Mbunge alia mbele ya waziri

Mbunge alia mbele ya waziri

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
MBUNGE wa Masasi mkoani Mtwara, Mariam Kasembe (CCM) jana alimwaga machozi mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alipotembelea kuona uharibifu wa mali na nyumba za mbunge huyo zilizochomwa na wananchi mapema mwaka huu. Waziri Maghembe ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara ya siku tano kukagua miradi ya maji, alifika nyumbani kwa mbunge jana asubuhi, kabla ya kwenda Wilaya ya Nanyumbu.

Mariamu alianza kumwaga chozi baada ya Waziri Maghembe na msafara wake, kufika mbele ya nyumba yake iliyoteketezwa kwa moto na wakati wa vurugu zilizotokea mwaka huu.

“Mheshimiwa waziri kama unavyoona, hii ndiyo hasaraniliyopata, nyumba yote imekwisha naisha maisha kama mkimbizi.

“Mali zangu zimeharibika unaona ile trekta pale haina kazi, gari langu limebaki vyuma chakavu… nina wakati mgumu kurudi katika hali ya kawaida,”alisema Mariamu huku akilia.

Alisema mpaka sasa baadhi ya wanafamilia wake wanaishi kwenye kontena ambalo liko ndani ya uzio wa nyumba yake ambayo imebaki gofu.

“Ninyi waandishi mbona mnapita hili kontena, hii ni nyumba yangu jamani ipigeni picha…namuachia Mungu,”alisema Mariamu ambaye alifuatana na mume wake.

Naye Waziri Maghembe aliwaomba viongozi wa Halmashauri ya Masasi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi kutafuta kila aina ya njia kumsaidia mbunge huyo.
 
Wale ambao hawana pa kukaa nao wasaidiwe na nani? Hao viongozi wa halmashauri wawasaidie wananchi ambao hawana kipato mbunge mshahara na marupurupu vinamtosha.
 
MBUNGE wa Masasi mkoani Mtwara, Mariam Kasembe (CCM) jana alimwaga machozi mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alipotembelea kuona uharibifu wa mali na nyumba za mbunge huyo zilizochomwa na wananchi mapema mwaka huu. Waziri Maghembe ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara ya siku tano kukagua miradi ya maji, alifika nyumbani kwa mbunge jana asubuhi, kabla ya kwenda Wilaya ya Nanyumbu.

Mariamu alianza kumwaga chozi baada ya Waziri Maghembe na msafara wake, kufika mbele ya nyumba yake iliyoteketezwa kwa moto na wakati wa vurugu zilizotokea mwaka huu.

“Mheshimiwa waziri kama unavyoona, hii ndiyo hasaraniliyopata, nyumba yote imekwisha naisha maisha kama mkimbizi.

“Mali zangu zimeharibika unaona ile trekta pale haina kazi, gari langu limebaki vyuma chakavu… nina wakati mgumu kurudi katika hali ya kawaida,”alisema Mariamu huku akilia.

Alisema mpaka sasa baadhi ya wanafamilia wake wanaishi kwenye kontena ambalo liko ndani ya uzio wa nyumba yake ambayo imebaki gofu.

“Ninyi waandishi mbona mnapita hili kontena, hii ni nyumba yangu jamani ipigeni picha…namuachia Mungu,”alisema Mariamu ambaye alifuatana na mume wake.

Naye Waziri Maghembe aliwaomba viongozi wa Halmashauri ya Masasi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi kutafuta kila aina ya njia kumsaidia mbunge huyo.

Hata wangeongozana na mtoto wa mkulima na M/kiti wake!
Hii kauli piga tu piga wanainchi haijawatoka Mioyoni mwao!
Na itawapeleka katika histori ya kwamba kulikuwepo na chama kijani tu a.k.a ccm mafisadi.
Mwaka 2015 si mbali kwa uweza wa Mungu mwenye mamlaka!
 
Angetoa machozi hayo kulilia wananchoi wanaoteseke na mipango mibovu na uonevu wa chama chake angekuwa mzalendo

Rejea wananchi wale wanaonyweshwa sumu jirani na migodi na kutoka magamba

Rejea wananchi wanaochomewa nyumba zao kuwahamisha kwa ubabe kupisha wawekezaji huko Loliondo
Orodha ni ndefu

Mh. Mbunge asubiri kiinua mgongo chake ajenge nyumba nyingine, nasi wananchi huumia pale anapopiga makofi na vigeregere vya kishabiki kwa hoja mfu na zenye kukera zitolewazo na aidha waziri. Naibu waziri au mbunge wa kimagamba pale bungeni

Huwa wananchi tunaumia sana ila hawa magamba hawajui tu, sasa 2015 ndio wataijua hasira yetu ya kiukweli

Wakati huo huyu Zombi alieamrisha wananchi kupigwa atakuwa amestaaf hapo tutakuwa tunaiadhibu CCM
 
Kama hakutakuwa na haki wengi tutalia, hizo ni dalili tu. Pole sana mama.
 
Funda nyondo, ujumbe umeifikia ccm, through mbunge wa kupendelewa. Vema sana wana mtwara, you done excellent.

Halafu bado mpuuzi mwingine anasema Halmashauri ifanye jitihada za kumtafutia namna ya kuishi licha ya mshahara na marupurupu mengine ya Ubunge! Ubongo wake umeshindwa kuvuta hisia za waTanganyika kwa mamilioni wanaoishi bila kuijua kesho yao, halafu bado huyo Mbunge apewe upendeleo maalum na Halmashauri! Watu wengine sijui huo u-Prof wanautumiaje!
 
Kama hakutakuwa na haki wengi tutalia, hizo ni dalili tu. Pole sana mama.

Kiongozi!

Hakuna cha pole wala nini. Kikombe hicho wanastahili kukinywa kabisa. Na bado, ni suala la muda tu!
 
Huyu mama hajielewi na kama anajielewa angechukua utaratibu wa kuomba hifadhi ya kudumu pale magogoni.

Badala ya kuungana na wananchi wanaodai haki ya wao kutambuliwa ili kupata maisha bora yeye anaenda kulia kwa Mkoloni mweusi??
Akijengewa hiyo nyumba halafu ikaja ikachomwa tena ataenda kulia kwa nani??? Pinda wengine, sufuriA
 
Hilo ni funzo kuwa wawe wanatanguliza maslahi ya umma mbele halaf chama baadae, kama wasipofanya hayo wajue hawapo salama kwani wamezungukwa na umma wa watanzania ambao wanateseka kutokana na sera mbovu za ccm
 
Kiongozi!

Hakuna cha pole wala nini. Kikombe hicho wanastahili kukinywa kabisa. Na bado, ni suala la muda tu!
Sawa, ndio maana nimesema watu kama nyinyi mkiongezeka, tutalia wengi, labda hata wewe mwenyewe. Ndio maana Dk Slaa anasisitiza uwepo wa haki, ndipo amani ya kweli itapatikana. Sio amani magumashi. Nakwambia kweli tutaumia wengi. Labda kama wewe huna kitu kabisa. Mpe pole huyo mama.
 
Kwa jinsi nilivyo pigika sina cha kupoteza. Kwangu naona anastahili hicho kikombe, maana kwa mfumo walio uchagua kutuongoza, wengi tunalia na kusaga meno. Ngoja nao wahisi maumivu.
 
MBUNGE wa Masasi mkoani Mtwara, Mariam Kasembe (CCM) jana alimwaga machozi mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alipotembelea kuona uharibifu wa mali na nyumba za mbunge huyo zilizochomwa na wananchi mapema mwaka huu. Waziri Maghembe ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara ya siku tano kukagua miradi ya maji, alifika nyumbani kwa mbunge jana asubuhi, kabla ya kwenda Wilaya ya Nanyumbu.

Mariamu alianza kumwaga chozi baada ya Waziri Maghembe na msafara wake, kufika mbele ya nyumba yake iliyoteketezwa kwa moto na wakati wa vurugu zilizotokea mwaka huu.

“Mheshimiwa waziri kama unavyoona, hii ndiyo hasaraniliyopata, nyumba yote imekwisha naisha maisha kama mkimbizi.

“Mali zangu zimeharibika unaona ile trekta pale haina kazi, gari langu limebaki vyuma chakavu… nina wakati mgumu kurudi katika hali ya kawaida,”alisema Mariamu huku akilia.

Alisema mpaka sasa baadhi ya wanafamilia wake wanaishi kwenye kontena ambalo liko ndani ya uzio wa nyumba yake ambayo imebaki gofu.

“Ninyi waandishi mbona mnapita hili kontena, hii ni nyumba yangu jamani ipigeni picha…namuachia Mungu,”alisema Mariamu ambaye alifuatana na mume wake.

Naye Waziri Maghembe aliwaomba viongozi wa Halmashauri ya Masasi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi kutafuta kila aina ya njia kumsaidia mbunge huyo.

Mkuki kwa nguruwe eeeeh,je wale wanaoishi kwenye mahema kutokana na mabomu ya mbagala,gongolamboto na mafuriko walioko mwabepande nao wamlilie nani?hayo ni matokeo ya serikali dhaifu ya ccm
 
MBUNGE wa Masasi mkoani Mtwara, Mariam Kasembe (CCM) jana alimwaga machozi mbele ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe alipotembelea kuona uharibifu wa mali na nyumba za mbunge huyo zilizochomwa na wananchi mapema mwaka huu. Waziri Maghembe ambaye yupo mkoani hapa kwa ziara ya siku tano kukagua miradi ya maji, alifika nyumbani kwa mbunge jana asubuhi, kabla ya kwenda Wilaya ya Nanyumbu.

Mariamu alianza kumwaga chozi baada ya Waziri Maghembe na msafara wake, kufika mbele ya nyumba yake iliyoteketezwa kwa moto na wakati wa vurugu zilizotokea mwaka huu.

“Mheshimiwa waziri kama unavyoona, hii ndiyo hasaraniliyopata, nyumba yote imekwisha naisha maisha kama mkimbizi.

“Mali zangu zimeharibika unaona ile trekta pale haina kazi, gari langu limebaki vyuma chakavu… nina wakati mgumu kurudi katika hali ya kawaida,”alisema Mariamu huku akilia
.

Alisema mpaka sasa baadhi ya wanafamilia wake wanaishi kwenye kontena ambalo liko ndani ya uzio wa nyumba yake ambayo imebaki gofu.

“Ninyi waandishi mbona mnapita hili kontena, hii ni nyumba yangu jamani ipigeni picha…namuachia Mungu,”alisema Mariamu ambaye alifuatana na mume wake.

Naye Waziri Maghembe aliwaomba viongozi wa Halmashauri ya Masasi na Mkuu wa Wilaya hiyo, Farida Mgomi kutafuta kila aina ya njia kumsaidia mbunge huyo.

Mbona kiranja wake aliposema wapigwe tu hakukemea na badala yake alimshangilia na kugonga meza. Na wao watambue kuwa wananchi waliowapa hizo nafasi wanafika mahali na wao wanachoka.

Liwalo na liwe; kama mbwai na iwe mbwai.
 
Wajifunze kuwa na bima,mtu anapesa anashindwa kukata bima ya mali.angekuwa ame insure hiyo nyumba saizi angekuwa anachekelea tu.
 
Back
Top Bottom