Mbunge asema wanaume wakubali hawana nguvu za kiume

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,800
Kutokana na wanaume wengi kuwa na matatizo ya nguvu za kiume, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema),Susan Lyimo ameishauri Serikali ya Tanzania kutoa elimu ya sababu ya baadhi ya wanaume kutokuwa na mbegu zenye nguvu ili kunusuru ndoa.

mbungepic.jpg

Susan Lyimo

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) nchini Tanzania, Susan Lyimo ameishauri Serikali ya nchi hiyo kutoa elimu ya sababu ya wanaume kutokuwa na mbegu zenye nguvu ili kunusuru ndoa.

Susan ametoa ushauri huo wakati kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilipokuwa ikipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake jana Jumatatu Januari 20, 2020.

“Kwa kweli ndoa nyingi sana zinavunjika. Na ndoa hizi zinavunjika kwa sababu ya watu kutopata watoto, tatizo hili lilikuwapo lakini linaongezeka,” alisema Lyimo.

Alisema kwa sababu ya mfumo dume walikuwa wanasema mwanamke ndiye mwenye tatizo lakini sasa hivi tatizo hilo limegeuka kwa wanaume.

“Wanaume nao wakubali kwa sababu nao wana tatizo. Mimi nilikuwa nadhani kuna haja ya kutoa elimu tuone nini sababu za wanaume kutokuwa na mbegu zisizokuwa na nguvu ili wake zao ama wanawake zao wapate watoto,” amesema.

Amesema kama wakienda kupima vinasaba watakuta watoto wengi sana baba zao sio kwa sababu baada ya mwanamke kuambiwa kuwa hazai anaamua kuchepuka ili apate mtoto.

“Kuna haja ya kutoa elimu ili kuhakikisha tunanusuru hizi ndoa kwa sababu. Mimi kama mshauri naletewa matatizo makubwa zaidi. Wanajinusuru kuogopa kupewa talaka,” alisema ambaye ni waziri kivuli wa elimu, sayansi na teknolojia

Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndungulile alisema changamoto ni kubwa sana na kwamba Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam imeanza maandalizi ya kutoka huduma ya ugumba.

“Tafiti duniani zinaonyesha kuwa kwa miaka 50 kumekuwa na punguzo la asilimia 50 ya nguvu za kiume. Nilikuwa nasoma tafiti moja inasema katika miaka 50 ijayo basi wanaume wote hapa tutakuwa hamna kitu,” alisema.

Alitaja visababishi kuwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, aina ya maisha na vyakula.

Hata hivyo, Dk Ndungulile alisema si kweli watoto wengi wanabambikiwa baba kwa sababu wanaokwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ni wale wenye hofu vya kuwa watoto si wao.

Alisema hata wale wenye hofu na kwenda kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupima ni chini asilimia 50 ndio wanagundua kuwa wamebambikiziwa watoto.

Chanzo: Mwananchi
 
Namna nguvu zinazosemwa sio kweli hata kidogo. Yani tatizo la wanaume ni kumaliza moja then mpaka baada ya siku 3 na kuendelea ila sio kweli kuwa hatuna nguvu za kurutubisha.

Pili,idadi ya wanawake ni kubwa sana na wanatuchukua kuanzia wakiwa na miaka 18 na kuendelea ila sisi ni kuanzia 25+ sasa hata ukiangalia takwimu wanawake sana ni wengi kuliko wanaume nina amini hata tukisema tuoe wake watatu kila mmoja bado watabaki ila swali ni je,tutaoa vipi na nguvu za kuwarizisha Hakuna?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Botha ambaye alikuwa rais wa Afrika Kusini wakati wa utawala wa Wazungu, waliwahi kusema ukitaka kumpoteza kabisa Mwafrika Mweusi, mpe pesa, pombe, mwanamke, mziki nk. Kwa kifupi mpe Starehe kwa wingi.
Tatizo la ugumba kwa Mwanaume Mweusi wa Kiafrika ni kufanya tendo la ndoa wakati wa ujana kama vile mlo wa kila siku na kwa hiyo kupunguza ufanisi wake siku za utu uzima kipindi ambacho anatakiwa kuzaa.
Waafrika wakati wa ujana tunatumia tendo la ndoa kuzidi kiasi na kusababisha kuuchosha mwili na kuleta uchakavu mkubwa na uzee tungali vijana.
Viungo vya mwili vikitumika bila kuzingatia kanuni za afya wakati wa ujana, zinaleta athari za kiafya kwenye umri wa utu uzima.
Tatizo la ugumba halipo kwa asilimia kubwa kwa wazungu kama ililivyo kwa mtu mweusi kwa sababu, wazungu walio wengi kwao kufanya tendo la ndoa hovyo hovyo ni fedheha wakati kwa mswahili ni fahari.
 
Kweli CHADEMA mmeishiwa Sera! Yaani mbunge mzima anakosa hoja ya kuongelea wananchi wa jimbo lake anaanza kuongelea ngono? Kwani huyu mbunge kaishatembea na wanaume wangapi wakakosa kumsimamishia mpaka kuleta takwimu? Uenda hana mvuto kiasi kwamba faragha yake haimvutii mwanaume kusimamisha ndo anaanza kuwatolea povu mabaharia. Kama ni kweli mbona ongezeko la watu linapanda mpaka kufikia karibia million 60? Wanaume tunafanya kazi yetu Bwana! ZeroIQ huko wapi? Huu uzi unakuhusu!
 
Mbona kachanganya madesa? Nguvu za kiume na ugumba ni vitu viwili tofauti kabisaa japo mtu anaweza akawa navyo vyote kwa pamoja
Hajui kuwa mtu anaweza kuwa na nguvu za kiume ila asiweze kutungisha mimba na mwingine ana tatizo la nguvu za kiume na akatungisha mimba vizuri tu... Yeye alipaswa kupewa elimu hii kwanza
 
Namna nguvu zinazosemwa sio kweli hata kidogo. Yani tatizo la wanaume ni kumaliza moja then mpaka baada ya siku 3 na kuendelea ila sio kweli kuwa hatuna nguvu za kurutubisha.

Pili,idadi ya wanawake ni kubwa sana na wanatuchukua kuanzia wakiwa na miaka 18 na kuendelea ila sisi ni kuanzia 25+ sasa hata ukiangalia takwimu wanawake sana ni wengi kuliko wanaume nina amini hata tukisema tuoe wake watatu kila mmoja bado watabaki ila swali ni je,tutaoa vipi na nguvu za kuwarizisha Hakuna?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umetumia sensa ya mwaka gani kuwa wanaume hata wakioa wake watatu bado wanawake watabaki?
 
Namna nguvu zinazosemwa sio kweli hata kidogo. Yani tatizo la wanaume ni kumaliza moja then mpaka baada ya siku 3 na kuendelea ila sio kweli kuwa hatuna nguvu za kurutubisha.

Pili,idadi ya wanawake ni kubwa sana na wanatuchukua kuanzia wakiwa na miaka 18 na kuendelea ila sisi ni kuanzia 25+ sasa hata ukiangalia takwimu wanawake sana ni wengi kuliko wanaume nina amini hata tukisema tuoe wake watatu kila mmoja bado watabaki ila swali ni je,tutaoa vipi na nguvu za kuwarizisha Hakuna?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo hapo unapinga mbunge au unaungana na Mbunge?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom