Mbunge ataka kiswahili kitumika hadi vyuo vikuu


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,490
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,490 280MBUNGE wa Karagwe, Gosbert Blandes (CCM), amehoji lini serikali itapitisha Kiswahili kitumike kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu. Aidha, alisema mwaka 2004, Umoja wa Afrika ulipitisha Kiswahili kiwe ni lugha ambayo itatumika katika mikutano na shughuli mbalimbali."Je, serikali imejiandaa vipi kupeleka wakalimani wa kutosha kutoka Tanzania ili waweze kujipatia ajira?" alihoji.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala alisema jitihada zinafanywa na taasisi hizo za kukuza Kiswahili mojawapo kuandika vitabu vingi vya kufundishia na kuongeza wataalamu.


"Nasema wazo hilo tumelipokea na sisi ndani ya serikali tunaendelea kulifanyia kazi na hata wakati tunawasilisha bajeti yetu zilitoka hoja hizo za kuwa Kiswahili kifundishwe madarasani," alisema.


Aidha, Makala alikiri kupitishwa kwa azimio hilo na kuongeza kuwa:


"Kama Tanzania tumeona kuwa hii ni fursa muhimu na tayari moja ya kazi zinazofanywa na Taasisi za kukuza Kiswahili, BAKITA, BAKIZA ni kuongeza wataalamu zaidi ili waweze kupata ajira hiyo."
Aliongeza kuwa Tanzania kama Tanzania mjini Addis Ababa kuna kituo cha kufundishia lugha ya Kiswahili. Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) alitaka kufahamu kama nchini Tanzania kuna Sera ya Lugha.


Pia, alihoji kama ipo, je, sera hiyo ya Lugha imeipatia hadhi gani lugha ya Kiswahili.
Aidha, alitaka kujua kuna mkakati gani mahsusi wa kuifanya Lugha ya Kiswahili kuwa ya kufundishia kwa viwango vyote vya elimu hapa nchini.


Akijibu swali hilo, Makala alisema Tanzania hakuna andiko mahususi au linalosimama pekee kama Sera ya Lugha, bali suala la lugha limezingatiwa kama Sura maalumu muhimu ndani ya Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997.
Alisema katika andiko hilo la sera ya Utamaduni, Kiswahili kimetambuliwa kuwa siyo tu lugha ya mawasiliano mapana nchini bali pia ni lugha ya taifa na mojawapo ya lugha rasmi mbili za Taifa.
Aidha, alisema miongoni mwa mikakati mahsusi ya kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni jitihada zinazoendelea za wataalamu wa Asasi za ukuzaji wa Kiswahili nchini ambazo ni kuboresha sarufi ya Kiswahili, kutunga Kamusi za Kiswahili za masomo na taaluma mbalimbali.MBUNGE ATAKA KISWAHILI KITUMIKA HADI VYUO VIKUU - MPEKUZI HURU
 
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Messages
1,625
Likes
75
Points
145
Age
44
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2013
1,625 75 145
If you import teachers, books and technology how can you use your native language to learn, a very stupid opinion ever given by an mp on the planet earth.
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,563
Likes
1,604
Points
280
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,563 1,604 280
Nilijua tu lazima atakuwa mbunge wa ccm...rais wake anaomba walimu jamaica yeye anaongelea kiswahili..yaaani nchi hii ya majuha kwa kweli daaah
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,490
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,490 280
Nilijua tu lazima atakuwa mbunge wa ccm...rais wake anaomba walimu jamaica yeye anaongelea kiswahili..yaaani nchi hii ya majuha kwa kweli daaah
Mkuu Yaya Toure Wewe hutaki lugha yako iwe ndio inazungumzwa dunia pote kuanzia nchini mwako?
 
Last edited by a moderator:
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
1,189
Likes
3
Points
0
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
1,189 3 0
If you import teachers, books and technology how can you use your native language to learn, a very stupid opinion ever given by an mp on the planet earth.
You are absolutely right, indeed, all African countries use foreign languages as a means of instruction at University level. Basically, Tanzania will completely kicked out of the world of competition when such silly decisions come to be in place. We expected to find visionary leaders who will engineer the process to making our education wholly provided in English and french be solo (option) subject, not otherwise.
 
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
1,189
Likes
3
Points
0
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
1,189 3 0
Mkuu Yaya Toure Wewe hutaki lugha yako iwe ndio inazungumzwa dunia pote kuanzia nchini mwako?
Nilipanga kukupa maneno makali sana lakini bahati njema niko katika funga za sunna na ni miongoni mwa member naowaheshimu sana humu JF. Ukweli ni kwamba hakuna vigezo vitakavyoifanya lugha ya kiswahili itumike(sio izungumzwe) duniani kote. Nadhani utakubaliana nami, pamoja na nchi za Japan, China na Korea kutumia Lugha zao na kuwa na maendeleo makubwa, lakini nchi hizi zina idadi kubwa sana ya vyuo vinavyotoa na kuendelea kukuza Lugha ya Kiingereza katika nchi zao. Vilevile, haina ubishi kwamba wataalamu wengi wa nchi hizi na graduates wa USA, UK na Canada ndio wanaotoa mchango mkubwa katika kuandaa mikakati ya kimaendeleo ya kimataifa. Tusifanye mchezo na Lugha jamani, hii lugha ya kulia ubwabwa hii haina nafasi kwa kweli duniani-tuache siasa
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,553
Likes
2,374
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,553 2,374 280
Hivi hawa watu wanakazana na Kiswahili ili kitupeleke wapi? No wonder watz wanashindwa kuingia kwenye soko la ajira hasa Kenya na Uganda kwasababu ya kutokuwa fluent kwenye Lugha za maana. Who would dare to opt for the language born in Tz, assassinated in Kenya and buried in Uganda?
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,028
Likes
5,490
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,028 5,490 280
Nilipanga kukupa maneno makali sana lakini bahati njema niko katika funga za sunna na ni miongoni mwa member naowaheshimu sana humu JF. Ukweli ni kwamba hakuna vigezo vitakavyoifanya lugha ya kiswahili itumike(sio izungumzwe) duniani kote. Nadhani utakubaliana nami, pamoja na nchi za Japan, China na Korea kutumia Lugha zao na kuwa na maendeleo makubwa, lakini nchi hizi zina idadi kubwa sana ya vyuo vinavyotoa na kuendelea kukuza Lugha ya Kiingereza katika nchi zao. Vilevile, haina ubishi kwamba wataalamu wengi wa nchi hizi na graduates wa USA, UK na Canada ndio wanaotoa mchango mkubwa katika kuandaa mikakati ya kimaendeleo ya kimataifa. Tusifanye mchezo na Lugha jamani, hii lugha ya kulia ubwabwa hii haina nafasi kwa kweli duniani-tuache siasa
Mkuu Zinedine Ungenipa maneno makali sio kunitukana hata Allah subhana wataala hapendi maneno ya matusi. Sisi Wa Afrika tutakuwa siku zote ni Watumwa wa watu weupe wenzetu huku wanatumia Lugha zao sisi

bado tunataka iwe lazima Lugha ya kiingereza ndio iwe lugha ya Taifa ? Kwani kujuwa lugha ya kiingereza ndio kusoma au ndio kuwa na Elimu? elimu mbali na lugha mbali Warusi wanatumia lugha yao mbona wana Elimu kubwa Duniani? Wajerumani wanatumia lugha

yao mbona wana Elimu kubwa duniani? Wa Sweden Wa Norway Wa Denmark wote wanatumia lugha yao mbona nao ni Matajiri Duniani? Wa Saudia Wa kuweti mbona wanatumia Lugha zao mbona nao ni Matajiri sana Duniani? Mkuu acha mambo

yako ya Utumwa Lugha ya kiswahili ipewe kipa umbele na lugha ya kiingereza iwepo pia ninaunga mkono lugha zote mbili zitumike Mashuleni mpaka Kwenye Vyuo vikuu. Tembea ujionee wewe mwenyewe Lugha ya Kiingereza ni Lugha ya kibiashara na mawasiliano tu huku Ulaya kila nchi wanatumia lugha zao za asili.
 
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
1,189
Likes
3
Points
0
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
1,189 3 0
Mkuu Zinedine Ungenipa maneno makali sio kunitukana hata Allah subhana wataala hapendi maneno ya matusi. Sisi Wa Afrika tutakuwa siku zote ni Watumwa wa watu weupe wenzetu huku wanatumia Lugha zao sisi

bado tunataka iwe lazima Lugha ya kiingereza ndio iwe lugha ya Taifa ? Kwani kujuwa lugha ya kiingereza ndio kusoma au ndio kuwa na Elimu? elimu mbali na lugha mbali Warusi wanatumia lugha yao mbona wana Elimu kubwa Duniani? Wajerumani wanatumia lugha

yao mbona wana Elimu kubwa duniani? Wa Sweden Wa Norway Wa Denmark wote wanatumia lugha yao mbona nao ni Matajiri Duniani? Wa Saudia Wa kuweti mbona wanatumia Lugha zao mbona nao ni Matajiri sana Duniani? Mkuu acha mambo

yako ya Utumwa Lugha ya kiswahili ipewe kipa umbele na lugha ya kiingereza iwepo pia ninaunga mkono lugha zote mbili zitumike Mashuleni mpaka Kwenye Vyuo vikuu. Tembea ujionee wewe mwenyewe Lugha ya Kiingereza ni Lugha ya kibiashara na mawasiliano tu huku Ulaya kila nchi wanatumia lugha zao za asili.
Mkuu, kukutukana sintoweza na haitatokea. Lakini! kwani lugha hasa ni nini? unadhani kuna tofauti gani ya anaeomba maji kwa kisukuma, kiingereza, kiswahili na kichina? Binafsi sina tatizo na kiswahili kama lugha, nina tatizo na kiswahili kama lugha ya nyenzo(tool) katika dunia tulionayo sasa, wazo hili lilifaa lifanyike immediately baada ya uhuru lakini si kwa sasa. Dunia kwa sasa haitoi tena nafasi ya nchi mpya kufanya "invention" bali kutafuta namna ya kufanya adaptation, imitation na innovation, hivyo nafasi ya kiswahili kama nyenzo ya kuweza kuhimili changamoto za utandawazi ni kujidanganya kitu ambacho mimi siwezi. Suala lingine, kama tunaamini Kiswahili ni bora kwa wakati huu, kwanini hao watetezi watoto wao wote wako English medium? wanafanya nini huko? kwanini wasiwapeleke "Shule za kisasa za kimataifa za kiswahili"? Nini tatizo? Naelewa vema, hata hapa Australia hawa wenyeji wana lugha yao lakini Lugha ya kufundishia ni Kiingereza ambacho kimetokana na asili ya ukoloni wao wa kiingereza, mbona maendeleo yapo? Naelewa sana nchi nyingi zilizoendelea zinatumia Lugha zao lakini nchi ZOTE zilizotawaliwa zinatumia Lugha za watawala wao( Amerika kusini yote, Marekani yenyewe, Australia, India, na nikakutolea mfano wa Afrika hakuna nchi yoyote inayotumia Lugha yake ya asili kufundishia, huu uspeciality wa Tanzania unatoka wapi? Ni nini kinachowanya nyie watu muwe special? Kwani kuondoa matatizo ya umaskini kunahitaji Lugha maalum tu? No! Ila tukubali kiingereza kiko karibu zaidi katika kutatua na kuishirikisha nchi katika kukabiliana na changamoto za dunia ya leo. Too late kufikiria lugha ya kufundishia leo kwa sababu nimekupa na mifano ya nchi hizo za Japan, Korea na China ambazo nimeishi na pamoja na kutumia lugha zao lakini zina idadi kubwa ya watu wao wanaowapeleka kusoma katika Shule za Marekani, Ulaya Canada na hapa Australia kwa pesa zao ambazo nyie watanzania hamna mnategemea udhamini wao ambao wanawataka muweze kujua kiingereza. Vilevile katika hizo nchi za huko Asia, kuna juhudi kubwa sana za kuimarisha mitaala yao ya elimu kuwawezesha kujua kiingereza na haishangazi vijana wengi wanaomaliza shule zao katika nchi hizo wanaongea kiingereza. Elimu ndiyo nyenzo kuu siku hizi ambayo imerahisishwa kupitia vyombo mbalimbali ikiwemo mawasilino ya Internet. Hebu niambie material gani ya msingi na muhimu yaliyoandikwa kwa kiswahili utakayoweza kuyapata kupitia Google? Na ni mkakati gani wa Serikali utakaowezesha ku-upload kiswahili materials ili vijana wetu wa kitanzania waende sambamba na kile kinachojadiliwa duniani? Ni wasomi gani hao tulionao wanaoweza kufanya kazi hiyo? Au wale wanaopiga kelele pale Radio One siku za Jumamosi? Umewahi kukutana na ile kamusi ya Kiswahili/Kiingereza ya TUKI, na hiyo kashfa ya juzi ya upotoshaji wa vitabu vya shule za msingi huko Tanzania unaichukuliaje? Tuacheni blabla ambazo zinatuchelewesha siku zote, tujadilini vitu vikubwa na tuache kujifananisha na developed countries wewe unajua namna tulivyotofautiana kiuchumi.
 
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Messages
1,625
Likes
75
Points
145
Age
44
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2013
1,625 75 145
hivi hawa watu wanakazana na kiswahili ili kitupeleke wapi? No wonder watz wanashindwa kuingia kwenye soko la ajira hasa kenya na uganda kwasababu ya kutokuwa fluent kwenye lugha za maana. Who would dare to opt for the language born in tz, assassinated in kenya and buried in uganda?
ni kweli wakenya kile kiswahili chao ni grammatical suicide
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
107,643
Likes
132,533
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
107,643 132,533 280
Tusikibeze kiswahili, ni lugha yetu ni utambulisho wetu, tuwekeze katika lugha yetu hiyo ni tunu ya taifa lakini vile vile tunazihitaji lugha nyinginezo za kimataifa ili tuweze kwenda sawa na utandawazi
Tusijaribu kujenga hoja kuwa lugha yetu si bora na kiingereza ndio bora tutapotea na mwisho wa Siku tutakipoteza kiswahili na kubaki na kiswakinge
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
107,643
Likes
132,533
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
107,643 132,533 280
ni kweli wakenya kile kiswahili chao ni grammatical suicide
Hivi kumbe kiingereza ni lugha ya maana kuliko kiswahili? Umenifumbua macho, na pia nakushauri Siku nyingine uchangie mada zako kwa kiingereza utakuwa umemaanisha na unachokinena la sivyo.....?
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
107,643
Likes
132,533
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
107,643 132,533 280
If you import teachers, books and technology how can you use your native language to learn, a very stupid opinion ever given by an mp on the planet earth.
By using foreign language your will always be a slave, we must not be brainwashed by foreign languages especially english!!! By woshipping english you are a condemned citizen
 
Ndoa

Ndoa

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Messages
997
Likes
23
Points
35
Ndoa

Ndoa

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2011
997 23 35
nilipanga kukupa maneno makali sana lakini bahati njema niko katika funga za sunna na ni miongoni mwa member naowaheshimu sana humu jf. Ukweli ni kwamba hakuna vigezo vitakavyoifanya lugha ya kiswahili itumike(sio izungumzwe) duniani kote. Nadhani utakubaliana nami, pamoja na nchi za japan, china na korea kutumia lugha zao na kuwa na maendeleo makubwa, lakini nchi hizi zina idadi kubwa sana ya vyuo vinavyotoa na kuendelea kukuza lugha ya kiingereza katika nchi zao. Vilevile, haina ubishi kwamba wataalamu wengi wa nchi hizi na graduates wa usa, uk na canada ndio wanaotoa mchango mkubwa katika kuandaa mikakati ya kimaendeleo ya kimataifa. Tusifanye mchezo na lugha jamani, hii lugha ya kulia ubwabwa hii haina nafasi kwa kweli duniani-tuache siasa
hasaa! Huo ndi ukweli wenyewe. Kwa kweli nashangaa sana hawa wanaong'ang'ania hii lugha ya kulia ubwabwa kwenye taaluma. Kiswahili tunakitumia katika maisha ya kila siku hapa nchini, naona hiyo yatosha. Kwenye taaluma naona ni bora tujichanganye na lugha inayotumika zaidi kwenye utandawazi ili wigo wa kupata information muhimu upanuke.
 
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Messages
1,625
Likes
75
Points
145
Age
44
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2013
1,625 75 145
By using foreign language your will always be a slave, we must not be brainwashed by foreign languages especially english!!! By woshipping english you are a condemned citizen
if you have not invented anything you are a slave per se, a consumer will always be a slave, to be free you need to have your own God, technology, and education in your own terms. Hizo hasira zako ni sawa na kupigana na giza badala ya kuwasha taa, amka brother.
 
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Messages
1,625
Likes
75
Points
145
Age
44
MBWA WA MANZESE

MBWA WA MANZESE

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2013
1,625 75 145
Hivi kumbe kiingereza ni lugha ya maana kuliko kiswahili? Umenifumbua macho, na pia nakushauri Siku nyingine uchangie mada zako kwa kiingereza utakuwa umemaanisha na unachokinena la sivyo.....?
ni kweli kiswahili hakina thamani kama kiingereza, kiswahili ni lugha ya kulia ubwabwa hafiti kwenye elimu huo ndio ukweli.
 
Nyikanavome

Nyikanavome

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
451
Likes
45
Points
45
Nyikanavome

Nyikanavome

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
451 45 45
Mjadala wa elimu ya kufundishia ni muhimu uendelee na kila mtu atoe maoni yake bila kushutumu mwenzie bali hoja zitawale.
Lugha ni nyenzo ya kupatia ujuzi na Ujuzi ndio utaotuwezesha kushindana na si lugha. Ukiwa na ujuzi mzuri utaweza kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ubora ambazo zitafanya washindani wako wakutafute hata ikibidi kwa kujifunza lugha yako.
Kwa maoni yangu taifa letu kwa sasa linahitaji watu wenye ujuzi mkubwa wa uzalishaji ambao pia utaweza kuvutia wawekezaji kuwekeza huku kwa sababu kuna hazina ya watu wenye ujuzi mbalimbali. Hii tabia ya kuchukulia kuwa mtu anaeporomsha kimombo ndio mwenye ujuzi inatupeka kubaya. Ulaya na marekani wanapeleka baadhi ya shughuli za uzalishaji huko uchina, thailand, Vietnam na kadhalika, sio kwa sababu watu wa huko wanajua kuporomosha kimombo bali wana ujuzi wa kuzalisha bidhaa nzuri tena kwa bei nafuu.
Kuhusu mfumo wetu, mie napekendekeza turuhusu lugha zote mbili zitumike kwa pamoja hadi chuo kikuu. Mtu aweze kusoma kutoka chekechea hadi chuo kikuu kwa Kiswahili na pia kwa kiingeraza kama akitaka
Mtu akishapata ujuzi wake kwa Kiswahili atajifunza lugha nyingine kutokana na mahitaji yake. Ukitaka kufanya kazi uchina utajifunza kichina, ukitakta kufanya kazi udachi utajifunza kidachi nakadhalika
JAMBO LA MSINGI NI KUWA UKIJIFUNZA KWA LUGHA UNAYOIJUA VIZURI UNAPATA UJUZI KWA URAHISI ZAIDI, NA UJUZI NDIO KITU CHA MUHUMU KULIKO LUGHA.
 
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
1,189
Likes
3
Points
0
Zinedine

Zinedine

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
1,189 3 0
Ulaya na marekani wanapeleka baadhi ya shughuli za uzalishaji huko uchina, mie napekendekeza turuhusu lugha zote mbili zitumike kwa pamoja hadi chuo kikuu. Mtu aweze kusoma kutoka chekechea hadi chuo kikuu kwa Kiswahili na pia kwa kiingeraza kama akitaka

JAMBO LA MSINGI NI KUWA UKIJIFUNZA KWA LUGHA UNAYOIJUA VIZURI UNAPATA UJUZI KWA URAHISI ZAIDI, NA UJUZI NDIO KITU CHA MUHUMU KULIKO LUGHA.
Ningeomba mnapojadili yanayotupasa kufanya kama Tanzania tusijifananishe na China kwa lolote lile. Kuna vigezo 'unique' ambavyo china vinaifanya kuwa nchi ya kipekee duniani. Idadi ya watu 1.3bilion kuzungumza kichina si suala la kujifananisha. Wakati sisi tunazungumzia umeme wa MW2000 China wanazungumzia umeme wa MW500,000???. Narudia tena, hakuna nchi yoyote Afrika ambayo inatumia lugha yake ya asili katika kufundishia elimu ya juu. Botswana na Mauritius ndizo nchi zinazojulikana Afrika kwamba zimepiga hatua kubwa sana kiuchumi lakini hawatumii kitswana katika elimu yao. Ilifaa tuwe na mfumo wa elimu ya kiswahili palepale 1961 sio leo 2013 ni tutaongeza changamoto zaidi za kukabiliana na mfumo wa maisha ya sasa ulimwenguni. Nimeeleza kwenye post yangu huko juu, china pamoja na kutumia lugha yao katika elimu ya juu, lakini ndio nchi ambayo ina idadi kubwa sana ya wanafunzi wanaojifunza elimu ya juu katika lugha ya kiingereza katika vyuo mbalimbali kote duniani(US, UK, Australia, Korea, Canada, Germany), ikiwa ni mkakati wa serikali wa kuiafanya "china for global take over" na pia wenyewe kujilipia. Kwa sababu china inajua kwamba ili kuweza kushindana duniani, kiingereza ni lazima na kichina ni kwa ajili ya 'kulinda' teknolojia na utamaduni wao. Sisi hatuna teknolojia wala utamuduni wa kulinda kwa kutumia lugha. Kazi ya lugha kwetu na Afrika kwa ujumla ni kuwasiliana tu. Hivyo tunaweza hata kuamua kisukuma kiwe lugha yetu, lakini je itatusaidaje kushindana? Ndio utabaini kuwa kwa kuwa kazi ya lugha kwetu ni mawasiliano tu ni vema tuchague kiingereza ambacho kikaribu zaidi ya kuwezesha kutumia fursa mbalimbli za maendeleo ya dunia ya leo. Hili halihitaji siasa, hususan kwa waliotembea kidogo tu nje ya nchi. Hapo kwenye red nadhani ni vema lakini kutakuwa na gharama kubwa, badala yake Kiswahili kibaki kwenye specialization tu.
 
Mwamgunda

Mwamgunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
247
Likes
2
Points
35
Age
31
Mwamgunda

Mwamgunda

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
247 2 35
Nyie mnajua sana kiswahili? Sasa nichanganulieni sentensi hii kwa njia ya matawi: Katika nchi ya mbali chongo ndiye raisi wao mpya!
 

Forum statistics

Threads 1,274,855
Members 490,833
Posts 30,526,000