamka kwa kinywa chake AJIUZURU, zaidi ya hapo ni unafiki na anataka watu wamhurumie.
 
Kama anasimamia anayoyatamka kwa kinywa chake AJIUZURU, zaidi ya hapo ni unafiki na anataka watu wamhurumie.
Anataka huruma ya watu huyo, kama kujiuzuru angejiuzuru kimyakimya kuliko kupiga kelele!
 
Huku ndio kule kule kuwaza kwa kutumia masaburi. Mbunge ulichaguliwa kuwawakilisha na kuwatetea wananchi wa jimbo lako, leo unatishia kujiuzulu kwa sababu tu umetiwa msukomsuko na polisi inashangaza mawazo haya ya kimasaburisaburi. Wewe huoni kuwa ukijiuzulu ndio umewasaliti wale waliokuchagua??? Au wewe ulifikiri kuwatetea wananchi ni kula kuku na kupanda ndege na bakshishi za barick??? Kuwatetea wananchi wako maana yake ni kujitoa mhanga uone haki inatendeka na yale waliyoporwa wanarudishiwa na faida. Mambo wanayofanyiwa wabunge wa vyama vya upinzani kama wote wangewaza kama wewe huo upinzani usingekuwepo leo. Kama kweli wewe ni muwakilishi wa jimbo hilo dawa sio kujiuzulu kwa sababu utawasaliti wapiga kura wako. Unachotakiwa kufanya ni kupambana mpaka kieleweke. Wakikutimua uanachama wa magamba hamia upinzani halafu gombea tena wananchi watakurudisha kwa vile watakuwa wamejenga imani kwako
Umesema kweli, inabidi asikate tamaa maana ameomba kazi mwenyewe!
 
Wabunge wa ccm bana wakiguswa kidogo tu na polisi wanaanza ooh nitajiuzulu. Mambo ya Cdm hamyawezi,unakamatwa, unapigwa ndani,unatoka unachapa kazi unakomaa nayo.
 
Back
Top Bottom