Mimi pia nafahamu sana maeneo hayo, kwakweli barabara ni mbaya sana na inasikitisha. SIYO TU kuanzia Tingi. Kuanzia Njia panda ya kwenda Mbambabay, (Panaitwa Nyoni), Mpapa, Ukuli, Kingirikiti, Makulukulu, Tingi, Ruhindo, Mpepo mpaka dar-pori ( ambapo Komba anapata kura nyingi sana), Barabara inatisha. Kuanzia Ruhindo, Ndondo, Liparamba mpaka mitomoni (huko ndio usiseme). Madaraja ya Lumeme, Ruhindo ni balaa. Safariya Nyoni kwenda Mpepo ( kama kilometa 60 hivi) inachukua zaidi ya masaa matatu/mannekwa gari dogo. Nakiri tu kwa takriban miaka miwili hivi sijapita barabaraza Mbambabay-Kwambe-Chimate(Chiwanda)-Ng'ombo mpaka Chiwindi ( along lakeNyasa), Hali pia ilikuwa mbaya sana.
Ni kweli tarehe hizo ambazo wanajamvi mmezitaja alikuwa huko. Lakini juhudi zake kubwa zilikuwa ni kuhangaika na makanisa tu. Pale Parokia ya Mpepo alisali mkesha siku ya Jumamosi ya tarehe 19/04/2014, Pasaka alikuwa Makulukulu ambako alitoa ahadi za mabati 60 ya kuezekea kanisa, nadhani na kakinanda. Approach ya kutoa elfu 50 kwa baadhi ya watu SIYO NJIA SAHIHI YAKUELEKEA MAENDELEO YA KWELI.
Kwakweli ukimwona Komba anafoka Bungeni, akitishia watukuingia Msituni kwa ajili ya idadi ya serikali, hutaamini siku utakapo kanyaga maeneo ya Jimbo lake, hasa utakapoona tatizo kubwa la barabara.
Limbongambonga umesema hoja ya Chizy za kitaa ni Umbea au vyovyote vile utakavyo amua kuuita. Lakini mimi nadhani ameleta issue ambayo tunaweza kuijadili. Ni wazi tunaweza kuwa na maoni tofauti kwa kadiri ya tunavyoweza kuona mambo na kuyatafakari, Maana sisi ni binanadamu, na si lazima kila tunalosema liwe na maana kubwa (so, ni lazima tuvumiliane), hapa naheshimu maoni ya wenzangu wote hata Nkongu ndasu, Tulimumu, na wengine. Lakini niwaambie tu kuwa, bila ushabiki, Komba ni BOMU kwa jimbo la MbingaMagharibi.
Yapo mambo mengi tunayoweza kujadili, tokea kwenye uwezo wa Komba wa kiutendaji, mpaka kwenye makosa makubwa yaliyofanyika kuligawa Jimbo la Mbinga kwa style ya kufuata maslahi ya wachache wanaotaka kuongoza wengine bila kujali wanawapeleka wapi. I know Mbinga very well, it is one of the very fast growing districts ( hata kabla ya kuigawa kimaslahi). The District has alot of potentials, Ziwa, Madini ya Mpepo, Kahawa, just to mention a few, Ikiunganishwa kwa barabara, Mbinga Magharibi na Mashariki zitakuwa mbali sana. NI HAYO TUKWALEO.