Mbunge Asumpta Mshana na Mary Mwanjelwa hawajui msimamo wa serikali ya Israel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbunge Asumpta Mshana na Mary Mwanjelwa hawajui msimamo wa serikali ya Israel

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kikulacho, Jul 10, 2012.

 1. K

  Kikulacho Member

  #1
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Leo katika kipinsi cha maswali na majibu Mbunge wa Nkenge Asumpta Mshama na Mery Mwanjelwa (CCM), wameitaka Serikali itoe Maelezo kwa nini haijafungua Ubalozi nchini Israel kwani kutofanya hivyo ni kuikosea biblia na Tanzania itapata laana.

  Kutokana na hali hiyo Wabunge hawa hawajajua msimamo wa Serikali ya Tanzania kwani inatambua kuwa Palestina ni Taifa huru na ndiyo maana nchi yetu katu haitafungua ubalozi katika nchi ya Israel na Lebanon kutokana na uonevu unaofanywa kwa chuki za kidini, hivyo hawa wabunge kuna kila chembe ya dalili ya kutumwa na makuadi wa Israel kwa kuwasemea kupitia Bunge.

  Ni vema wawe wanasoma kwanza wabunge wetu kabla ya kukupuka na hoja butu.
   
 2. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Usiseme uongo kuhusu Lebanon, tuna Consulate pale na Mzee Zakhem ni Desk Officer.

  Taarifa: Lebanon isiingizwe kwenye maelezo yako kama pro-Israel. Jua pia PLO iliundwa na kuwa na makao yake makuu ya kwanza kijijini Chebaa, kusini mwa Lebanon. Lebanon ina kundi la Hizbullah ambalo linakinzana na Israel na inavitunza vikundi vya kipalestina vinvokinzana na Israel nchini mwao. Mgogoro wa Israel na Palestina ni wa kijiographia (mipaka) na sio wa kidini. Nchi zote mbili zina wakristu na waislamu!!

  Msingi wa wabunge hawa kudai ubalozi unatoka na Biblia kuwa "Nchi ya Kanaan" ambayo sehemu yake ni Israel ya leo, ni taifa teule. Si kwa sababu wanataka kuonesha kuwa wanaipinga Palestina. Kwa taarifa tu, mataifa mengi ya magharibi yana balozi za Palestina hali kadhalika za Israel. Kwa sababu mamlaka ya Palestina kwa Ghaza na West Bank yanajulikana kimataifa!!
   
 3. T

  TrueVoter JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 868
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 80
  enzi za juchagua marafiki kwa maslahi ya kisiasa ulishapita, kwa nini tunatangaza diplomasia ya kiuchumi kwa maneno tuu? Yapo mengi tunaweza faidika kiuchumi kutoka israel hasa kupitia kilimo na utalii..
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hao ndio wabunge wa CCM! Kwa umri naamini walisoma kabla shule za kata hazijaanza, sasa tatizo ni nini? Wamepoteza kumbukumbu? Membe una kazi, aanzisha evening class Dodoma ili tuondokane na hii aibu.
   
 5. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nyerere alifunga UBALOZI wa Israel hapa Tanzania kuwafurahisha Waislamu ambao leo hii wanamuona eti alikuwa adui wao mkubwa.

  Matokeo ya kuwafukuza wa Israel Bugando Hospital Haikumalizika, Nkurumah Hall haikulimazika maana ilitakiwe iwe flyer ove bridge, mradi wa kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria to Dodoma hakufanyika, majuzi tu ndiyo EL ali struggle na kupeleka maji Kahama. Just Kahama hata Singida hayajafika.

  Ila hilo la kupata laana kutokana na kutofungua ubalozi wa Israel is a RELIGIOUS FANATISIM.

  BTW, nimesikia Wa israel wameanzisha mradi mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji maji Zanzibar. Labda ndiyo wanaanza kurudi taratibu.
   
 6. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Wote wawili nasikia wanajiita walokole! Kama sikosei tumeisha rudisha mahusiano ya kibalozi. Balozi wa Israel Kenya ndiye anawakilisha nchi yake hapa Tanzania.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pia wapo Dodoma, wana kama eka laki moja hivi chini ya Kilimo kwanza na Bwana Dustan Mrutu. Kama utakumbuka rais alitembelea hilo shamba mwezi uliopita, wanalima mboga mboga na wanasema in 3-4 years time Tanzania (maybe kupita kwao) itakuwa ina export kwa E/Africa & bayond.

  Ila swali la msingi hapa nadhani na umbumbumbu wa legislatures wetu. Inakuwaje mbunge asijue issue/sera ya Tanzania Middle East?
   
 8. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  tuna uhusiano na Israel ila hatuna ubalozi huko wala wao hawana ubalozi hapa. Balozi wa Israel Kenya ndio anasimamia maslahi ya Israel hapa. Mambo kuwa nchi itapata laana si sahihi na mimi binafsi sipendi siasa za vitisho. Kumbuka anayetoa laana humrudia yeye, sasa hawa kwa kutishia watu sidhani kama wapo sahihi.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa muda Diplomatic issues za Israel zimekuwa zikifanyika Nairobi. Balozi wa Israel Kenya anawahudumia nchi za E/Africa pamoja na Malawi.

  Hawa walokole wameshindwa kutofauita bunge na imani zao? Na huyu Mary Mwanjelwa sio ndio tuliambiwa aliiba taulo hotelini huko Arusha? Ulokole wake unaanzia wapi na unaashia wapi?
   
 10. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,049
  Trophy Points: 280
  Inaelekea NewOrder na Kikulacho ni wajuzi wa siasa za kimataifa embu mnijuze sababu hasa za kina za sie kutokuwa na mahusiano na Israel maana wengine JF tunaichukulia kama vyuo vingine tu vinavyotoa elimu mbalimbali japokuwa hakuna cheti kinachotolewa zaidi ya kupanua uelewa wetu na ukichanganya na vyeti vyetu vya kuungaunga vya QT mpaka juu tunakuwa tupo fit.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Hata Mushama ni mtata sana!
   
 12. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu asante kwa elimu uliyonipa leo mimi nilikuwa sijui
   
 13. K

  Katufu JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 433
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Hawa wabunge wameuliza jambo la msingi sana ambalo serikali yoyote makini ilipaswa kuwa imelifanya juzi na zio jana. Maandiko matakatifu katika biblia yako wazi kuhusu kubarikiwa wale wanaibariki Israel kama taifa teule la Mungu. Na anayechaguaa ukilaani Israeli anachagua laana badala ya baraka. KWA HIYO< TANZANIA KUTOKUWA NA UHUSIANO WA KIBALOZI KAMA ILIVYOKUWA HUKO NYUMA AUTOMATICALLY IMECHAGUA LAANA. Jambo lolote laweza kutanguka lakini chochote kilichotajwa kwenye biblia lazima kitatimia tu.

  Chukua mfano wa Marekani anabarikiwa kwa sababu ya kuwa na uhusiano mzuri na Israel na kuitetea Israel. Au tuangalia jirani zetu Kenya moja ya chanzo cha mambo yao kwenda vizuri ni kutokana na wao kuwa na uhusiano mzuri na Israel. Hebu angalia Tanzania pamoja na kuwa na rasilimali nyingi kuliko Kenya kwa mbali, Tanzania bado iko hoi sana. Wenzetu mpaka wamegundua mafuta sisi bado tupo tunapiga mark time. Kumbuka hili ni suala la kiroho zaidi ambalo taathira zake kwenye uchumi na maisha jumla ya kimwili ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

  MIMI NASEMA UBALOZI WA ISRAEL NCHINI TANZANIA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ISRAEL ULITAKIWA KUWA UMEFUNGULIWA JUZI NA SIO JANA. Tanzania una nafasi ya kuchagua laana au BARAKA.
   
 14. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zanzibar lakini ina mahusiano mazuri sana tena sana na Israel, hivi nikiandika katika Hotel ya Aga Khan mjini Zanzibar wapo waandishi ya habari na Mwanadiplomasia mkubwa wa Israel
   
 15. N

  Nambombe Senior Member

  #15
  Jul 10, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini ni kweli,asiyeheshimu israel atalaaniwa na hii ni kutokana na biblia.Labda waislam watuambie quorani inasema nini kuhusu israel.
   
 16. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,148
  Likes Received: 1,882
  Trophy Points: 280
  "Hakuna aliye adui mkubwa wa waaminio (waislamu) kama wayahudi....."
   
 17. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,058
  Likes Received: 3,984
  Trophy Points: 280
  Huu ndio udini wenyewe tunaouongea sasa Waislam nao wakisema kuhusu Saudi Arabia, Mecca na Medina utawajibu nini? jamani ioneeni huruma Tanzania, tumeishi bila ya huo ubalozi na Israel sasa sioni kwanini tushindwe sasa hizi chokochoko za dini zitalipasua taifa hili! Tuwe na staha uisomavyo Biblia wewe usitake ieleweke hivyohivyo na kila mtu! Give us a brake nyie Walokole
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Bora tukosane na palestina kuliko Israel
   
 19. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #19
  Jul 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Asumpta Mshama mbunge wangu ila ni aibu............TISS huyo.......maana huku kwetu ni wachache wanaojuan kazi yake . mara ruanbiwe alikuwa mpishi wa raisi...mara Air hostess.......mara nini yaani vurugu tupu.
   
 20. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Kuwa na mahusiano mazuri na Israel si lazima tufungue ubalozi wao kwetu na wetu kwao. Kimsingi tayari tuna mahusiano mazuri na Israel kielimu ambapo tuna wanafunzi wengi wapo huko vyuo vikuu vya Tel Aviv, Jerusalem, Haifa na kwingineko nchini humo.
   
Loading...