Mbunge ataka kiswahili kitumika hadi vyuo vikuu

wanasema kiswahili kitumike wakat watoto wao wanasoma international na nje ya nchi. mshtuke nyie. amken

huyo wazr awe mfano wa kusomesha watoto wake shule za kiswahili.mbna watoto wao wote wanasoma english medium,tena inawezekana hata budget za bakita znaandaliwa ktwa kiingereza,pia makampun meng bongo ni ya kigeni na mabos wanataka ripot kwa kiingereza.KISWAHllI KITUMIKE KAMA LUGHA YA MAZUNGUMZO TU SI KATIKA MITAALA YA CHUO KIKUU.
 
if you have not invented anything you are a slave per se, a consumer will always be a slave, to be free you need to have your own God, technology, and education in your own terms. Hizo hasira zako ni sawa na kupigana na giza badala ya kuwasha taa, amka brother.

Ni mtizamo tu, sishangai kwakuwa hata njiwa Ana Makinda lakini sio spika
 
Nashauri lugha ya kufundishia iwe Kiingereza toka shule za awali mpaka chuo kikuu ILA kiswahili iwe ni somo la lazima au kipindi cha lazima toka chekechea mpaka chuo kikuu na kiwe na adhabu kali kwa atakayedharau!
 
Nashauri lugha ya kufundishia iwe Kiingereza toka shule za awali mpaka chuo kikuu ILA kiswahili iwe ni somo la lazima au kipindi cha lazima toka chekechea mpaka chuo kikuu na kiwe na adhabu kali kwa atakayedharau!
Nimependa sana maoni haya; yaani kama yalivyo full stop
 
Unajua kumbe watu wengi wana upungufu wa akili.
Kiswahili kitumike mpaka zaidi ya vyuo vikuu ila kingereza kiwe somo na kifundishwe vizuri ili watu wakijue tu kwa dhima ya mawasiliano.
 
Mkuu, kukutukana sintoweza na haitatokea. Lakini! kwani lugha hasa ni nini? unadhani kuna tofauti gani ya anaeomba maji kwa kisukuma, kiingereza, kiswahili na kichina? Binafsi sina tatizo na kiswahili kama lugha, nina tatizo na kiswahili kama lugha ya nyenzo(tool) katika dunia tulionayo sasa, wazo hili lilifaa lifanyike immediately baada ya uhuru lakini si kwa sasa. Dunia kwa sasa haitoi tena nafasi ya nchi mpya kufanya "invention" bali kutafuta namna ya kufanya adaptation, imitation na innovation, hivyo nafasi ya kiswahili kama nyenzo ya kuweza kuhimili changamoto za utandawazi ni kujidanganya kitu ambacho mimi siwezi. Suala lingine, kama tunaamini Kiswahili ni bora kwa wakati huu, kwanini hao watetezi watoto wao wote wako English medium? wanafanya nini huko? kwanini wasiwapeleke "Shule za kisasa za kimataifa za kiswahili"? Nini tatizo? Naelewa vema, hata hapa Australia hawa wenyeji wana lugha yao lakini Lugha ya kufundishia ni Kiingereza ambacho kimetokana na asili ya ukoloni wao wa kiingereza, mbona maendeleo yapo? Naelewa sana nchi nyingi zilizoendelea zinatumia Lugha zao lakini nchi ZOTE zilizotawaliwa zinatumia Lugha za watawala wao( Amerika kusini yote, Marekani yenyewe, Australia, India, na nikakutolea mfano wa Afrika hakuna nchi yoyote inayotumia Lugha yake ya asili kufundishia, huu uspeciality wa Tanzania unatoka wapi? Ni nini kinachowanya nyie watu muwe special? Kwani kuondoa matatizo ya umaskini kunahitaji Lugha maalum tu? No! Ila tukubali kiingereza kiko karibu zaidi katika kutatua na kuishirikisha nchi katika kukabiliana na changamoto za dunia ya leo. Too late kufikiria lugha ya kufundishia leo kwa sababu nimekupa na mifano ya nchi hizo za Japan, Korea na China ambazo nimeishi na pamoja na kutumia lugha zao lakini zina idadi kubwa ya watu wao wanaowapeleka kusoma katika Shule za Marekani, Ulaya Canada na hapa Australia kwa pesa zao ambazo nyie watanzania hamna mnategemea udhamini wao ambao wanawataka muweze kujua kiingereza. Vilevile katika hizo nchi za huko Asia, kuna juhudi kubwa sana za kuimarisha mitaala yao ya elimu kuwawezesha kujua kiingereza na haishangazi vijana wengi wanaomaliza shule zao katika nchi hizo wanaongea kiingereza. Elimu ndiyo nyenzo kuu siku hizi ambayo imerahisishwa kupitia vyombo mbalimbali ikiwemo mawasilino ya Internet. Hebu niambie material gani ya msingi na muhimu yaliyoandikwa kwa kiswahili utakayoweza kuyapata kupitia Google? Na ni mkakati gani wa Serikali utakaowezesha ku-upload kiswahili materials ili vijana wetu wa kitanzania waende sambamba na kile kinachojadiliwa duniani? Ni wasomi gani hao tulionao wanaoweza kufanya kazi hiyo? Au wale wanaopiga kelele pale Radio One siku za Jumamosi? Umewahi kukutana na ile kamusi ya Kiswahili/Kiingereza ya TUKI, na hiyo kashfa ya juzi ya upotoshaji wa vitabu vya shule za msingi huko Tanzania unaichukuliaje? Tuacheni blabla ambazo zinatuchelewesha siku zote, tujadilini vitu vikubwa na tuache kujifananisha na developed countries wewe unajua namna tulivyotofautiana kiuchumi.
Nakuunga mkono asilimia mia kwa mia, mkuu umenena. KIswahili kitatumika University kufundisha masomo au fani gani hapa Tanzania? Elimu au mfumo wa elimu tulio nao uliletwa na Wazungu na waliona ni vema kufundisha kwa lugha yao. Vitabu vingi vya maarifa na elimu hiyo ya kizungu vimeandikwa na Wazungu. Fikiria Kiswahili kufundisha mathalani mathematics topics kama vile, calculus, trigonometric, complex number, logarithm, Science topics kama vile Nuclear Science kwa kiswahili tunazo hizo terminology au ni kutafsiri maneno ambayo hata hayaeleweki kwa Kiswahili? Economics, Anthropology, Biology, environment, building and construction list inaendelea. tutapata wapi pesa na wataalam wa kutafsiri vitabu vya Kingereza ambavyo hutupa maarifa. Au tuseme Kiswahili kimedevelop theory kama zile za kina WEBER, MAX, ARISTOTLE, ISAAC NEWTON,ACHIRMEDES, EUCLID,ADAM SMITH, KEYNES na wazungu wengine wengi ambao uvumbuzi,maarifa na mawazo yao yanatawala na kuongoza jamii zote za dunia.
Kama tumepata Wavumbuzi wa Tz ambao wamekuja na mapya yatakayoeleweka kwa Kiswahili sawa. Ukiwasikiliza waTz Wegi wanaopinga English kama lugha ya kufundishia Tz wanasema eti hawaelewi wakifundishwa kwa English. Nawashangaa sana kwa sababu WaTz wote
waliotujengea nchi walifundishwa kwa kiingereza na wakaelewa. ndio sababu waliweza kujenga majengo imara yanayodumu hadi leo. wakaanzisha taasisi mbalimbali zinazotoa huduma hapa nchini kama vile mahakama, bunge, hospital, shule, vyuo, posta, wizara, mashirika ya umma na kadhalika. Tutafute njia sahihi za Kufundisha Kiingereza ili kieleweke kama walivyofanya wenzetu wa nchi jirani Kenya, Uganda, Malawi na Zambia. Wana Lugha zao za asili wanazotumia kuwasiliana lakini hawakutupa Kiingereza na wanafanya vizuri katika nyanja mbalimbali nje na ndani ya nchi zao. Kiswahili kama lugha ya Mawasiliano katika jamii yetu hamna ubaya ila tusijidai kubomoa misingi ya Elimu za Kimataifa ambayo sisi siyo waanzilishi.
Kutokuelewa Kiingereza kwa Watz shuleni na vyuoni hunishangaza kwa kuwa kuna wanafunzi wanamaliza form six wanapata ufadhili
Urusi na Uchina. wanasoma masomo yote kwa Kirusi na Kichina wanaelewa na wanapata shahada safi tu na wamerudi hapa kwetu ni wataalamu kama vile Doctors, kilimo, maji, waalimu, vertinary doctors, meteorologists, environmentalists, wahasibu
etc. Hao imekuwaje wakaelewa lugha za Kigeni tena ukubwani? WaTZ tuache uvivu tujibishe kusoma na kubadilika.
 
Nawashangaa sana watu wanaolazimisha kiswahili kitumike vyuoni..! Hii lugha inakosa misamiati technical mingi sana hasa kwenye ulimwengu wa sayansi.., mtasubiri sana.
 
Back
Top Bottom