Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe amesema kibano wanachokipata wapinzani kutoka Serikalini kinatokana na hofu waliyonayo viongozi wa chama tawala cha CCM.
Amesema hofu hiyo inatokana na CCM kuhofia kushindwa kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020 kwa Chadema kuibuka mshindi na kuongoza dola.
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alitoa kauli hiyo Jumamosi Mei 4 wakati anazindua tawi maarufu la Chadema la Urusi lililopo Mwanga mjini Kigoma.
Alisema viongozi na wanachama wa CCM wana hofu ya kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao, hivyo kuamua kuzuia mikutano ya hadhara na kuhakikisha viongozi wa vyama vya upinzani wanafunguliwa kesi mahakamani kila uchao.
"CCM wapo hoi, wamelegea wameishiwa mbinu za kisiasa ndio maana vyama vya upinzani vinapata kibano kwa viongozi wake kukamatwa, kupigwa na hata kuumizwa," alisema Mbowe.