Mbunge Butondo Ashauri Pembejeo za Kilimo cha Pamba Kutolewa Mapema

Mbunge Butondo Ashauri Pembejeo za Kilimo cha Pamba Kutolewa Mapema

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE BUTONDO ASHAURI PEMBEJEO ZA KILIMO CHA PAMBA KUTOLEWA MAPEMA​

Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Boniphace Butondo ameishauri Serikali kusambaza pembejeo za kilimo cha zao la Pamba kwa wakati ili wakulima waanze maandalizi mapema hali itakayoongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo.

Mhe. Boniphace Butondo Ameeleza hayo wakati akichangia makadirio ya bajeti ya wizara ya kilimo ambapo amebainisha kuwa kuchelewa kwa pembejeo hizo kunapunguza uzalishaji wa pamba zenye ubiora.

Katika hatua nyingine, Mhe. Boniphace Butondo ameiomba Serikali kuurejesha mpango wa awali uliokuwa na lengo la kuanzisha mfuko wa kulinda bei ya zao la hilo.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-05-25 at 14.55.38.mp4
    49.7 MB
Back
Top Bottom