Mbunge Azan Zungu aboronga Bungeni

Mbunge Azan Zungu aboronga Bungeni

kisugujira

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2012
Posts
774
Reaction score
200
Kutokuwa na busara na hekima kwa viongozi wetu kutaendelea kuleta matatizo na kutoelewana miongoni mwetu katika nchi yetu iliyokuwa na amani Tanzania.

Leo hii katika mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi 2013-2014, mbunge wa Ilala Azan Zungu, amesababisha kutokea kwa kelele bungeni zilizotokana na minong'ono toka kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge hasa toka vyama vya upinzani, baada ya kutangaza na kuwatambulisha vijana wawili, Mwampamba na Juliana Shoza waliohama toka CHADEMA na kujiunga na CCM!

Bila ya kutokuwa na haya, mbunge huyo amediriki pia kuwataka wanafunzi wa shule ya msingi Ilala wakue haraka ili waje kumpigia kura siku zijazo! Ameshindwa kuwaasa wanafunzi hao waliokwenda bungeni kujifunza, kuwa wasome sana ili kesho waje kuwa viongozi bora na waadilifu katika nchi! Badala yake anawafundisha kuwa na tamaa ya kukaa madarakani kwa muda mrefu!

"Leave your mark where others can only dream on going."
 
Mlishaambiwa kuwa kuna wabunge wanafanya biashsra ya kuuza madawa ya kulevya ambao baba MwanaAsha anawafahamu lakini anawalinda!!!
 
Kutokuwa na busara na hekima kwa viongozi wetu kutaendelea kuleta matatizo na kutoelewana miongoni mwetu katika nchi yetu iliyokuwa na amani Tanzania.

Leo hii katika mjadala wa bajeti ya wizara ya uchukuzi 2013-2014, mbunge wa Ilala Azan Zungu, amesababisha kutokea kwa kelele bungeni zilizotokana na minong'ono toka kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge hasa toka vyama vya upinzani, baada ya kutangaza na kuwatambulisha vijana wawili, Mwambapa na Juliana Shoza waliohama toka CHADEMA na kujiunga na CCM!

Bila ya kutokuwa na haya, mbunge huyo amediriki pia kuwataka wanafunzi wa shule ya msingi Ilala wakue haraka ili waje kumpigia kura siku zijazo! Ameshindwa kuwaasa wanafunzi hao waliokwenda bungeni kujifunza, kuwa wasome sana ili kesho waje kuwa viongozi bora na waadilifu katika nchi! Badala yake anawafundisha kuwa na tamaa ya kukaa madarakani kwa muda mrefu!

"Leave your mark where others can only dream on going."
Hizi ni dharau yaani anamaanisha hao wanafunzi wakue wawe wapiga kura wake anaamaanisha wao hawatafaa kuwa viongozi wakiwa watu wazima ila watakuwa wapiga kura tuu, hivi hii mijitu ya CCM mbona inajisahau sana??? hebu fikiria kwa mtu mwenye akili timamu atasemaje Mwampamba na Juliana wamehama Chadema ilihali wamefukuzwa? Na hawa watu wawili wana umuhimu gani mpaka wakatangazwa kama watu special? mbona anapafanya bungeni pawe kama kijiwe cha wahuni?
 
Anachowaza Zungu ni kuwa 2015 agombee
tena Ubunge maana kaongea kama hajijui
vile eti Kueni mje mnipigie Kura.
 
Kilicho Nishangaza Ni Watoto Wa Shule Ya Msingi Kwa Makadilio Ni Kati Ya Miaka 7-14. Sasa Zungu Anazani Ilala Itakua Yake Milele
 
Zungu ni mfadhiri na mwezeshaji mkuu wa vijana waleta unga toka ugaibuni. Anastahili kuhojiwa!!
Pili kaleta mpasuko mkubwa ndani ya UVCCM kwani wale wengine wamejina hawana umuhimu kama walionao Shonza na Mwampamba; vijana wanapanga kususia kazi waone kama hawa wateule wapya wa ccm walofukuzwa CHADEMA waweza kufanikisha kampeni za udiwani zinazokuja mwezi ujao.
 
Kweli ni ukosefu wa hekima. hasa hapo kwenye suala la wanafunzi
 
Hizi ni dharau yaani anamaanisha hao wanafunzi wakue wawe wapiga kura wake anaamaanisha wao hawatafaa kuwa viongozi wakiwa watu wazima ila watakuwa wapiga kura tuu, hivi hii mijitu ya CCM mbona inajisahau sana??? hebu fikiria kwa mtu mwenye akili timamu atasemaje Mwampamba na Juliana wamehama Chadema ilihali wamefukuzwa? Na hawa watu wawili wana umuhimu gani mpaka wakatangazwa kama watu special? mbona anapafanya bungeni pawe kama kijiwe cha wahuni?

Ujinga uco na hasara ni bora kuliko elimu icyo na faida.
 
Kwani kosa lake nini mbona wabunge wengine huwa wanatambulisha wake na shemeji zao!
 
it is not every destined to stand out from the crowd; we have real very few leaders, but a lot wants to lead; generous people are chosen to lead!
 
Hizi ni dharau yaani anamaanisha hao wanafunzi wakue wawe wapiga kura wake anaamaanisha wao hawatafaa kuwa viongozi wakiwa watu wazima ila watakuwa wapiga kura tuu, hivi hii mijitu ya CCM mbona inajisahau sana??? hebu fikiria kwa mtu mwenye akili timamu atasemaje Mwampamba na Juliana wamehama Chadema ilihali wamefukuzwa? Na hawa watu wawili wana umuhimu gani mpaka wakatangazwa kama watu special? mbona anapafanya bungeni pawe kama kijiwe cha wahuni?

Tangu hapo, Bunge lenyewe linaendeshwa na wahuni kichwa cha CCM
 
Back
Top Bottom