Mbunge ataka wafungwa waende gerezani na magodoro

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Songwe Neema Gerald, amesema kuwa ili kuipunguzia serikali mzigo wa kununua magodoro kwa ajili ya wafungwa na mahabusu gerezani, basi ione haja ya wafungwa hao kuwa wanaenda na magodoro yao.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Songwe Neema Gerald

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo hii leo Septemba Mosi, 2021, Bungeni Jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

"Tunafahamu kabisa Magereza kuna changamoto ya magodoro na serikali inawajibika kuhakikisha magodoro yanakuwepo, sasa haioni haja ya mahabusu au wafungwa wote wakawa na kigezo cha kwenda na magodoro yao ili waweze kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro Gerezani, kwa sababu siyo wote wanashindwa kuwa na magodoro kuliko kuiongezea serikali mzigo," amesema Mbunge Neema
 
Kama wanayo waende nayo tu
 
Ni kweli! Na mimi naunga mkono.
 
"Tunafahamu kabisa Magereza kuna changamoto ya magodoro na serikali inawajibika kuhakikisha magodoro yanakuwepo, sasa haioni haja ya mahabusu au wafungwa wote wakawa na kigezo cha kwenda na magodoro yao ili waweze kupunguza changamoto ya upungufu wa magodoro Gerezani, kwa sababu siyo wote wanashindwa kuwa na magodoro kuliko kuiongezea serikali mzigo," amesema Mbunge Neema
wacha weeee.,!¡!!!

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…