MBUGA YA TAIFA YA BURIGI CHATO.
Leo 13:15pm,06/07/2019.
Burigi Chato ni hifadhi ya Taifa iliyopandishwa hadhi awamu ya nne na kuwa Mbuga ya Taifa.
Burigi Chato ni eneo zuri sana kihifadhi na kitalii linalonogeshwa na mandhari nzuri ya miti ya chini na juu, majani mapana mafupi na marefu na ya kijani pamoja na Ziwa kubwa linalofanya hifadhi kuwa na uhakika wa maji ya kunywa kwa viumbe hai vinavyopatikana mbugani humo.Ni hifadhi iliyocheleweshwa kutambulishwa sawa sawa na Selous Game Reserve ambayo dunia inahifahamu kama Mbuga kubwa ya pili duniani.
Mbuga ya Burigi Chato haina tofauti sana na Mbuga ya Saadani,Mbuga ya Saadani imezungukwa na bahari lakini Mbuga ya Burigi Chato inalo Ziwa la asili Ziwa Burigi.
Ziwa Burigi ni Ziwa la nane kwa ukubwa kwa Tanzania baada ya Ziwa Victoria,Ziwa Tanganyika,Ziwa Nyasa,Ziwa Rukwa,Ziwa Eyasi,Ziwa Natron,Ziwa Manyara,Ziwa Burigi,Ziwa Balangida,Ziwa Jipe,Ziwa Babati,Ziwa Ambussel,Ziwa Chala.
Katika Ziwa Burigi utapata kuwaona viboko wakiogelea,ndege wazuri pembeni ya Ziwa na Wanyama mbalimbali wakinywa maji,
Mbuga ya Burigi Chato iliyojaa wanyama adimu kabisa kama Simba,Chui,Twiga,Tembo,Nyati,Kifaru,Swala,Pundamilia na aina ya ndege mia tatu inaanzia sehemu ya Kwimba,Mwamala linapita kahama,Bukombe,Mbogwe,Geita,Kakonko,Biharamulo hadi Chato.
Burigi Chato ipo muda mrefu,miaka mingi sana lilikuwa pori kubwa linalotambulika,kuanzia Chato,Kimisi,Kasindaga,Karagwe hadi Kigoma.
Ucheleweshwaji wa kulipandisha hadhi pori hili kuwa Mbuga kulifanya wakimbizi toka nchi jirani kukimbilia kwenye msitu huo kuua tembo,Simba,Chui,Twiga, Nyani na kuchukua kila walichokikuta kwenye msitu huo.
Kutambulika rasmi kwa hifadhi ya Taifa kulisaidia kulinda maliasili za pori hilo,na sasa hifadhi hiyo imekuwa Mbuga ya Taifa hili ni jambo la kupongezwa sana,na kujivunia maliasili nyingi tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu,
Mwenyezi Mungu ametujaalia mapori makubwa yenye wanyama wazuri japo binadamu nao ujificha humo kufanya ujambazi,Kufanyika hifadhi na kutoa uangalizi wa mapori hayo kutawapa ulinzi wanyama waliopo kwenye mapori hayo.
Hali ya hewa ya ukanda wa Kagera hadi Chato ina mvua za misimu mitatu ya mvua kwa mwaka hivyo ukame ni nadra sana kutokea katika ukanda huo. Na kwa sababu ya kuwa upande wa magharibi wa ziwa Victoria, upepo unaovuma kuelekea nchi kavu unasafirisha hewa yenye umajimaji.
Kijiografia Upepo unaovuma kutoka magharibi mwa ukanda wa Kagera hadi Chato kwenda mashariki, unakuwa na mvuke kutoka msitu mkubwa wa Kongo. Na kutokana na ziwa kuna mawingu ya Cb (Cumuloninbus) yanayo leta mvua nyingi inayo ambatana na radi siku 215 kwa mwaka katika sehemu hizo za Chato na Kagera kwa ujumla.
Majani na miti hubaki ya kijani (evergreen ) mwaka mzima.Hizi ndizo baraka za Mungu na urithi wa dunia tuliojaaliwa Watanzania.
#Karibu Mbuga ya Burigi-Chato.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.