Mbunge avamiwa, aporwa bastola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge avamiwa, aporwa bastola

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Boflo, May 8, 2010.

 1. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Suzy Butondo na Shija Felician, Shinyanga
  MBUNGE wa jimbo la Bukombe mkoani hapa, Emmanuel Luhahula juzi alivamiwa na majambazi waliompora fedha taslimu na vitu vingine, ikiwemo bastola ambayo aliporwa baada ya kushindwa kuitumia.

  Kabla ya uporaji huo, majambazi hayo yalimshambulia mbunge huyo pamoja na katibu wa CCM wa wilaya ya Bukombe, Mberito Magova, ambaye alikuwa akisafiri naye, kwa kuwakata na mapanga

  Kwa mujibu wa habari hizo mbali na bastola hiyo majambazi hao pia walimpora mbunge huyo fedha taslimu takriban Sh14 milioni zilizokuwa katika dola 10,000 za Kimarekani na Sh50,000 za Kitanzania pamoja na simu mbili za mkononi.

  Kabla ya kuwapora mali hizo, majambazi hao waliwashambulia viongozi hao wa chama na serikali kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili. Imesemekana kuwa dereva wao alifanikiwa kuwakimbia watekaji hao.

  Katibu wa CCM, Mberito Magova aliliambia gazeti hili jana kuwa walikutwa mkasa huo majira ya saa 3.15 usiku wa kuamkia jana kwenye eneo la Kijiji cha Nasikukulu wilayani Bukombe wakati walipokuwa wanatokea Kahama kwenda Bukombe.

  Alisema walipokaribia eneo la tukio walikuta mawe barabarani na kulazimika kusimama na ndipo majambazi hao sita walipowavamia na kuwapiga.

  “Tukiwa hatujui tufanye nini, majambazi hao walituteka na kutuamuru kuteremka; ile kushuka tu, walianza kutushambulia kwa kutupiga marungu na mapanga,” alieleza katibu huyo wa CCM.

  Alisema mbuge huyo alijaribu kupiga risasi hewani ili kuwatishia majambazi hao wakimbie, lakini risasi ziligoma na ndipo waporaji walipompora bastola na baadaye kuwanyang’anya simu za mikononi na fedha.

  “Baada ya kumpora bastola mbunge, majambazi hao walianza kuitumia papo hapo... walifyatua risasi hewani na kuteka magari mengine yaliyokuwa yakitokea Kahama kuelekea Bukombe,” alieleza Magova.

  Alisema katika uvamizi huo yeye (Magova) alijeruhiwa kichwani na ameshonwa nyuzi tano. Alisema amepata maumivu zaidi miguuni na maeneo mengine ya mwili.

  “Mheshimiwa mbunge alikatwa panga sehemu za kichwani, mkono wake wa kulia wakati akiporwa bastola na mgongoni, lakini hali yake siyo mbaya sana, japo hivi tunapoongea (saa 4.59 asubuhi) alikuwa bado yupo chumba cha upasuaji akipatiwa matibabu,” alieleza.

  Alisema yeye na mbunge huyo wote walipatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, Shinyanga.

  Alisema katika tukio hilo majambazi hao pia walitumia bastola ya mbunge huyo kuteka lori na katika purukushani hizo, ndipo waliwatoroka na kukimbilia porini ambako baadaye waliomba msaada.

  “Bahati nzuri dereva wetu alipata gari lililopenya katika kizuizi hicho na kwenda kutoa taarifa kwa polisi wa Bukombe ambao walifika na kutoa msaada zaidi,” alieleza Magova.

  Alisema baada ya muda mfupi, polisi pamoja na wanakijiji walifika eneo hilo na ndipo walipokimbizwa hospitalini.

  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na wanaendelea na msako wa watu waliohusika
  SOURCE: Mwananchi
   
 2. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #2
  May 8, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Pole sana Bro. Nakutakia a quick recovery.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  May 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  .

  Duh..Haya mbunge ana dollar 10,000 za Kimarekani nyumbani kwake! - Wapi?...Bukombe!
  kaazi kweli kweli!
   
 4. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #4
  May 8, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini watu wanatunza mapesa kiasi hicho majumbani mwao?
  Unakumbuka kisa kilichompata mke wa Andrew Daraja?

  Labda mapesa hayo ni kwa ajili ya michakatuo ya uchaguzi mkuu ujao!
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  poleni sana majeruhi wote, ila mh, mbunge na liwe fundisho dola elfu kumi unatembea nazo kama njugu?
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nampa pole sana. hizo dola elfu kumi alikuwa na mpango wowote wakufanyia kitu bukombe nini, labda eneo hilo wanatumia dola badala ya shilingi. nafikiri wafanye utafiti tu, pengine si majambazi ila in visa vya kisiasa, si unajua tunakaribia uchaguzi hivyo kuna uwezekano kukawa na visa vingi tu vya kutumiwa majambazi nk. wenye vyeo humu ndani kuweni macho.
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  May 9, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wahanga.hayo ni madhara ya watu walioahidiwa ahadi hewa za maisha bora kwa kila mtanzania

  Hata hivyo,ni aibu Mbunge mzima kutembea na dola au let me hope ulikua na nia ya kuzitumia nje ya nchi lakini kama matumizi yake yalikua yatumike hapa Tanzania ktk transaction za kawaida,basi tuna kazi.wabunge wanashiriki uhujumu uchumi?let me be fair,nakupa benefit of doubt
   
 8. b

  bwanashamba Senior Member

  #8
  May 9, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  silaa alikua nayo risasi zikagoma kutoka lakini silaha iyoiyo iliposhikwa na jambazi
  risasi zilitoka je uyo mbunge anajua kuitumia iyo silaaa kisawasawa?/////////////:help:
   
 9. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  bastola za madoido,unanunua silaha kwa maonyesho tu na kutishia watu,tukio hili liwe funzo kwa wamiliki wa silaha ambao hawafanyi practice ktk range,hawazitunzi jinsi inavyotakiwa ndo maana risasi imegoma kutoka,
  Dola Elfu 10. zote hizi alikuwa akipeleka ktk kuwanunua wanaCCJ,or sorry wana
  CCM ili aendelee an ubunge.
  pole sana Mr.Mbunge,na pole wote mlijeruhiwa ktk msafara huo,i wish them a quick recovery.
   
 10. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  hiyo ilikuwa ni fedha ya kawaida kabisa ya mbunge wa Tanzania, nadhani ilikuwa ni pesa ya matumizi ya kawaida kabisa ya mwisho wa wiki,

  Mshahara wake na marupurupu unaujua wewe?, hiyo ni pesa kwako wewe unaepata KCC cha 114000Tsh kwa mwezi, lakini kwa Wabunge mshahara na marupurupu unaozidi 10mTsh kwa mwezi bado ni mdogo na wanahitaji nyongeza.
   
 11. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,778
  Likes Received: 20,713
  Trophy Points: 280
  matumizi ya kawaida ya mwisho wa wiki ya $10,000,mfano?
   
 12. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #12
  May 9, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,778
  Likes Received: 20,713
  Trophy Points: 280
  mh kazi kwelikweli,lakini bastola huwa ina lock ili usije kujipiga bahati mbaya,sasa nafikiri katika purukushani alipanic hata hakukumbuka ku-unlock hio bastola,i guess.
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  MBUNGE wa jimbo la Bukombe mkoani hapa, Emmanuel Luhahula juzi alivamiwa na majambazi waliompora fedha taslimu na vitu vingine, ikiwemo bastola ambayo aliporwa baada ya kushindwa kuitumia.

  Kabla ya uporaji huo, majambazi hayo yalimshambulia mbunge huyo pamoja na katibu wa CCM wa wilaya ya Bukombe, Mberito Magova, ambaye alikuwa akisafiri naye, kwa kuwakata na mapanga

  Kwa mujibu wa habari hizo mbali na bastola hiyo majambazi hao pia walimpora mbunge huyo fedha taslimu takriban Sh14 milioni zilizokuwa katika dola 10,000 za Kimarekani na Sh50,000 za Kitanzania pamoja na simu mbili za mkononi.

  Kabla ya kuwapora mali hizo, majambazi hao waliwashambulia viongozi hao wa chama na serikali kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili. Imesemekana kuwa dereva wao alifanikiwa kuwakimbia watekaji hao.

  Katibu wa CCM, Mberito Magova aliliambia gazeti hili jana kuwa walikutwa mkasa huo majira ya saa 3.15 usiku wa kuamkia jana kwenye eneo la Kijiji cha Nasikukulu wilayani Bukombe wakati walipokuwa wanatokea Kahama kwenda Bukombe.

  Alisema walipokaribia eneo la tukio walikuta mawe barabarani na kulazimika kusimama na ndipo majambazi hao sita walipowavamia na kuwapiga.

  “Tukiwa hatujui tufanye nini, majambazi hao walituteka na kutuamuru kuteremka; ile kushuka tu, walianza kutushambulia kwa kutupiga marungu na mapanga,” alieleza katibu huyo wa CCM.

  Alisema mbuge huyo alijaribu kupiga risasi hewani ili kuwatishia majambazi hao wakimbie, lakini risasi ziligoma na ndipo waporaji walipompora bastola na baadaye kuwanyang’anya simu za mikononi na fedha.

  “Baada ya kumpora bastola mbunge, majambazi hao walianza kuitumia papo hapo... walifyatua risasi hewani na kuteka magari mengine yaliyokuwa yakitokea Kahama kuelekea Bukombe,” alieleza Magova.

  Alisema katika uvamizi huo yeye (Magova) alijeruhiwa kichwani na ameshonwa nyuzi tano. Alisema amepata maumivu zaidi miguuni na maeneo mengine ya mwili.

  “Mheshimiwa mbunge alikatwa panga sehemu za kichwani, mkono wake wa kulia wakati akiporwa bastola na mgongoni, lakini hali yake siyo mbaya sana, japo hivi tunapoongea (saa 4.59 asubuhi) alikuwa bado yupo chumba cha upasuaji akipatiwa matibabu,” alieleza.

  Alisema yeye na mbunge huyo wote walipatiwa matibabu Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, Shinyanga.

  Alisema katika tukio hilo majambazi hao pia walitumia bastola ya mbunge huyo kuteka lori na katika purukushani hizo, ndipo waliwatoroka na kukimbilia porini ambako baadaye waliomba msaada.

  “Bahati nzuri dereva wetu alipata gari lililopenya katika kizuizi hicho na kwenda kutoa taarifa kwa polisi wa Bukombe ambao walifika na kutoa msaada zaidi,” alieleza Magova.

  Alisema baada ya muda mfupi, polisi pamoja na wanakijiji walifika eneo hilo na ndipo walipokimbizwa hospitalini.

  Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa na wanaendelea na msako wa watu waliohusika

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/1439-mbunge-avamiwa-aporwa-bastola
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Bukombe (CCM), Emmanuel Luhaula  Mbunge wa Bukombe (CCM), Emmanuel Luhaula, ambaye alivamiwa na majambazi juzi usiku na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, anaendelea vizuri.
  Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana katika Taasisi ya Mifupa (MOI) alikolazwa kwa matibabu zaidi, Luhaula alisema baada ya kupatiwa matibabu, hali yake imeanza kuimarika.
  “Namshukuru sana Mungu kwa kuniona, bila yeye nisingekuwa hapa leo maana kwa muujiza wake wale watu baada ya kupora bastola yangu hawakunidhuru nayo, waliitumia kuteka magari mengine,” alisema.
  Alisema maumivu anayosikia kwa sasa ni mkono wa kulia na kichwani ambako alijeruhiwa zaidi.
  “Naendelea vizuri lakini maumivu ni kwenye mkono wa kulia ambao vidole vimeumia sana, kichwani na kinywani (meno),” alisema.
  Luhaula alivamiwa akiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kahama, Mberito Magova, usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Nasikukulu kilichopo wilayani Bukombe, mkoani Shinyanga.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Duh Pole Sana Mbunge Sijuwi hili Tatizo la Ujambazi Litaisha lini Tanzania?
   
Loading...