Mbunge anapotumia muda mwingi kutoa shukrani

Makene

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,475
282
Je utaratibu huu wa mbunge kabla ya kutoa mchango wake anakuwa na orodha ndefu ya watu wa kuwapa shukrani, nashukuru mtoto wangu mdogo, nashukuru bla bla.
Je haya ndiyo mambo wananchi wanahitaji kusikia toka kwa wawakilishi wao pale bungeni?
 
Hata mwenyekiti kaliona hilo na kalisemea lakini mchangiaji anadai ni kuonewa wivu. Sisi kama watazamaji salamu hizo zinatu bore saana. kama msululu wa salamu aliokuwa nao Ghasia asubuhi ni kero. Anakumbushia hadi msiba mbichi wamama yake Anne - alitaka amuone anatiririsha machozi sijui!!!!!!!!
 
Huku ni kutumia muda vibaya.......shukrani naziita time stealer.... maana kuna wabunge mpaka leo wanampongeza makinda kwa kuwa spika..... that is crap......wananchi hatutaki kusikia mambo ya kurudia rudia kila siku.........
 
Bunge halina kanuni. Angalia mabunge ya wenzetu full itifaki, hakuna huu upuuzi. Ukitaja kujua hilo chukua mfano mdogo tu siku Hu Jin Tao , presidaa wa China siku alipokuwa pale national stadium akifungua uwanja, ilikuwa ni aibu kwa mawaziri wetu. yaani mara huyu anasoma messeji kwenye simu mara wanapiga stori. Lakini wachina walikuwa na nidhamu ya hali ya juu, hata hotuba zao hazikuwa na upuuzi mwingi wa kutaka kumshukuru kila mtu mpaka mtoto wako.
 
mbunge wa magamba anashukuru, anatambulisha wageni wake wawili watatu, analaumu maandamano na migomo kisha anaunga mkono hoja anakaa anasubiri posho huku amelala na kutoka udenda kidogo siku imeenda. wamefanya hivyo kwa karibu miaka 50 sasa.
 
kizazi cha bongofleva mpaka bungeni kutajana majina tuuuu na shukrani inaudhi kweli hawa ghasia katumia dk kumi nzima anashukuru tuuuu wakati hotuba yake mbovuuu no mshahara kuongezwa.
 
Je utaratibu huu wa mbunge kabla ya kutoa mchango wake anakuwa na orodha ndefu ya watu wa kuwapa shukrani, nashukuru mtoto wangu mdogo, nashukuru bla bla.
Je haya ndiyo mambo wananchi wanahitaji kusikia toka kwa wawakilishi wao pale bungeni?

Hili tatizop nafikiri liko kuanzia ngazi za juu maana kama mawaziri wanatumia mpaka hotuba za bajeti kushukuru usitegemee mbunge aache kutumia njia hiyo hiyo
Ilitakiwa kwenye issue kama bajeti kusiwe na kitu kama hicho ila ndo hivyo wanatumia muda kuwashukuru mpaka watoto wao
 
kizazi cha bongofleva mpaka bungeni kutajana majina tuuuu na shukrani inaudhi kweli hawa ghasia katumia dk kumi nzima anashukuru tuuuu wakati hotuba yake mbovuuu no mshahara kuongezwa.

unamaana wanapaishana mpk maproducer RA, papaa mkwele, papaa ngeleja, pededjeeee masha
 
Ina nikumbusha baadhi ya nyimbo za densi ambazo badala ya kutoa ujumbe mwimbaji anatumia muda mwingi zaidi kutaja majina. Mwisho wa siku hata madhumuni ya wimbo unakuwa hauoni. Ni aibu na ina chekesha.
 
namuangalia Tundu Lissu akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais, kaanza na points straight!! kwa wapambanaji kama hawa hawana muda wa kupoteza ila wana magamba dakika wanazopewa kuchangia hoja ni nyingi sana kwao ndio maana wanaanza kutaja majina hadi ya vimada wao katika shukrani+mipasho+vijembe
 
Je utaratibu huu wa mbunge kabla ya kutoa mchango wake anakuwa na orodha ndefu ya watu wa kuwapa shukrani, nashukuru mtoto wangu mdogo, nashukuru bla bla.
Je haya ndiyo mambo wananchi wanahitaji kusikia toka kwa wawakilishi wao pale bungeni?

Ni jambo la kupoteza muda, kwa kuwa hawana hoja. Halina maana kabisa. Nimemsikia Spika akiwaambia msipoteze muda kwa kupongezana, lakini haya majitu hayasikii.
 
[h=6]Wanakera sana hawa! Nilikuwa naangalia Bunge kwenye Tv Mbunge anatoa salam bungeni kwa mjukuu wake anayedai ndo anajifunza kuzungumza eti kila akimuona kwenye televisheni, anasema "aona babu Malole kwenye Tv" unauma sana kugawa muda wetu kwa salamu za kinafiki[/h]
 
huku ni kukosa uzalendo na kukosa hoja , wabunge wengi wa magamba hawafanyi utafiti kabla ya kungea na hata ukiwasikiliza utaona hoja zao ni dhaifu. ili kupoteza muda wanaanza na salamu zisizo na kichwa wala mkia ili mradi waonekane wameongea, kisha uorodhesha mrorongo wa matatizo ya jimbo lake na baadaye wanaunga mkono 100%.

Inahitajika sheria kalina spika mzalendo ili kukomesha ujinga huu
 
Mm huwa siwaelewagi pale wa kushukuriwa ni wananchi peke yake hayo mengine fanyia ndani kwako ccm kuna baadhi ya wabunge ni hewa sana ,
 
mbunge wa magamba anashukuru, anatambulisha wageni wake wawili watatu, analaumu maandamano na migomo kisha anaunga mkono hoja anakaa anasubiri posho huku amelala na kutoka udenda kidogo siku imeenda. wamefanya hivyo kwa karibu miaka 50 sasa.
Inauma sana ndugu yangu!hii inaashiria ni kiasi gani wabunge wetu hawataki kwenda majimboni,badala yake pongezi zote zinatolewa mjengoni!ni upuuzi!
 
Back
Top Bottom