Mbunge alia mbele ya waziri

Mbunge alia mbele ya waziri

Angetoa machozi hayo kulilia wananchoi wanaoteseke na mipango mibovu na uonevu wa chama chake angekuwa mzalendo

Rejea wananchi wale wanaonyweshwa sumu jirani na migodi na kutoka magamba

Rejea wananchi wanaochomewa nyumba zao kuwahamisha kwa ubabe kupisha wawekezaji huko Loliondo
Orodha ni ndefu

Mh. Mbunge asubiri kiinua mgongo chake ajenge nyumba nyingine, nasi wananchi huumia pale anapopiga makofi na vigeregere vya kishabiki kwa hoja mfu na zenye kukera zitolewazo na aidha waziri. Naibu waziri au mbunge wa kimagamba pale bungeni

Huwa wananchi tunaumia sana ila hawa magamba hawajui tu, sasa 2015 ndio wataijua hasira yetu ya kiukweli

Wakati huo huyu Zombi alieamrisha wananchi kupigwa atakuwa amestaaf hapo tutakuwa tunaiadhibu CCM
Jamani tumwonee huruma,huyu ni kutokana na huko aliko a.k.a kijani ila ni mtu mzuri haikupaswa kufanyiwa hivi wananchi walivyomtenda.
 
mmbunge asaidiwe na Halmashauri? Je akina mama wanaojifungulia chini au kwa kibatari?
Zile posho anapeleka wapi?
 
Mbunge huyu aache wengine wawakilishe wananchi asilete machozi yake
 
Bora yy kachomewa nyumba na gari,
Mbona hawasei wananchi wake waliobakwa na Askari
Walioteswa kwa kupigwa,
Walioibiwa mali zao,wake zao.
 
Kama inasikitisha hivi japo nashindwa kukusaidia mheshimiwa Mbunge maana orodha ya wanaolala nje kwa ufisadi wa chama chako ni ndefu sana,hivyo vumilia tu maana hauko peke yako,wapo wengi walikuwa wanataka msaada kabla hata hujafanyiwa hivyo visa lkn hukuweza kuwasaidia hata kwa kuinua tu mdomo.......hembu jionee na wewe jinsi inauma ukikosa msaada kwa uliowategemea.
 
mmbunge asaidiwe na Halmashauri? Je akina mama wanaojifungulia chini au kwa kibatari?
Zile posho anapeleka wapi?

Jamani hilo lilikuwa ni wazo tu na siyo amri ukizingatia ni mbunge mwenzake tena wa chama chake. Kumsaidia mtu aliyeumia siyo vibaya hata kama mtu huyo ni adui yako. Pamoja ubunge inawezekana ana mikopo inayohitaji mrejesho kwa hiyo tusiwe wakali sana. Ni kweli wananchi wana hasira na ni maskini zaidi, lakini hata maskini aweza kumsaidia maskini mwingine. Kutoa ni moyo ...

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Atoe hela ya mfukoni mwake, kuiingiza halmashauri kwenye huruma ya moyo wake ni ----- tu.
Angitisha harambee bungeni kama kaguswa sana


Hujui serikalini bosi akisema ni amri?

Jamani hilo lilikuwa ni wazo tu na siyo amri ukizingatia ni mbunge mwenzake tena wa chama chake. Kumsaidia mtu aliyeumia siyo vibaya hata kama mtu huyo ni adui yako. Pamoja ubunge inawezekana ana mikopo inayohitaji mrejesho kwa hiyo tusiwe wakali sana. Ni kweli wananchi wana hasira na ni maskini zaidi, lakini hata maskini aweza kumsaidia maskini mwingine. Kutoa ni moyo ...

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Angetembelewa na Jk sijui ingekuaje..! nadhani ndo angelia hadi angevaa chupi kichwani.. shit sana..
 
----- tu hilo li mamaa tumechoka liwalo na liwe jk
 
Magamba yakiwafika huwa wanakuwa wapole sana,hapo ndiyo utasikia neno "tuko pamoja" na kutafuta huruma.Wakiwa kwenye viyoyozi sasa!!!!?????
 
Sawa, ndio maana nimesema watu kama nyinyi mkiongezeka, tutalia wengi, labda hata wewe mwenyewe. Ndio maana Dk Slaa anasisitiza uwepo wa haki, ndipo amani ya kweli itapatikana. Sio amani magumashi. Nakwambia kweli tutaumia wengi. Labda kama wewe huna kitu kabisa. Mpe pole huyo mama.

amani ya kweli hailetwi bila haki kwa wote... haki ya kusikilizwa, kuheshimiwa km binaadam nk. huletwa na sera sahihi zilizopo nchini pindi haya hayatafanyika ieleweke matokeo yake ndio haya.... hata ukiyaitaje hata uyakemee vipi au uwauwe wasiothaminika na dola hayatakoma mpaka kuwepo na usawa wa haki ya msingi wa ubinaadam... unapo tenda shuruti kwa binaadam mwenzio unamgeuza kuwa mnyama... matokeo ya Mtwara ni matokeo ya kiutendaji
 
Analia nini hao si ndio mabingwa wa kuisifia ccm hiyo ndio mood ya nchi nzima dhidi ya watawala wa ccm.
 
Hiyo ndiyo nguvu ya wananchi mama yangu , bora wamekuachia roho yako .
 
weka picha ya hiyo nyumba iliyoharibiwa
 
Inawezekana wananchi waliona huyu si mbunge wao bali ni wa CCM, anapitisha maamuzi yanayo wakandamiza na kuwanyonya bila ridhaa yao. Sasa waliamua kumshikisha adabu ili akome. Kama alipitisha kodi ya simu ni lazima huyu si mtetezi wa wananchi na alistahili adhabu hiyo!
 
I concur with you.Sasaa,Kama waliomchagua hapo ndipo walipofika,si aachie ngazi.Anamwakilisha nani Bungeni sasa.Dah! Hawa jamaa wana ujasiri wa kipepo aisee.
Wale ambao hawana pa kukaa nao wasaidiwe na nani? Hao viongozi wa halmashauri wawasaidie wananchi ambao hawana kipato mbunge mshahara na marupurupu vinamtosha.
 
Tatizo ni gap kubwa lililopo kati ya maskini na tajiri.
 
pole zake....ndio wakome kuwageuza wananch mifugo.
 
Ndiyo wajue wanainchi wana hasira zaidi ya wajuavyo!


Hiyo ni tela tu!
Alie tu...zile kauli zao za "ndiyooooooooooooooooooooooo!"...haya ndo matokeo yake.Wabunge wetu hata wajibu wao hawaujui,wanafikiri kazi yao ni kuitetea serikali.Sasa wananchi wakiamua kujitetea wanalia nini!
 
Back
Top Bottom