GENERAL | |
---|---|
Salutation | Honourable |
First Name: | Assumpter |
Middle Name: | Nshunju |
Last Name: | Mshama |
Member Type: | Constituency Member |
Constituent: | Nkenge |
Political Party: | CCM |
Office Location: | Box 64, Kyaka. 21494, Dar Es Salaam |
Office Phone: | +255 783 852736/+255 752 131913 |
Ext.: | |
Office Fax: | |
Office E-mail: | amshama@parliament.go.tz |
Member Status: | Current Member |
Date of Birth Hiyo hapo juu ndo CV ya Mbunge wetu Asupmter |
Pia wapo Dodoma, wana kama eka laki moja hivi chini ya Kilimo kwanza na Bwana Dustan Mrutu. Kama utakumbuka rais alitembelea hilo shamba mwezi uliopita, wanalima mboga mboga na wanasema in 3-4 years time Tanzania (maybe kupita kwao) itakuwa ina export kwa E/Africa & bayond.
Ila swali la msingi hapa nadhani na umbumbumbu wa legislatures wetu. Inakuwaje mbunge asijue issue/sera ya Tanzania Middle East?
"Hakuna aliye adui mkubwa wa waaminio (waislamu) kama wayahudi....."
Inaelekea NewOrder na Kikulacho ni wajuzi wa siasa za kimataifa embu mnijuze sababu hasa za kina za sie kutokuwa na mahusiano na Israel maana wengine JF tunaichukulia kama vyuo vingine tu vinavyotoa elimu mbalimbali japokuwa hakuna cheti kinachotolewa zaidi ya kupanua uelewa wetu na ukichanganya na vyeti vyetu vya kuungaunga vya QT mpaka juu tunakuwa tupo fit.
Kwa muda Diplomatic issues za Israel zimekuwa zikifanyika Nairobi. Balozi wa Israel Kenya anawahudumia nchi za E/Africa pamoja na Malawi.
Hawa walokole wameshindwa kutofauita bunge na imani zao? Na huyu Mary Mwanjelwa sio ndio tuliambiwa aliiba taulo hotelini huko Arusha? Ulokole wake unaanzia wapi na unaashia wapi?
Leo katika kipinsi cha maswali na majibu Mbunge wa Nkenge Asumpta Mshama na Mery Mwanjelwa (CCM), wameitaka Serikali itoe Maelezo kwa nini haijafungua Ubalozi nchini Israel kwani kutofanya hivyo ni kuikosea biblia na Tanzania itapata laana.
Kutokana na hali hiyo Wabunge hawa hawajajua msimamo wa Serikali ya Tanzania kwani inatambua kuwa Palestina ni Taifa huru na ndiyo maana nchi yetu katu haitafungua ubalozi katika nchi ya Israel na Lebanon kutokana na uonevu unaofanywa kwa chuki za kidini, hivyo hawa wabunge kuna kila chembe ya dalili ya kutumwa na makuadi wa Israel kwa kuwasemea kupitia Bunge.
Ni vema wawe wanasoma kwanza wabunge wetu kabla ya kukupuka na hoja butu.
naomba tuheshimiane humu kwa imani zetu, unapouponda ulokole ukidhani unamponda Marry mwanjelwa ujue kwamba ni wengi unatuboa, pia elewa kuwa Marry kasema kwa maoni yake basi na ww utoe yako na sio kuattack mawazo ya mtu.
Hawa wabunge wameuliza jambo la msingi sana ambalo serikali yoyote makini ilipaswa kuwa imelifanya juzi na zio jana. Maandiko matakatifu katika biblia yako wazi kuhusu kubarikiwa wale wanaibariki Israel kama taifa teule la Mungu. Na anayechaguaa ukilaani Israeli anachagua laana badala ya baraka. KWA HIYO< TANZANIA KUTOKUWA NA UHUSIANO WA KIBALOZI KAMA ILIVYOKUWA HUKO NYUMA AUTOMATICALLY IMECHAGUA LAANA. Jambo lolote laweza kutanguka lakini chochote kilichotajwa kwenye biblia lazima kitatimia tu.
Chukua mfano wa Marekani anabarikiwa kwa sababu ya kuwa na uhusiano mzuri na Israel na kuitetea Israel. Au tuangalia jirani zetu Kenya moja ya chanzo cha mambo yao kwenda vizuri ni kutokana na wao kuwa na uhusiano mzuri na Israel. Hebu angalia Tanzania pamoja na kuwa na rasilimali nyingi kuliko Kenya kwa mbali, Tanzania bado iko hoi sana. Wenzetu mpaka wamegundua mafuta sisi bado tupo tunapiga mark time. Kumbuka hili ni suala la kiroho zaidi ambalo taathira zake kwenye uchumi na maisha jumla ya kimwili ni kubwa kuliko unavyoweza kufikiri.
MIMI NASEMA UBALOZI WA ISRAEL NCHINI TANZANIA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ISRAEL ULITAKIWA KUWA UMEFUNGULIWA JUZI NA SIO JANA. Tanzania una nafasi ya kuchagua laana au BARAKA.
Wewe ni msomi wa wapi? daima katika mjadala wowote kinachotakiwa kuwa "attacked" ni mawazo na hoja za mtu na sio mtu mwenyewe. Sasa wewe unataka tofauti yake?naomba tuheshimiane humu kwa imani zetu, unapouponda ulokole ukidhani unamponda Marry mwanjelwa ujue kwamba ni wengi unatuboa, pia elewa kuwa Marry kasema kwa maoni yake basi na ww utoe yako na sio kuattack mawazo ya mtu.
Huu ndio udini wenyewe tunaouongea sasa Waislam nao wakisema kuhusu Saudi Arabia, Mecca na Medina utawajibu nini? jamani ioneeni huruma Tanzania, tumeishi bila ya huo ubalozi na Israel sasa sioni kwanini tushindwe sasa hizi chokochoko za dini zitalipasua taifa hili! Tuwe na staha uisomavyo Biblia wewe usitake ieleweke hivyohivyo na kila mtu! Give us a brake nyie Walokole
Tanzania kuvunja ubalozi na Israel sio kwasababu nyingine zaidi ya uonevu unaofanywa na Israel la kutaka na bado inaendelea kuiondoa Taifa la ki PALESTINA fatlikia kinachoendelea uko utashangaa km kweli Taifa linalojiona teule linaweza kufanya hivyo...Swala sio udini kwani ata Israel penyewe ukristu ni kiduchu sana.....Try to read the following data below:
Religion affiliation of Israel population as of 2011 was:
- 75.5% Jewish
- 16.7% Muslim
- 2.1% Cristian
- 1.7% Druze
Kwa uzoefu wangu, wayahudi wanaongoza kwa ubaguzi. Na si kwa waislamu tu. Hawa jamaa ni wabaguzi sana. Fuatilia news uone hatua wanazochukua kukabiliana na wahamiaji kutoka Africa. Sina taarifa kuhusu nchi nyingine yeyote yenye sera mbaya namna hiyo kwa wahamiaji. Nikifuatilia mwenendo ya Taifa hili na watu wake, nina mashaka kuwa hili ni taifa teule. Na kwamba eti, tusipokuwa na mahusiano ya kibalozi na nchi hii tutalaaniwa. This is utterly nonsense at best. Mahusiano na taifa lolote lile hapa duniani hayapaswi kuwa kwa misingi ya kidini. Ni makosa makubwa kufanya hivyo. Hata ukizingatia dini, Wayahudi si waisilamu wala wakristo. And remember, religions are evil. You just look at the evidences.