John Komba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Komba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MAMA POROJO, Jul 25, 2010.

 1. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  25th July 2010

  Waandishi wa habari wawili waliokuwa wakifuatilia mchakato wa kampeni za kura za maoni ili kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge wilayani Mbinga kupitia CCM, wamekamatwa na Mbunge aliyekuwa anashikilia Jimbo la Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba na kuwaweka kizuizini kwa madai kuwa ni majambazi waliotumwa kufuatilia msafara wake.

  Waandishi waliokumbwa na mkasa huo ni Godfrey Mushi wa Kampuni ya The Guardian Limited anayeandikia Nipashe na Kassian Nyandindi anayeandikia magazeti ya Majira yaliyopo chini ya Kampuni ya Business Times.
  Waandishi hao ambao waliwekwa kizuizini na mgombea huyo kwa zaidi ya saa 8, hadi walipochukuliwa na Polisi Wilaya ya Mbinga na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi.
  Kabla ya mgombea huyo kuchepuka kinyume cha taratibu katika msafara huo wa wagombea wenzake saba wanaowania nafasi hiyo, alianza kuwafukuza waandishi hao kwa gari lake lenye namba za usajili T 664 BAQ Land Cruiser VX kwa zaidi ya kilometa 30 kutoka yalipo makao makuu ya Hospitali ya Mission ya Mpepo hadi nje ya Kijiji cha Tingi ulipokuwa ukifanyika mkutano mwingine wa kampeni.
  Wakati tafrani hiyo ikitokea, gari la Kapteni Komba lilikuwa likipeperusha bendera na kuwasha taa kuashiria hatari.
  Tukio hilo lilitokea nje kidogo ya mji huo wa Tingi, ambapo gari lililokuwa limewabeba waandishi hao aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 134 ACA, lilimpisha mgombea huyo apite na ndipo aliposimama mbele ya gari lao na kushuka kwa hasira, na kusema "lazima niwamalize na nitawaua" huku akimwamuru dereva wake kufunga barabara kwa kutumia gari lake.

  Baada ya kitendo hicho, gari lililokuwa limewabeba waandishi hao lilirudi kinyume nyume umbali wa kilometa mbili hivi na kupaki karibu na Ofisi za Serikali ya Kijiji cha Tingi ambako kulikuwa kunafanyika mkutano mwingine wa kampeni za wagombea hao ndipo waandishi hao waliposhuka na kujieleza lakini mgombea huyo alidai waandishi hao ni majambazi waliokuwa wakifuatilia msafara wao akidai kuwa wametumwa.

  Majira ya saa 8:10 mchana, Kapteni Komba aliwaita askari wawili wa Jeshi la Wananchi (Jwtz) waliokuwa wamevalia sare za jeshi hilo wakiwa katika kijijini hicho na kuwaamuru kuwashusha waandishi hao ndani ya gari hilo na kuwaweka chini ya ulinzi pamoja na gari lao na baadae kuikabidhi kazi hiyo kwa askari mgambo wanne wa kijiji hicho hadi kikosi cha askari polisi kilipofika kutoka Mbinga Mjini.

  “Hawa ni majambazi ila kazi yao imekwisha maana nitawamaliza, nimeshapiga simu polisi wanakuja, inawezekana wanafanya kampeni au wametumwa kunifuatilia,” alisema Kapteni Komba.

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, polisi zaidi ya sita walifika eneo la tukio hilo majira ya saa 1:30 usiku wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Mbinga Abdalah Mussa na kumhoji Kapteni Komba, viongozi wawili wa msafara huo Wilgis Ndunguru, Beda Hyera na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho cha Tingi.

  Hata hivyo, waandishi hao hawakuchukuliwa maelezo yao hadi walipofikishwa kituo kikuu cha Polisi Wilaya ya Mbinga majira ya saa 5 za usiku na kuachiwa kwa maelezo kwamba wanatakiwa kuripoti asubuhi kituoni hapo.
  Maelezo ya waandishi hao yalichukuliwa majira ya saa tano asubuhi jana.
  Baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo, waandishi hao waliomba kufungua jalada la kutishiwa kuuawa na Kapteni Komba, kudhalilishwa kwa kuitwa majambazi na kisha kuzuiwa kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.

  Hata hivyo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo ASP-Christopher Milinga alikataa kufanyika kwa zoezi hilo akidai wao wamefungua jalada lao la uchunguzi lenye namba MBI/RB/1860/2010 hivyo waandishi hao hawastahili kufungua kesi kwa kuwa Polisi ndiyo itakayochunguza sakata hilo.
  Wagombea wanaomchachafya Kapteni Komba ni Mwandishi wa Habari mkongwe, Alex Shauri, Stanley Vumu, Daudi Haule Dosantos, Monica Chipungahelo na Daniel Magwea ambaye ni Afisa Mipango Mkoa wa Morogoro.

  Hata hivyo, katika mikutano iliyofanyika matawi ya Dar Pori na Mpepo wanachama wa CCM walikuwa wakimzomea Kapteni Komba kila mara kwa madai kwamba ameshindwa kutekeleza ahadi zake alizoahidi tangu mwaka 2005, jambo ambalo lilimfanya apandwe na jazba na kushindwa kujibu swali aliloulizwa kuhusiana na makao makuu ya Wilaya, jina la Wilaya, mgawanyo wa mipaka ya wilaya mpya ya Nyasa na Mbinga ambapo wananchi wanataka muda ukifika wilaya hiyo igawanywe kwa kufuata Jiografia ya maeneo husika, uchumi na makubaliano ya mipaka ya awali.

  Katika tukio jingine, lililowashangaza wanachama wa CCM, mmoja wa viongozi wa msafara huo aliyeteuliwa kuongoza msafara huo Beda Hyera, alishuka katika gari la viongozi wa CCM na kupanda kwa muda gari la Kapteni Komba ambaye ni mgombea bila ya kujua alikuwa akikiuka taratibu na hivyo baadhi ya wagombea kumlalamikia hali hiyo, kwamba huenda mgombea huyo alikuwa akiwarubuni kwa fedha viongozi hao ili wawabane wagombea wengine na kumpa yeye nafasi ya kujitengenezea nafasi ya ushindi.
  Komba alipoulizwa na Nipashe Jumapili kwa njia ya simu jana, kwanza alimtaka mwandishi kueleza alikozipata habari hizo.

  Alipojibiwa kuwa ni kutoka Mbinga, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa vile nafasi yake ni ya mgombea ubunge kama wagombea wengine, hivyo, haimruhusu kufanya hivyo.
  "Mimi ni mgombea kama wagombea wengine, mtafute aliyekwambia hayo. Muulize mkuu wa msafara, polisi, au DC (Mkuu wa Wilaya) wa Mbinga. Usitafute mengine. Gari yao (waandishi) iko polisi, waulize polisi, ndio waliowakamata. Tumeelewana? Uandike kama nilivyosema. Najua unanirekodi na mimi nimekurekodi yote," alisema Komba.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, alithibitisha kukamatwa kwa waandishi hao kwenye msafara wa mwanasiasa huyo.

  Alisema waandishi hao walikamatwa baada ya polisi kupokea simu kutoka kwa baadhi ya watu waliokuwa kwenye msafara huo. Kamanda huyo alisema jana asubuhi waandishi hao walihojiwa na polisi katika kituo cha Mbinga, ambako pia alisema gari lao lilikuwa likishikiliwa.

  "Tunafanya uchunguzi, tunataka kujua nini kilitokea," alisema Kamuhanda.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu tutaona na kusikia vituko vingi vya uchaguzi. Ningekuwa mwandishi ningeandika kitabu na kukiita "Vimbwanga vya uchaguzi"
   
 3. K

  Kibafuta Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kaptn John Kombe maji yameshamfika shingoni hana pa kupulia na kwa kufanya hivyo ndio anazidi kujipaalia makaa bure akubali yaishe. Yeye sindie anaisimamia Bendi ya CCM hicho cheo hakimtoshi..??

  Ameshakula vya kutosha 2005- 2010 awaache na wengine wafaidi Mafao ya kuwa Wabunge kama miaka yote hiyo alishindwa kufanya alichowahaid wananchi wa Mbinga sasa atawezaje kuwatekelezea kwa kuda wa miaka mitani mengine 2010-2015..??
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Heheheeee, atarudi Kukata Kiuno.

  Mwaka huu atakuwa na muda wa kutosha kumwimbia Kikwete kila kona ya Tanzania maana watamgalagaza chali kifo cha mende kwenye chaguzi za CCM. Hawa watu waliambiwa na Mwakyembe kuwa "Watanzania siyo mabwege tena" sijui walifikiri utani?
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hivi kapeteni John Komba ni Mwanajeshi mstaafu kweli ? anaweza kutumika Jeshi ikibidi?mhhh hh yaani mwanajeshi mstaafu tena wa cheo ya kapteni anashindwa kuishi kiafya.

  Ndio yale yale wanayoyasema sio wanayoyatenda. Sasa anapeleka uafande kwenye siasa.
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu kidogo sina ufahamu kuhusu sheria za madaraka ya wabunge. Mbunge ana madaraka yoyote ya kumuweka kizuizini mtu yoyote ikiwa ni pamoja na mwandishi wa habari? au mbunge ana uwezo wa kutoa tishio kwa uhai wa mtu yoyote awe mwandishi wa habari au la? Au kwa kuwa yeye ni mbunge wa CCM yuko juu ya sheria?
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mbunge hana mamlaka hayo, kama ana tatizo na mwananchi yeyote anatakiwa awasilishe shauri lake hilo polisi, au mahakamani.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwa jimwili alilo nalo huyu mbaba, changanya na homa ya uchaguzi nahofia tunaweza kumpoteza kwa presha!...huh!
  Hii ndio tabu ya kushindwa kubadilika...Amejimilikisha jimbo huyu!..bahati mbaya safari hii atalia kilio cha mbwa!
   
 10. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :doh: Matatizo ya kichwa huanza polepole
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kapteni anatumia ustaafu wake kuishi kwa vitisho..huko Mbinga Magharibi itakuwa kivumbi..sio rushwa tena zile za zamani za kuwahonga wananchi "Nyimbo za Hayati Baba wa Taifa"..au "Mgeni huyu Balaaa"...

  Huyo Mangwea msomi wa mipango naona anampa joto na presha kali mcheza ngoma Capt. JK.

  Kama ameshindwa kutekeleza vyema ahadai alizotoa kwa wananchi asitumie jazba na kuwaandama wanaadishi, watamaliza kabisa. Kama hajui kazi ya waandishi ni vizuri akarejea yale ya Uongozi wa Mkoa wa Ruvuma enzi za Nicodemus Banduka na Hayati Adam Mwaibabile wa Radio One (R.I.P) na pia ya Mhe. Saidi Kalembo akiwa Moro...


  [​IMG]
  Mheshimiwa Kapteni Komba-Mbunge wa Mbinga pichani akiserebuka na Mheshimiwa Anna Lupembe.
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  ..........na hapa ndio kwanza wanaanza, sijui mambo yakipamba moto itakuwaje!
   
 13. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Wakuu wizara inalirudia tena tangazo hili:

  TANGAZO TOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
  Tanzania si salama tena na kila mkaaji raia/mwenyeji anapaswa kujilinda mwenyewe, kwani kwasasa geshi la polisi linawalinda baadhi tu ya wagombea wa CCM. Hivyo basi raia na wageni toka nje ya nchi ni jukumu lenu kujilinda wenyewe. Jeshi la polisi/UT na hata JWTZ halitahusika na lolote kwasasa na wala lisilaumiwe. Kubenea na wenzako(waandishi wa habari) ambao hamko kwenye pay-roll ya Mafisi-maji, no Mafisadi Kaeni chonjo.
  MSEMAJI WA WIZARA
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  :tape:
   
 15. k

  kirongaya Member

  #15
  Jul 26, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfa maji, wapo wengi sana siyo komba peke yake, tatizo wanafiri kila siku sikukuu kumbe kila moja ina tarehe yake cha kushukuru kila muda unaposogea wadanganyika sasa wanaelimika na tatizo ubunifu wa kutunga uongo mwingine hawana wanaishia kujishtukia kwa kushika waandishi wa habari kama hivyo, na jeshi la polisi nalo lisikubali kupokea maagizo yasiyo na kichwa wala miguu kumweka mtu siku 8 kisa amesema mbunge ni kudhalilisha jeshi, kila mtu akiwa kiongozi akatoa amri itakua nchi tena hii wafanye kazi kwa nidhamu ya kazi si maagizo hasa kipindi hiki cha uchuguzi.
   
 16. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kombaaa! presha inapanda! presha inashuka! Komba asilaumu sheria za mchezo alaumu uchezaji wake mwenyewe, huyu jamaa hajui nguvu ya media eeh! kalamu ya mwandishi inau kuliko risasi za mwanajeshi, sasa si ameichokoza ngondo asubiri ngodo igwa! Ngoja nimkumbushe Capt. John Damian Komba " Ukitaka kuwa mpishi, usiogope joto la jikoni" kulikoni yeye anaanza kuogopa joto la jikoni?
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
 18. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  :doh: hivi hao wanajeshi walifuat nn kwenye huo msafara wa KOMBA, kazi yao ni kumsikiliza komba na kutii amri ya komba wakati alistastaafu jeshi??? mbona JWTZ mnajidhalaulisha hivo!!! hii inaonyesha jinsi gani mafisadi walivyo na sauti mbele ya pesa haya nawe OCD kwann uwakatalie wananchi kufungua mashtaka polisi wakatu wamatishiwa kuuwawa ana nawe ni mfuasi wa komba??
  kumbukeni mwisho wenu wote mnao watumikia hao mnao waita MABWANA WAKUBWA mafisadi wa CCM mwishowenu ni Octoba 31 DR SLAA atakapo waaibisha kwenye uchaguzi.
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu kama ni kweli nadhani tayari kuna mazingira mazuri ya kumfikisha mahakamani kwa kosa alilofanya. Lakini kwa kuwa ni mbunge wa CCM nadhani tunaweza kusahau hilo, otherwise ajitokeze mgombea mwingine ndani ya CCM atakayeamua kumfikisha mahakamani.
   
 20. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Daniel Mangweha alikuwa Afisa Mipango Dar es salaam enzi ya Makamba...huyu mzee muadilifu sana yaani anachukia rushwa kutoka kwenye damu...John Komba ana kazi ya ziada.
   
Loading...