Mbunge afanya mambo ya aibu kuhujumu uchaguzi wa UVCCM - Muleba

Kobe123

Member
Jul 4, 2023
82
216
Katika hali isiyo ya kawaida, mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini amejitanabaisha kama mtu ambaye ameingilia uchaguzi wa katibu wa hamasa Wilaya ya Muleba. Huu ni mwendelezo wa matendo ya kubaka haki na kuingilia utendaji kazi wa jumuiya.

Hii habari imeanza hivi:

Mwenyekiti wa Vijana wa Wilaya alimteua mtu ambaye aliona atafanya naye kazi. Wajumbe wote wakampitisha kwa moyo mmoja.

Baada ya siku kadhaa, ikagundulika kuwa mbunge hakumkubali kijana aliyechaguliwa na baraza. Baada ya muda kupita, ukapenyezwa mlungula mmoja wa hatari kwenda kamati ya mkoa.

Ambapo inasemekana mwenyekiti wa mkoa alipewa milioni 1 na katibu akapewa laki 3.

Watu hawa baada ya kupata fedha hiyo wakaamua kusema kuwa hawamkubali mtu aliyeteuliwa, basi wakaona wamwagize mwenyekiti wa wilaya aitishe baraza na kuteua mtu mwingine.

Vijana wamegomea uchaguzi huo kurudiwa kabisa, kiasi kwamba ikapelekwa fedha ya kutosha ili wakubali maamuzi hayo ya kihuni. Katibu wa mbunge alionekana akituma watu wagawe shilingi elfu kumi kwa kila kijana ili wabadili maamuzi.

Kwa kanuni za CCM, katibu wa mkoa sio mjumbe wa baraza la wilaya, lakini amekomaa kuanzia usiku akiwa amelala nyumbani kwa katibu wa vijana wilaya.

Mpaka sasa, watu wanaoratibu huu uhuni ni mwenyekiti wa vijana mkoa, katibu wa vijana mkoa, katibu wa CCM wilaya, katibu wa vijana wilaya, na mbunge wa Muleba Kusini.

Ambapo mpaka sasa, akidi ya kikao haikutimia, wanabebwa watu ambao hata sio wajumbe, wanalazimishwa wasaini mahudhurio ili kubariki uhuni.

Vijana wanaingiliwa maamuzi yao, huku mbunge akisema lolote like lazima aihujumu jumuiya.

Ni vyema uongozi wa juu wa taifa ukaamua kuingilia jambo hili.

Pia ni vyema chama kikamuita kwenye kikao cha maadili mbunge wa Muleba Kusini kwa kuendelea kuratibu genge linalovuruga uhai wa CCM ndani ya Wilaya Muleba.
 
Back
Top Bottom