Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MBUNGE AESHI HILALY MGENI RASMI KAMATI YA CCM KATA YA MAFULALA
Kata ya Mafulala iliyopo Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa leo imefanya mkutano mkuu wa CCM Kata na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Mh. Aeshi Hilaly Khalfan.
Mheshimiwa Aeshi akiwa katika kikao hicho ameeleza mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa JMTZ Mh. Samia Suluhu Hassan juu ya ufanikishaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Jimbo la Sumbawanga Mjini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Barabara za kiwango cha Lami zilivyojengwa, ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Sumbawanga mjini na matazamio ya ujenzi wa hospital ya Rufaa.
Kwa kipekee Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini ameunga mkono juhudi za ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Mafulala kwa kuchangia Mabati pamoja na mbao ili kukamilisha ujenzi huo.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-07-23 at 19.53.59.jpeg52.8 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-23 at 19.54.01.jpeg57.3 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-23 at 19.54.06.jpeg59.5 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-23 at 19.54.25.jpeg55.2 KB · Views: 2
-
WhatsApp Image 2023-07-23 at 19.54.26.jpeg57.4 KB · Views: 2