Mbunge ajaye wa Mbeya Mjini, Sugu, kusikika Clouds TV 23/11/2023

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,722
218,278
Screenshot_2023-11-22-23-37-15-1.png

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mbunge ajaye wa Mbeya Mjini, Mfanyabiashara, Mwekezaji wa Kimataifa, Bilionea Joseph Mbilinyi, asubuhi ya 23/11 /23, atakuwepo kwenye Clouds TV kwa mahojiano Maalum.

Usibadili Channel kwa Mawe Matakatifu.
 
Pumbavu Bilionea unawajua wewe?

Ila Mbowe sijui alikupa chai gan
Huyu mleta mada ndio alinifanya mimi nikubali kuwa uchawi upo japo siuamini.

Sababu huyu mleta mada ni mtu smart sana kiasi kwamba sio rahisi mwanasiasa uchwara aina ya Mbowe aweze kuimiliki akili yake, na fikra zake bila kutumia ndumba. I mean kijana alianza kwanza kulogwa ili iwe rahisi kutumiwa katika chama kama hivi.

Hata hivyo makamu mwenyekiti wake ameshakataa chama chao kuingia katika uchaguzi mkuu kupitia tume hii. Sasa huyo sugu wake sijui atakuwa mbunge kupitia chama gani, labda chauma au nccr mageuzi.
 
Sugu hawezi kushindana na msomi na mwanasheria nguli. Mbeya mjini siyo jimbo la wahuni .sugu apeleke uhuni wake huko na ubabaishaji wake huko. Amekaa miaka kumi bungeni lakini ukimuuliza ni kipi anajivunia na alama aliyoiacha pale Mbeya huwezi ukaonyweshwa hata kwa tochi.

Sugu hana chake tena Mbeya mjini. Hakuna mwenye akili Timamu anayeweza kumpigia kura. labda vichaa na wendawazimu ndio wanaweza kumpigia kura lakini kwa bahati mbaya ni kuwa hakuna anayeweza ruhusu vichaa wapige kura. kwa hiyo sugu akae kwa kutulia tu maana hatapata tena ubunge mbele ya Dr Tulia Rais wa IPU anayeangaliwa na kutizamwa na Dunia nzima.
 
Mbunge ajaye bila Tume Huru na Katiba
Mpya?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hii ndio hali halisi katika chama cha ukoo wa kambale 👇

M/mwenyekiti: Hatuingii katika uchaguzi bila tumehuru na katiba mpya.

Mwenyekiti: Tutaingia katika uchaguzi hata kwa tume hii na katiba hii hii.

Ukiangalia kwa makini hayo maelezo yao hapo juu, utagundua kuwa kila mtu ana malengo yake.

Kwa upande wa Lisu (yeye ni mbinafsi) , anaamini kuwa yeye atakuwa mgombea uraisi wa Chadema. Hivyo akiingia kugombea uraisi kupitia tume na katiba hii, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuangukia pua, hivyo kujikuta anakosa uraisi na pia hatoweza kuwa mbunge kama wenzake kina Mbowe, Lema nk, ambao watakuwa wanapokea maburungutu ya mishahara ya ubunge huku yeye aking'aa ng'aa sharubu tu mitaani. Hivyo anaona ni afadhali amshawishi mwenyekiti wasiingize chama kwenye uchaguzi mkuu, ili kama kukosa wakose wote kuanzia ubunge na uraisi.

Kwa upande wa mwenyekiti yeye anaamini katika uhai wa chama. Anaona kama ataendelea kususia chaguzi zingine zinazokuja kwa kigezo cha kutaka tumehuru na katiba mpya, basi kuna uwezekano wa chama hicho kupoteza wanachama wengi ambao hawatokubali kuona chama hicho kinaendelea kukaa tena miaka mitano bila wabunge bungeni.

Wengi wataamua kwenda CCM, ACT Wazalendo, CUF, NCCR nk ili kupata nafasi za kugombea ubunge na nafasi zingine katika chaguzi.

Kumbuka Chadema ni chama kikubwa, hivyo kinahitaji hela kujiendeleza (na sio kutegemea michango ya wanachama ambao 75% ni masikini kila siku mikutanoni), hivyo ni lazima kiingie katika uchaguzi hata kama hawatoshinda uraisi lkn kishinde wabunge kadhaa ambao watasaidia kuki busti chama kupitia ruzuku na ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kila mwezi na chama.

Kwa sasa hivi swala la tumehuru na katiba mpya, kamwe haliwezekani hata iwe kwa maandamano au kwa kususia uchaguzi. Hivyo mwenyekiti anaona ni bora chama kiingie hivyo hivyo ili kukinusuru na hasa ukizingatia makamu wake ni mtu wa mguu nje mguu ndani. Anajifanya anapambania chama, alaf akiona mambo yanakwenda mrama anakimbilia zake ulaya na kumuacha mwenyekiti apambane kivyake kukirudisha chama kwenye mstari.

Mambo yakishakaa sawa chamani, ndo anarudi tena kutoka ulaya na mikwara yake.
 
Sugu hawezi kushindana na msomi na mwanasheria nguli. Mbeya mjini siyo jimbo la wahuni .sugu apeleke uhuni wake huko na ubabaishaji wake huko.amekaa miaka kumi bungeni lakini ukimuuliza ni kipi anajivunia na alama aliyoiacha pale Mbeya huwezi ukaonyweshwa hata kwa tochi.

Sugu hana chake tena Mbeya mjini.hakuna mwenye akili Timamu anayeweza kumpigia kura. labda vichaa na wendawazimu ndio wanaweza kumpigia kura lakini kwa bahati mbaya ni kuwa hakuna anayeweza ruhusu vichaa wapige kura. kwa hiyo sugu akae kwa kutulia tu maana hatapata tena ubunge mbele ya Dr Tulia Rais wa IPU anayeangaliwa na kutizamwa na Dunia nzima
John Sigwemisi Malecela aliyekuwa Waziri Mkuu aliangushwa kwa kishindo na Lusinde
 
Hii ndio hali halisi katika chama cha ukoo wa kambale

M/mwenyekiti: Hatuingii katika uchaguzi bila tumehuru na katiba mpya.

Mwenyekiti: Tutaingia katika uchaguzi hata kwa tume hii na katiba hii hii.

Ukiangalia kwa makini hayo maelezo yao hapo juu, utagundua kuwa kila mtu ana malengo yake.

Kwa upande wa Lisu (yeye ni mbinafsi) , anaamini kuwa yeye atakuwa mgombea uraisi wa Chadema. Hivyo akiingia kugombea uraisi kupitia tume na katiba hii, kuna uwezekano mkubwa wa yeye kuangukia pua, hivyo kujikuta anakosa uraisi na pia hatoweza kuwa mbunge kama wenzake kina Mbowe, Lema nk, ambao watakuwa wanapokea maburungutu ya mishahara ya ubunge huku yeye aking'aa ng'aa sharubu tu mitaani. Hivyo anaona ni afadhali amshawishi mwenyekiti wasiingize chama kwenye uchaguzi mkuu, ili kama kukosa wakose wote kuanzia ubunge na uraisi.

Kwa upande wa mwenyekiti yeye anaamini katika uhai wa chama. Anaona kama ataendelea kususia chaguzi zingine zinazokuja kwa kigezo cha kutaka tumehuru na katiba mpya, basi kuna uwezekano wa chama hicho kupoteza wanachama wengi ambao hawatokubali kuona chama hicho kinaendelea kukaa tena miaka mitano bila wabunge bungeni.

Kumbuka Chadema ni chama kikubwa, hivyo kinahitaji hela kujiendeleza (na sio kutegemea michango ya wanachama ambao 75% ni masikini kila siku mikutanoni), hivyo ni lazima kiingie katika uchaguzi hata kama hawatoshinda uraisi lkn kishinde wabunge kadhaa ambao watasaidia kuki busti chama kupitia ruzuku na ile michango waliokuwa wanakatwa wabunge kila mwezi na chama.

Kwa sasa hivi swala la tumehuru na katiba mpya, kamwe haliwezekani hata iwe kwa maandamano au kwa kususia uchaguzi. Hivyo mwenyekiti anaona ni bora chama kiingie hivyo hivyo ili kukinusuru na hasa ukizingatia makamu wake ni mtu wa mguu nje mguu ndani. Anajifanya anapambania chama, alaf akiona mambo yanakwenda mrama anakimbilia zake ulaya na kumuacha mwenyekiti apambane kivyake kukirudisha chama kwenye mstari.
Hilo la Lissu na ubinafsi hebu tuliweke pembeni, ni mawazo yako binafsi pia.

Hili la Chadema ni chama kikubwa, kinahitaji pesa kujiendesha hivyo lazima kishiriki uchaguzi, kwasababu hapo watapata ruzuku na michango ya wabunge kwaajili ya shughuli za chama, naona hapo ndio umeandika pointi.

Lakini, hiyo pointi yako nakuja kuipinga kwasababu walishatuambia wana kitu kinaitwa Chadema digital, kwamba walikuwa na mpango wa kuwaandikisha wanachama milioni moja au zaidi nchi nzima, kisha hawa wanachama watapolipia kadi zao, basi chama kitapata pesa za kujiendesha, huu mpango wao sijui uliishia wapi.

Hapo utaona kwamba, Chadema na mapato sio lazima kushiriki uchaguzi, wana njia nyingine tofauti, kwangu mimi nionavyo zaidi, kushiriki uchaguzi kunakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa mbunge binafsi, zaidi ya chama chao, au hata majimbo wanayo bahatika kushinda.

Kwa kukung"ata sikio , Chadema Digital imeandikisha wanachama mil 15 waliolipia kadi zao kwa vitita vizito sana .
 
Back
Top Bottom