Mbunge Asumpta Mshana na Mary Mwanjelwa hawajui msimamo wa serikali ya Israel

Wote wawili nasikia wanajiita walokole! Kama sikosei tumeisha rudisha mahusiano ya kibalozi. Balozi wa Israel Kenya ndiye anawakilisha nchi yake hapa Tanzania.

Back from ban. wadau huyo mlokole anaeitwa doc mwanjelwa ndo yule aliyeiba mashuka ya gesti kule arusha au mwingine?
 
Shardcole, sina hakika ulikusudia kunijibu lakini ukahafilika au hukunielewa nilichouliza. Labda nifafanue zaidi, Mbunge anaposema serikali ifanye jambo kwa sababu limeandikwa kwenye kitabu cha dini anayofuata mbunge ni sahihi? Hasa kwa Tanzania ambayo tunasema serikali haina dini?

Assumpta Mshana ana-argue kwamba Tanzania kutokuwa na ubalozi wa marekani ni kinyume na maandiko ya biblia, na hivyo tutapata laana! Sasa nikuulize bunge linaendeshwa kwa biblia? au kitabu kingine cha dini? Sababu zilizopelekea Tanzania kuvunja mahusiano yake na Israel huko nyuma anazifahamu mbunge? Na kama hazifahamu, inatupa picha gani sisi wananchi wa kawaida kuhusu watunga sheria wetu (wabunge) kutojua sera za za nchi? Watangiaje maboresho ya sheria kama hata historia ya nchi inawapiga chenga?

Kwenye red: Nimeuliza ulokole wake unaanzia wapi na unashia wapi? Do you know?

Tusiwe wabaguzi bila sababu..kuomba haki zilizopo katika biblia sio ndio kuliendesha bunge.Hivi mahakama ya kadhi si ni mambo ya kwenye vitabu vya dini na inaongelewa bungeni?Anyway Mungu awabariki wakristo wa Tanzania maana ni watulivu mno na wana busara za ajabu.
 
2.1% Cristian alafu watu wanaongelea mahusiano ya nchi ya Israel na Tanzania kwa Udini? Jamani muda wakufikiri nje ya kapu la mawazo finyu umefika. Yako mambo zaidi ya Udini kwa mustakabali wa Tanzania.

Kama Israel wakristo ni wachache hivyo na bado Wakristo wa Tanzania wanadai mahusiano mema basi ni ushahidi kuwa kuibariki Israel si suala la kidini (la Kikristo) ni kanuni ambayo imeonekana ikitenda kazi kwa wengi. Ndio maana Misri na nchi kadhaa za Kiislam ambazo zinaijua kanuni hiyo zina mahusiano mazuri na Israel licha ya maonevu ambayo wengi wanadai Israel inafanya. Mara nyingi humu JF watu wamekuwa wakijiuliza hivi sisi Tanzania tumerogwa na nani mbona mambo yetu hayaendi? Wengine hujibu kuwa mchawi aliyeturoga alikufa hivyo hatuna namna ya kutoka. Si kweli. Tumejiroga wenyewe na ukijiroga mwenyewe nani atakuponya?
Kwa wale wanaoamini kuwa Mungu yupo (na hasa Yeye aliyeteua Israel kuwa taifa lake - "Mzaliwa wangu wa kwanza") basi ndiye aliyeagiza wakati akianza agano na Ibrahim kwamba "atakayekubariki nitam-bariki na atakaye kulaani nitamlaani". Yaani ni automatic! Sisi Tanzania tumetoa matamko mengi sana ya kuilaani Israel na zawadi yetu tunaipata. Matokeo yake nasi tumelaaniwa au kwa usahihi zaidi tumejilaani. Maana ukiambiwa kwamba ukijifyatulia risasi utakufa halafu wewe unajifyatulia - kufa lazima ufe, na utakuwa umejiua mwenyewe. Kwa kuilaani Israel tunajilaani wenyewe. haina mjadala! Hebu niambie ni nchi gani duniani yenye madini ya Tanzanite? Nani muuzaji mkubwa wa madini hayo duniani? Ni wapi tena kwenye hali kama hiyo duniani kama si kwenye nchi zenye mahusiano mabaya na Israel? Dadisi uone!
Ugomvi wa Israel na Wapalestina ni wa kifamilia (kugombea ardhi ambayo haki alipewa Isaka na Ismail akanyimwa) wala si ugomvi wa kidini, na mambo ya kifamilia ukiingilia mtu mwingine (TZ) shauri yako. Mahusiano yetu hayapaswi kuhusishwa na ugomvi huu wa kifamilia. Vilevile kuna watu ambao wanadai kuwa ingekuwa taifa teule lisingefanya linavyofanya. Mnakosea. Mungu hakuichagua Israel kwa ajili ya utakatifu wake bali kwa sababu alikuwa na haki ya kuchagua taifa lolote lile kuwa teule na akaamua taifa hilo liwe Israel. Ndiyo maana haliitwi taifa Takatifu bali Teule. Kuna wanaotishwa na mikasa kama Katrina kuonyesha kuwa si baraka (kwa Marekani). Kwanza fikiria kama Katrina lile lingetupata Tanzania ingekuwaje? Bila shaka tungefutika kabisa katika uso wa dunia. Wamemudu Wamarekani (wenye uhusiano mwema na Israel) kwa sababu kweli wamebarikiwa. Pili kubarikiwa hakukuondolei majaribu na hata hukumu dhidi ya kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Wewe mwanao unayempenda sana na ambaye umem-bariki kwa mema mengi akikukosea, unamwadhibu sio? Na Mungu je hana haki hiyo?
 
Hao ndio wabunge wa CCM! Kwa umri naamini walisoma kabla shule za kata hazijaanza, sasa tatizo ni nini? Wamepoteza kumbukumbu? Membe una kazi, aanzisha evening class Dodoma ili tuondokane na hii aibu.

Chukua 7 mkuu hili neno zito sana .Hao ndiyo ma CCM
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Haya bana.

Na hao JEWISH yani wanamisimamo ya hatari sana wanafuga madevu kuliko ata OSAMA wanawatenga wanawake na miezi miwili iliyopita walikua wanagawa vipondo kwa wanawake wanaovaa vibaya na wao wanawabagua ata wakristo na ndo wanaojiona wapo karibu na YESU na ata hao viongozi wa ISRAEL majority ni jewish so tusishabikie tusijokijua kwa Taifa la ISRAEL ni zaidi ya ulijuavyo mwezi ulioisha walikua wanawapiga mawe RAIA WENYE ASILI YA AFRICA na kuwajerui,kuwapasulia vioo vya magari na nk....INSHORT WITHOUT US SUPPORT NO JEWISH STATE...Na by the way ISRAEL inajengwa kwa kodi za WAMAREKANI so hawana maendeleo yakutufanya tubabaike kwao na isitoshe waziri wao wa ulinzi kasha alizotoa juu ya TANZANIA bado tunazikumbuka ila kuna MTZ mmoja alimjibu na kucompare achievement za TANZANIA dhidi ya ISRAEL yani tunawazidi mbali ukuangalia misaada wanayopewa then uangalie na maendeleo waliyonayo ni ***** tu...sisi tupu 40 milion, Israel only 7 milion.......so hawana jipya
 
Kama Israel wakristo ni wachache hivyo na bado Wakristo wa Tanzania wanadai mahusiano mema basi ni ushahidi kuwa kuibariki Israel si suala la kidini (la Kikristo) ni kanuni ambayo imeonekana ikitenda kazi kwa wengi. Ndio maana Misri na nchi kadhaa za Kiislam ambazo zinaijua kanuni hiyo zina mahusiano mazuri na Israel licha ya maonevu ambayo wengi wanadai Israel inafanya. Mara nyingi humu JF watu wamekuwa wakijiuliza hivi sisi Tanzania tumerogwa na nani mbona mambo yetu hayaendi? Wengine hujibu kuwa mchawi aliyeturoga alikufa hivyo hatuna namna ya kutoka. Si kweli. Tumejiroga wenyewe na ukijiroga mwenyewe nani atakuponya?
Kwa wale wanaoamini kuwa Mungu yupo (na hasa Yeye aliyeteua Israel kuwa taifa lake - "Mzaliwa wangu wa kwanza") basi ndiye aliyeagiza wakati akianza agano na Ibrahim kwamba "atakayekubariki nitam-bariki na atakaye kulaani nitamlaani". Yaani ni automatic! Sisi Tanzania tumetoa matamko mengi sana ya kuilaani Israel na zawadi yetu tunaipata. Matokeo yake nasi tumelaaniwa au kwa usahihi zaidi tumejilaani. Maana ukiambiwa kwamba ukijifyatulia risasi utakufa halafu wewe unajifyatulia - kufa lazima ufe, na utakuwa umejiua mwenyewe. Kwa kuilaani Israel tunajilaani wenyewe. haina mjadala! Hebu niambie ni nchi gani duniani yenye madini ya Tanzanite? Nani muuzaji mkubwa wa madini hayo duniani? Ni wapi tena kwenye hali kama hiyo duniani kama si kwenye nchi zenye mahusiano mabaya na Israel? Dadisi uone!
Ugomvi wa Israel na Wapalestina ni wa kifamilia (kugombea ardhi ambayo haki alipewa Isaka na Ismail akanyimwa) wala si ugomvi wa kidini, na mambo ya kifamilia ukiingilia mtu mwingine (TZ) shauri yako. Mahusiano yetu hayapaswi kuhusishwa na ugomvi huu wa kifamilia. Vilevile kuna watu ambao wanadai kuwa ingekuwa taifa teule lisingefanya linavyofanya. Mnakosea. Mungu hakuichagua Israel kwa ajili ya utakatifu wake bali kwa sababu alikuwa na haki ya kuchagua taifa lolote lile kuwa teule na akaamua taifa hilo liwe Israel. Ndiyo maana haliitwi taifa Takatifu bali Teule. Kuna wanaotishwa na mikasa kama Katrina kuonyesha kuwa si baraka (kwa Marekani). Kwanza fikiria kama Katrina lile lingetupata Tanzania ingekuwaje? Bila shaka tungefutika kabisa katika uso wa dunia. Wamemudu Wamarekani (wenye uhusiano mwema na Israel) kwa sababu kweli wamebarikiwa. Pili kubarikiwa hakukuondolei majaribu na hata hukumu dhidi ya kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Wewe mwanao unayempenda sana na ambaye umem-bariki kwa mema mengi akikukosea, unamwadhibu sio? Na Mungu je hana haki hiyo?

DM naamini kabisa katika haya maandiko uliyoandika. Nilitaka kubainisha tu mahusiano kwa taifa hili teule ni zaidi ya Udini. Mungu ndiye aliyelichagua hili taifa, na Mungu huyo hana dini maana dini ni za wanadamu. Kwa uamini wangu hili ni Taifa teule.
 
naomba tuheshimiane humu kwa imani zetu, unapouponda ulokole ukidhani unamponda Marry mwanjelwa ujue kwamba ni wengi unatuboa, pia elewa kuwa Marry kasema kwa maoni yake basi na ww utoe yako na sio kuattack mawazo ya mtu.

Big up!!!!!!!!!!
 
Na hao JEWISH yani wanamisimamo ya hatari sana wanafuga madevu kuliko ata OSAMA wanawatenga wanawake na miezi miwili iliyopita walikua wanagawa vipondo kwa wanawake wanaovaa vibaya na wao wanawabagua ata wakristo na ndo wanaojiona wapo karibu na YESU na ata hao viongozi wa ISRAEL majority ni jewish so tusishabikie tusijokijua kwa Taifa la ISRAEL ni zaidi ya ulijuavyo mwezi ulioisha walikua wanawapiga mawe RAIA WENYE ASILI YA AFRICA na kuwajerui,kuwapasulia vioo vya magari na nk....INSHORT WITHOUT US SUPPORT NO JEWISH STATE...Na by the way ISRAEL inajengwa kwa kodi za WAMAREKANI so hawana maendeleo yakutufanya tubabaike kwao na isitoshe waziri wao wa ulinzi kasha alizotoa juu ya TANZANIA bado tunazikumbuka ila kuna MTZ mmoja alimjibu na kucompare achievement za TANZANIA dhidi ya ISRAEL yani tunawazidi mbali ukuangalia misaada wanayopewa then uangalie na maendeleo waliyonayo ni ***** tu...sisi tupu 40 milion, Israel only 7 milion.......so hawana jipya
BN,
Usitoke povu bila kufanya tafiti ndugu, Hawa watu wanahistoria ndefu hata kukumbatiwa kwao na Marekani hakukupi maswali? Usipotoshe jamii na fikra zako, Taifa la watu Mil 7 wote wanajuana kokote walipo ulimwenguni na wote wanalipa kodi kwa serikali yao hata kama wako taifa jingine nje ya Israel.
 
:israel::israel::israel::israel::israel: Taifa teule! Hata Mwalimu alilijua hili, ila akalifumbia macho.! matokeo yake tunayaona sasa.
 
Ebu sikia wewe Gezaulole kwani walokeole si watu? Tena sasa tunataka sensa ya watu na makazi iwe na kipengele cha kuonyesha hapa Tanzania walokole tuko wangapi na wako wapi ili nasi tuweze kutetea maslahi yetu. Hao wabunge wametusemea sisi. Kama wewe unaona si point ni kwa vile huna maslahi nayo. walokole tuna maslahi yetu na Israel tena kwa sana. Tunataka Tanzania ifungue huko ubalozi haraka.

mkuu hapo umenena kwani wapagani wa nchi hii bado hawajajua kwamba israel ni taifa gani kwa kupuuza maandiko mtakatifu yenye pumzi ya Mungu.
 
Member of Parliament CV

GENERAL
Salutation
Honourable
First Name:
Assumpter
Middle Name:
Nshunju
Last Name:
Mshama
Member Type:
Constituency Member
Constituent:
Nkenge
Political Party:
CCM
Office Location:
Box 64, Kyaka. 21494, Dar Es Salaam
Office Phone:
+255 783 852736/+255 752 131913
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail:
amshama@parliament.go.tz
Member Status:
Current Member
Date of Birth

Hiyo hapo juu ndo CV ya Mbunge wetu Asupmter

tunaomba malizia na kazi na uzoefu alionao kisiasa
 
Kwa uzoefu wangu, wayahudi wanaongoza kwa ubaguzi. Na si kwa waislamu tu. Hawa jamaa ni wabaguzi sana. Fuatilia news uone hatua wanazochukua kukabiliana na wahamiaji kutoka Africa. Sina taarifa kuhusu nchi nyingine yeyote yenye sera mbaya namna hiyo kwa wahamiaji. Nikifuatilia mwenendo ya Taifa hili na watu wake, nina mashaka kuwa hili ni taifa teule. Na kwamba eti, tusipokuwa na mahusiano ya kibalozi na nchi hii tutalaaniwa. This is utterly nonsense at best. Mahusiano na taifa lolote lile hapa duniani hayapaswi kuwa kwa misingi ya kidini. Ni makosa makubwa kufanya hivyo. Hata ukizingatia dini, Wayahudi si waisilamu wala wakristo. And remember, religions are evil. You just look at the evidences.

You hit the top of the nail!! Hakuna uhusiano kati ya kufanikiwa/kufeli kwetu na baraka/laana ya Israel. Ni kweli kuwa kuna ubaguzi sana wa wahamiaji lakini katika uhalisia mtu anaweza akaelewa kwanini ni lazima wafanye hivo:
a) Majirani zao wote isipokuwa Jordan, hawana border crossings. Hivo ni uhasama full!!
b) Uyahudi ni kitu cha kuzaliwa nacho, hakuna conversion!! Mila za kiyahudi ni ngumu sana, wageni hawaziwezi na wayahudi hawavumilii zivunjwe katika nchi yao. Hili ni sawa na jinsi ilivo ngumu kuvunja mila za kiislamu Saudi Arabia.
c) Wageni wameonesha kufanya espionage kwa mataifa maadui, au kwa kudhaniwa au kwa ukweli. Kama unatoka taifa rafiki na Palestina hutaweza kuingia Israel. Na kama umewahi kuingia Israel, hutaweza kuingia nchi yoyote ya kiarabu kwa urahisi. Hizi si habari za utani.

Ndio kiasi cha uhasama kilivyo!!
 
Hawa wabunge wameuliza jambo la msingi sana ambalo serikali yoyote makini ilipaswa kuwa imelifanya juzi na zio jana. Maandiko matakatifu katika biblia yako wazi kuhusu kubarikiwa wale wanaibariki Israel kama taifa teule la Mungu. Na anayechaguaa ukilaani Israeli anachagua laana badala ya baraka. KWA HIYO< TANZANIA KUTOKUWA NA UHUSIANO WA KIBALOZI KAMA ILIVYOKUWA HUKO NYUMA AUTOMATICALLY IMECHAGUA LAANA. Jambo lolote laweza kutanguka lakini chochote kilichotajwa kwenye biblia lazima kitatimia tu.

Chukua mfano wa Marekani anabarikiwa kwa sababu ya kuwa na uhusiano mzuri na Israel na kuitetea Israel. Au tuangalia jirani zetu Kenya moja ya chanzo cha mambo yao kwenda vizuri ni kutokana na wao kuwa na uhusiano mzuri na Israel. Hebu angalia Tanzania pamoja na kuwa na rasilimali nyingi kuliko Kenya kwa mbali, Tanzania bado iko hoi sana. Wenzetu mpaka wamegundua mafuta sisi bado tupo tunapiga mark time. Kumbuka hili ni suala la kiroho zaidi ambalo taathira zake kwenye uchumi na maisha jumla ya kimwili ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

MIMI NASEMA UBALOZI WA ISRAEL NCHINI TANZANIA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ISRAEL ULITAKIWA KUWA UMEFUNGULIWA JUZI NA SIO JANA. Tanzania una nafasi ya kuchagua laana au BARAKA.

Mkulu

Israel ni jina la Abraham...wana wa Israel, maana yake nyingine ni wana wa Abraham...

Sasa tujiulize wana wa Abraham ni akina nani?

Somo hili ni kubwa na pana sana ndugu yangu kuliko unavyotaka kuwaaminisha baadhi ya members humu.

MPAKA HAPA TULIPOFIKA KAMA TAIFA...KAMA KUNA LAANA....BASI NI KUMTELEKEZA DOSA AZIZ PALE MLANDIZI AKIUGUZA MARADHI YAKE PALE TUMBI HOSPITALI ....LIKE HE WAS NOBODY....

SIYO KUTOFUNGUA UBALOZI TEL AVIV...

TAFAKARI
 
Lakini ni kweli,asiyeheshimu israel atalaaniwa na hii ni kutokana na biblia.Labda waislam watuambie quorani inasema nini kuhusu israel.
Swali lako lipo kiujumla mno, ila ngoja nikudokezee kidogo halafu unaweza kuuliza kama ukipenda.
Bani Israel (watoto wa Israel) ni watoto wa mtume Yaaqub (Jacob) mmoja wa mitume wa Kiislamu hawa waliishi sehemu za mashariki ya kati na kuna kila dalili kuwa Wapalestina wametokana na asili ya watoto wa Israel.Pia kuna katika Wapalestina ambao walikuwa katika dini za Kiyahudi na Kikristo halafu baada ya kuja nabii wa mwisho Muhammad (SAW) wakaendelea kumfuata na kuwa ni Waislamu kama hivi tunavyowaona wengi wao sasa.
Bali mitume wa Kiislamu kama Issa (Jesus), Muusa (Moses) na wengineo walitoka katika kizazi cha Bani Israel hii ndio maana ninakuambia kuwa swali lako ni la kiujumla.
Hivyo ukiangalia matamko na historia utakuja kugundua kuwa wengi wa Waisrael wa sasa hivi walioko katika nchi inayoitwa Isreal si kutoka katika vizazi vya Wana wa Israel bali ni vizazi vya Khazar watu kutoka Ulaya ya Mashariki. Sasa sielewi hao wabunge wakisema kuwa atabarkiwa anayeibarki Israel wanamaanisha "Waisrael" Khazar ambao wameikalia ile ardhi au wanamaanisha Sphoridic Jews ambao wana asili ya Kiarabu pamoja na Wapalestina.....Kimtazamo wangu sidhani kama ilikuwa ni busara kwa hawa wabunge kujiingiza katika hili suala ambalo nina hakika wakija sehemu kama hapa JF kutawafanya waonekana ni vichekesho!
 
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya wiki mbili zilizopita Balozi wa Israel Tanzania alikuja Dar kujitambulisha na kwa taarifa balozi wa Israel nchini ndiye pia anawakilisha Tanzania na anakaa Nairobi. Sisi watanzania tunadandia lifti ya wakenya badala ya kuwa na Ubalozi wetu kamili pale Jerusalemu na wao wawe na ubalozi wao kamili hapa Dar. Tatizo la nchi yetu tunarithi hata vitu ambavyo sio vya msingi, kama Mwl. Nyerere alivunja uhusiano wetu na Israel ina maana kuwa Rais mwingine akija ni mpaka afuate yale yale tu??? Hatuna uwezo wa kuamua mambo yetu wenyewe kama sisi ni mpaka tuangalie tu the past things ambavyo havina mashiko, Mwl alikosea kabisa kuharibu mahusiano na Taifa teule la Israel na cha kushangaza akaanzisha uhusiano na taifa la Palestina very wrong, ndio maana Tanzania tuko hapa directly tunapata laana according to the scriptures. Kwa hivyo hawa Wabunge wako sahihi na niko nyuma yao kwa 150%

Na hakuna namna Tanzania tunaweza kujitoa katika laana hii kwa kisingizio cha kudandia kutoka kwa Kenya,
kama tunataka kujitoa katika laana hii ni kuwa na ubalozi wa Israel Tanzania na Tanzani kuwa na ubalozi nchini Israel
.
 
Watanzania pamoja na Rais alishasema,hajui kwa nini Tanzania ni maskini,jibu ni hili iko
chini ya laana kwa sababu ya kutokuwa na ubalozi wa Israel.
 
Mkulu

Israel ni jina la Abraham...wana wa Israel, maana yake nyingine ni wana wa Abraham...

...

Mkuu mimi sio mtaalamu wa maandiko lakini hapo kwenye red umepotoka kidogo. Israel ni jina jingine la Yakobo (James) ndugu yake Essau. Ni mtoto wa pili wa "kuzaliwa" lakini wa KWANZA kwa HAKI kwa Isaka na mkewe Rebecca. Kwa maana hiyo, ni mjukuu wa Ibrahim au Abramu yule Baba wa Imani na mkewe Sarai au Sara yule mama wa WANA WA AHADI.

Kwa wasifu huu mfupi, Israel ana(ina)tengwa kabisa na wale wana wa zinaa waliopatikana kutoka kwa yule kijakazi. Hii ni very sensitive issue mzee, usikurupuke au kuchanganya mambo hapo; utamnufaisha Shetaji na matokeo yake ni dhahiri.
 
enzi za juchagua marafiki kwa maslahi ya kisiasa ulishapita, kwa nini tunatangaza diplomasia ya kiuchumi kwa maneno tuu? Yapo mengi tunaweza faidika kiuchumi kutoka israel hasa kupitia kilimo na utalii..

Kwa taarifa yako, mahusiano ya kisiasa ndiyo ingredient muhimu katika kufungua na kuendesha ubalozi. Sasa kama huielewi diplomasia ya uchumi na inakoanzia then ni vizuri ukaomba kuelimishwa.
 
Tanzania kuvunja ubalozi na Israel sio kwasababu nyingine zaidi ya uonevu unaofanywa na Israel la kutaka na bado inaendelea kuiondoa Taifa la ki PALESTINA fatlikia kinachoendelea uko utashangaa km kweli Taifa linalojiona teule linaweza kufanya hivyo...Swala sio udini kwani ata Israel penyewe ukristu ni kiduchu sana.....Try to read the following data below:
Religion affiliation of Israel population as of 2011 was
:
  1. 75.5% Jewish
  2. 16.7% Muslim
  3. 2.1% Cristian
  4. 1.7% Druze

These flattering statistics are a kick in the teeth of these two hopeless lawmakers. Kwa ufinyu wao walidhani kwamba kwa sababu tu kwamba kuna maeneo matakatifu na uhusiano wa Israel na ukristo basi nchi ile ni ya kikristo. Forgetting kwamba Jews ndiyo walimuua Yesu.
 
Back
Top Bottom